Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naiandika Makala fupi yenye mighani mifupi inayotafakarika na kubayanishika.
Baada ya uchaguzi wa 2020 vyama vya upinzani viliibuka na malalamiko na matamko kadha wa kadha wakilalamikia mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi mkuu 2020.
Walidai kwamba wakurugenzi ambao Ni wateule wa Rais hawakutenda haki katika zoezi Hilo na kwamba walipokea maelekezo ya kuiba na kupora kura za wapinzani, na waliwatangaza wagombea wa ccm kwa nguvu ya mamlaka zilizo juu.
Kwa hali hiyo walidai kwamba hawatajihusisha na Jambo lolote la serikali iliyopatikana kwa Kura za wizi na walidai serikali na bunge vyote havina uhalali kabisa.
Mtakumbuka moja ya cyama Cha upinzani kilidai hakitawaruhusu wabunge wa viti maalum kuhudhuria Wala kutambuliwa na bunge batili.
Kwa mkitadha huo walimaanisha kwamba wabunge wote wa ccm walio bungeni Ni batili kwa sababu walitangazwa kwa Kura za wizi.
Baada ya siku kadhaa tume ya uchaguzi ilitoa orodha ya majina ya wabunge 19 wa viti maalumu, lakini katibu wa chadema Bwn JJ Mnyika alitoa taarifa kwa umma ya kwamba chama chake hakitambui orodha hiyo na kilishatoa msimamo wa kutoshiriki bunge la wabunge waliopatikana kwa Kura za wizi, yaani wabunge wote wa chama Cha mapinduzi.
Licha ya mvutano wote huo bado wabunge hao 19 waliapishwa na hata Sasa Ni wabunge wa chadema ambayo inapokea ruzuku kutokana na kuwepo kwao bungeni.
Hivi Sasa ninapoandika makala haya,
Nimeona mivutano baina ya viongozi wa chadema na spika wa bunge Mh. J Ndugai yakizuka na hii ni baada ya kifo Cha aliyekuwa Rais wa JMT, Hayati JP Magufuli.
Hii Ina maana gani?
Kwamba Sasa wapinzani wanadhani Mh. Rais Samia Ni dhaifu Sana asiyeweza kupambanua hoja zao za siri, na kwamba watamfanya usigundue kwamba atakuwa anakubaliana na hoja yao ya kwamba uchaguzi mkuu 2020 ccm iliiba kura na kwamba serikali yake na bunge havina uhalali na Ni batili.
Haya tutayaona mara tu Mh. Rais atakapokubaliana na maombi yao kivuli yaliyo na agenda ya kutaka kumdhalilisha baadae, endapo ataamuua kumshauri spika wa bunge na kupokea hoja za chadema za kuwavua ubunge, ndipo tutakapowaona wakiibuka na ajenda yao halisi ya kwamba Hilo bunge Sio halali maana hata Rais mwenyewe kakubaliana hoja ya kwamba wabunge wa ccm walitangazwa kwa Kura za wizi.
Hata wale wabunge wa ccm wanaosisitiza kwamba maamuzi ya chadema yaheshimiwe wanakosea bila wao wenyewe kujua kwamba wanaunga mkono hoja ya chadema juu ya kutangazwa kwa Kura za wizi.
Chadema wafanye Nini?
1. Wanapaswa kumeza kauli zao za awali kwamba Kura ziliibiwa na wakili hadharani kwamba uchaguzi huo 2020 walipoteza kihalali.
2. Waibuke na hoja yao Sasa ya kwamba wabunge wanaoketi bungeni kwa tiketi ya chadema na mahakama Sio wabunge halali kwa sababu majina yao hayakuwasilishwa na chama kwenye ofsi ya tume.
Lakini wafute kabisa hoja ya kutoshiriki bungeni kwa kisingizio Cha kuibiwa kura, maana watakuwa wakimtukana Rais huku wakiomba msaada wake.
Naitwa Mtemi Nyakarungu
0754459572