Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Wakuu Salaam,

Jana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi kuna kauli alizitoa ambazo binafsi naona hakupaswa kuzitoa hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mtu mwenye nguvu na mamlaka na dhamana kubwa kabisa kwa sasa ndani ya JMT.

Jambo la kwanza alionyesha kushangazwa na vitendo vya matapeli wa kwenye mitandao ya simu ilhali sote tumesajiliwa kwa alama za vidole, jambo hili ni kweli linatushangaza wengi inakuaje hawakamatwi na kushughulikiwa kirahisi na bado wanaendelea, lakini yeye kwa nafasi na mamla aliyonayo alitakiwa kusimama kwenye zamu na nafasi yake kwanza kwa kuonyesha kutoridhishwa na kufutahishwa na jinsi watendaji wanavyoshughulikia swala hilo na pili atoe maelekezo ya nini anataka kuona kinafanyika tena haraka, lakini si kusema tu kuwa na yeye anashangaa, swali linabaki kuwa uongozi wake juu ya jambo hili ni upi?

Jambo la pili ni kuhusu kesi za kubambikiza, ameonyesha kuridhishwa na TAKUKURU kufuta kesi nyingi ambazo wameona hazikua sahihi, halafu akawaambia Polisi wajitafakari. Kama kiongozi liko tatizo ameliona ilikua jambo zuri angeonyesha alichokiona kisha atoe maelekezo ya utekelezaji, mfano ili kupunguza msongamano wa wafungwa JPM hakumwambia DPP ajitafakari bali alimwagiza aende magerezani aonane na mahabusi ili aone kesi za kufuta lakini pia azungumze na watu walio tayari kulipa fedha waachiwe. Hadi akafikia hatua ya kusema hayo ina maana yako mambo ambayo yeye ameyaona ambayo inawezekana watendaji wa maeneo husika either hawajayaona au wanayaona ni ya kawaida, sasa kiongozi kama mbeba maono jukumu lake ni kuwaonyesha yale anayoyaona na kuwaelekeza wayafanye.

Kama mimi kila siku ninapotoka nyumbani kwangu napita mlangoni kwa kupiga sarakasi, ukiniona ukashangaa kuwa nafanya kitu cha ajabu halafu ukaniambia nijitafakari wakati mimi naona ni kitu cha kawaida, usitegemee kuona mabadiliko.

Mama usishangae, kama sisi wananchi tusio na mamlaka, wewe ndiye kiongozi wetu uliye mbele yetu, toa maelekezo, kemea, amrisha mambo yaende.
Rais anaomba polisi waangalie kuhusu PF-3. Mheshimiwa toa amri hiyo PF-3 ifutwe, kwanza taratibu hii haikuwekwa na bunge, ni utaratibu wa ovyo.
 
... hoja nzuri! "Kushangaa kwa Rais" kimsingi sio kushangaa kwa kawaida kwa maana ya halisi ya neno hilo; kushangaa kwa Rais ni onyo na maelekezo kwa mwenye kufikiri. Waliozoea "stata mzuka" za "nimtumbue, nisimtumbueee"; "tumbuaaa" bila kushirikisha ubongo au kujali utawala wa sheria sembuse "haki ya kusikilizwa" wanadhani Rais anashangaa.
Mwalimu wa rais sasa alishawahi kushangaa kwanini Tanzania masikini wakati ni rais,itakuwa huyu?

Naomba mfikishieni nahitaji kununua LUKU maana imegoma tokea juzi
 
... ni kazi ya Rias kuuza umeme?
 
Sahihi kabisa mkuu
 
Mbona yule mwingine alikuwa anashangaa kana kwamba nchi ilitawaliwa na chadema?
 
Wakuu Salaam,

Jana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi kuna kauli alizitoa ambazo binafsi naona hakupaswa kuzitoa hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mtu mwenye nguvu na mamlaka na dhamana kubwa kabisa kwa sasa ndani ya JMT.

Jambo la kwanza alionyesha kushangazwa na vitendo vya matapeli wa kwenye mitandao ya simu ilhali sote tumesajiliwa kwa alama za vidole, jambo hili ni kweli linatushangaza wengi inakuaje hawakamatwi na kushughulikiwa kirahisi na bado wanaendelea, lakini yeye kwa nafasi na mamla aliyonayo alitakiwa kusimama kwenye zamu na nafasi yake kwanza kwa kuonyesha kutoridhishwa na kufutahishwa na jinsi watendaji wanavyoshughulikia swala hilo na pili atoe maelekezo ya nini anataka kuona kinafanyika tena haraka, lakini si kusema tu kuwa na yeye anashangaa, swali linabaki kuwa uongozi wake juu ya jambo hili ni upi?

Jambo la pili ni kuhusu kesi za kubambikiza, ameonyesha kuridhishwa na TAKUKURU kufuta kesi nyingi ambazo wameona hazikua sahihi, halafu akawaambia Polisi wajitafakari. Kama kiongozi liko tatizo ameliona ilikua jambo zuri angeonyesha alichokiona kisha atoe maelekezo ya utekelezaji, mfano ili kupunguza msongamano wa wafungwa JPM hakumwambia DPP ajitafakari bali alimwagiza aende magerezani aonane na mahabusi ili aone kesi za kufuta lakini pia azungumze na watu walio tayari kulipa fedha waachiwe. Hadi akafikia hatua ya kusema hayo ina maana yako mambo ambayo yeye ameyaona ambayo inawezekana watendaji wa maeneo husika either hawajayaona au wanayaona ni ya kawaida, sasa kiongozi kama mbeba maono jukumu lake ni kuwaonyesha yale anayoyaona na kuwaelekeza wayafanye.

Kama mimi kila siku ninapotoka nyumbani kwangu napita mlangoni kwa kupiga sarakasi, ukiniona ukashangaa kuwa nafanya kitu cha ajabu halafu ukaniambia nijitafakari wakati mimi naona ni kitu cha kawaida, usitegemee kuona mabadiliko.

Mama usishangae, kama sisi wananchi tusio na mamlaka, wewe ndiye kiongozi wetu uliye mbele yetu, toa maelekezo, kemea, amrisha mambo yaende.
Mkuu 'Itoye', nikiri hapa, sijawahi kukusoma humu JF.

Kutokana na mchango wako huu, wewe siyo mtu wa kupuuzwa, ni mtu mwenye uelewa.

Uliyoeleza hapa ni kweli tupu, pamoja na kwamba yanaonekana kulenga kwenye kumkandia rais kwa uongozi wake, hasa hilo la kwanza kuhusu simu, ni 'petty issue', lakini ujumbe wako bado unasimama kuwa kweli.

Ni dhahiri ulipenda mtindo wa uongozi wa Magufuli, na ungependa mama naye atumie aina hiyo ya uongozi, kitu ambacho hakiwezekani.

Kwa hiyo, pamoja na kukubaliana nawe hapa kumsihi mama avute soksi katika uongozi wake, baadhi ya wasomaji wako watakuona kwamba wewe ni shabiki tu wa marehemu Magufuli.

Kuna uzuri wa aina ile ya uongozi kwenye baadhi ya mambo, lakini usisahau pia kwamba namna hiyo ya kufanya maamuzi nako pia kuna udhaifu wake; na ni kutokana na ubaya wa aina ile ya uongozi iliyofanya Magufuli aonekane kuwa mbaya kwenye maeneo kadhaa ya maamuzi yake.

Nitaendelea kukusoma, kwa maana naona unacho kina cha kutosha.
 
Naona wengi wanalisema hilo. Huenda lina ukweli ndani yake. Lakini kingine huenda ndio personality ya Mama. Sio rahisi akabadilika na kuwa mkali. Tathmini ya kufanya ni kuangalia je hayo anayoyataja yanafanyiwa kazi? Hilo ndio muhimu.
"Tathmini ya kufanya ni kuangalia je hayo anayoyataja yanafanyiwa kazi"?

Kama anao wasaidizi wanaomkusanyia taarifa muhimu popote zinapopatikana, wakikosa kumfikishia ushauri huo, hao wasaidizi watakuwa wanamwangusha sana.

Siku siyo nyingi. Miaka minne ni muda mfupi sana.

Asipokuwa mwangalifu atajikuta hakufanya lolote katika muda huo.
 
Mwalimu wa rais sasa alishawahi kushangaa kwanini Tanzania masikini wakati ni rais,itakuwa huyu?

Naomba mfikishieni nahitaji kununua LUKU maana imegoma tokea juzi
'misasa'!

Mtu hatari sana, bila ya kuonekana kuwa ni hatari!

'Stealth'
 
Mama anatumia akili kuliko kutumia nguvu! Mbona Mwendazake pamoja na ukali wake kwa nini Wizi wa mitandao ulishamiri?
 
Baada ya kusikia eti mapapai Yana Corona nilijua Kuna watu wanaenda kuharibiwa feature zao tuombe mama wakumbuke watu Hawa walioonewa. Poleni wataalamu wetu lakini Mungu ni mwema.
 
uzi utapigwa ban sio mda,wanao mpenda watakuja kufanya figisu
 
Wakuu Salaam,

Jana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi kuna kauli alizitoa ambazo binafsi naona hakupaswa kuzitoa hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mtu mwenye nguvu na mamlaka na dhamana kubwa kabisa kwa sasa ndani ya JMT.

Jambo la kwanza alionyesha kushangazwa na vitendo vya matapeli wa kwenye mitandao ya simu ilhali sote tumesajiliwa kwa alama za vidole, jambo hili ni kweli linatushangaza wengi inakuaje hawakamatwi na kushughulikiwa kirahisi na bado wanaendelea, lakini yeye kwa nafasi na mamla aliyonayo alitakiwa kusimama kwenye zamu na nafasi yake kwanza kwa kuonyesha kutoridhishwa na kufutahishwa na jinsi watendaji wanavyoshughulikia swala hilo na pili atoe maelekezo ya nini anataka kuona kinafanyika tena haraka, lakini si kusema tu kuwa na yeye anashangaa, swali linabaki kuwa uongozi wake juu ya jambo hili ni upi?

Jambo la pili ni kuhusu kesi za kubambikiza, ameonyesha kuridhishwa na TAKUKURU kufuta kesi nyingi ambazo wameona hazikua sahihi, halafu akawaambia Polisi wajitafakari. Kama kiongozi liko tatizo ameliona ilikua jambo zuri angeonyesha alichokiona kisha atoe maelekezo ya utekelezaji, mfano ili kupunguza msongamano wa wafungwa JPM hakumwambia DPP ajitafakari bali alimwagiza aende magerezani aonane na mahabusi ili aone kesi za kufuta lakini pia azungumze na watu walio tayari kulipa fedha waachiwe. Hadi akafikia hatua ya kusema hayo ina maana yako mambo ambayo yeye ameyaona ambayo inawezekana watendaji wa maeneo husika either hawajayaona au wanayaona ni ya kawaida, sasa kiongozi kama mbeba maono jukumu lake ni kuwaonyesha yale anayoyaona na kuwaelekeza wayafanye.

Kama mimi kila siku ninapotoka nyumbani kwangu napita mlangoni kwa kupiga sarakasi, ukiniona ukashangaa kuwa nafanya kitu cha ajabu halafu ukaniambia nijitafakari wakati mimi naona ni kitu cha kawaida, usitegemee kuona mabadiliko.

Mama usishangae, kama sisi wananchi tusio na mamlaka, wewe ndiye kiongozi wetu uliye mbele yetu, toa maelekezo, kemea, amrisha mambo yaende.
Ni kama sukuma gang bado mna wenge na style ya utawala wa mwendazake
 
Mama mpole mno

Wenzetu wa kutoka visiwani ndio hulka yao ni watu wenye busara wasiotaka papara! Nakumbuka hata Mwalimu Nyerere aliwahi kumsihi Alhaji Mzee Mwinyi kuwa alikuwa mpole sana hivyo alimshauri AONGEZE UKALI KIDOGO!!!

Mpeni muda mama Samia mtaona mambo mazuri! Anapowapa muda Viongozi kujitafakari maana yake ni kwamba ameona dosari mahari na hivyo anawapa muda wahusika kujirekebisha kabla ya yeye kuchukua hatua . Huo ni muda unaompa yeye nafasi ya kuchunguza na kupata ukweli wa jambo husika badala ya kukurupuka na kutoa uamuzi kama mlivyozoeleshwa!
 
Mama mungu akujaalie uwe na maamuzi sahihi wakati sahihi. Problem solution oriented na sio na na wewe uwe bado kwenye mchakato nchi hii michakato bado haimalizikagi.

Tofuati ya mwenda zake na maraisi wengine magufuli alikuwa anatoa solution bila.kuona aibu wala kupepesa macho.
 
Wakuu Salaam,

Jana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi kuna kauli alizitoa ambazo binafsi naona hakupaswa kuzitoa hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mtu mwenye nguvu na mamlaka na dhamana kubwa kabisa kwa sasa ndani ya JMT.

Jambo la kwanza alionyesha kushangazwa na vitendo vya matapeli wa kwenye mitandao ya simu ilhali sote tumesajiliwa kwa alama za vidole, jambo hili ni kweli linatushangaza wengi inakuaje hawakamatwi na kushughulikiwa kirahisi na bado wanaendelea, lakini yeye kwa nafasi na mamla aliyonayo alitakiwa kusimama kwenye zamu na nafasi yake kwanza kwa kuonyesha kutoridhishwa na kufutahishwa na jinsi watendaji wanavyoshughulikia swala hilo na pili atoe maelekezo ya nini anataka kuona kinafanyika tena haraka, lakini si kusema tu kuwa na yeye anashangaa, swali linabaki kuwa uongozi wake juu ya jambo hili ni upi?

Jambo la pili ni kuhusu kesi za kubambikiza, ameonyesha kuridhishwa na TAKUKURU kufuta kesi nyingi ambazo wameona hazikua sahihi, halafu akawaambia Polisi wajitafakari. Kama kiongozi liko tatizo ameliona ilikua jambo zuri angeonyesha alichokiona kisha atoe maelekezo ya utekelezaji, mfano ili kupunguza msongamano wa wafungwa JPM hakumwambia DPP ajitafakari bali alimwagiza aende magerezani aonane na mahabusi ili aone kesi za kufuta lakini pia azungumze na watu walio tayari kulipa fedha waachiwe. Hadi akafikia hatua ya kusema hayo ina maana yako mambo ambayo yeye ameyaona ambayo inawezekana watendaji wa maeneo husika either hawajayaona au wanayaona ni ya kawaida, sasa kiongozi kama mbeba maono jukumu lake ni kuwaonyesha yale anayoyaona na kuwaelekeza wayafanye.

Kama mimi kila siku ninapotoka nyumbani kwangu napita mlangoni kwa kupiga sarakasi, ukiniona ukashangaa kuwa nafanya kitu cha ajabu halafu ukaniambia nijitafakari wakati mimi naona ni kitu cha kawaida, usitegemee kuona mabadiliko.

Mama usishangae, kama sisi wananchi tusio na mamlaka, wewe ndiye kiongozi wetu uliye mbele yetu, toa maelekezo, kemea, amrisha mambo yaende.
Hii ni kweli ...nilitegemea mama ajue tatizo lipo wapi na atoe maelekezo ya kuchukuliwa hatua kwa wabambikizaji....Pia atoe amri kali kwa Polisi kulifanyia kazi ndani ya muda maalum na kumletea ripoti ili achukue hatua....sasa kujitafakari kwa mbongo sana sana ni kwenda kupiga vyombo na vitu kama hivyo
 
Back
Top Bottom