Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Sawa Bashite tumekuelewa hata sabaya nae alikua mthubutu vilevile na akaenda kwenye media kujinadi

Ila kaa ukijua kwa namna yeyote ile kunasiku utalipia dhuluma uliyowafanyia watanzania, mauaji na uhalifu ulioutekeleza

Nabii G.Lema alishakutabiria tunasubiri wakati tu ila hukumu yako ipo njiani. Itakuwaje sijui lakini inakuja
 
Hakuna mtanzania ambae amezoea kufanya dhuluma atapenda kiongozi mwenye calliber ya Paul Makonda ataeuliwe. Maana akiteuliwa tu kila dhuluma inakufa.


Sisi ni mashahhidi kuwa Paul Makonda ni mmoja wa viongozi ambao alipambana kuhakikisha haki inapatikana Dar na Tanzania nzima kwa ujumla. Dhuluma kwa maskini hata wanyonge zilikwama. Leo hii wapenda ufisadi na dhuluma wanampiga vita.

Huu ndio wakati mama Samia kuwarudisha wale akina Makonda ambao wamewekwa benchi na sasa wapambe wa mafisadi wanannza ngebe.

My take: Huu ndio wakati wa kupambana na dhuluma.
Makonda ni gaidi, muhuni na tapeli kama Sabaya tu, siku yake inakuja! Atahukumiwa bila huruma![emoji1787]
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Akumbuke kulipa madani ya ndani ndiyo yanainua uchumi sababu za awamu ya 5 eti wanahakiki madeni nizakipuuzi
 
Hivi kweli kama mtu ana uwezo wa kusoma elimu ya juu kwa kujilipia ada hii si ingekuwepo toka alipoanza kindagate.

watu mnakurupuka na mawazo ya kuwabana watanzania hata sehemu zisizostahiki, leo hii unampatia mkopo mtoto wa kitanzania kwa ajili ya malazi na mlo tu na hali ya watanzania walio wengi hali mnazitambua.

Haituingii akilini kama alishindwa kusoma shule zenye mazingira na elimu bora kwenye walimu bora kama inavyofikirika (private schools) itawezekanaje kulipa ada ya mamilioni kwa elimu ya juu ukizingatia mama na baba kipato ni duni.

Kwa mwaka huu 2021elimu ya juu nadhani imelengwa kwa washua tuu mimi gharama ya mamilioni sidhani ka nitaimudu labda system ibadilike kwa mwendo huu hali ni mbaya.

Mama aliangalie hili na kubadili hii system ya utoaji mkopo wa elimu ya juu.mimi binafsi sijui nianzie wapi kwa hili.
 
Hivi kweli kama mtu ana uwezo wa kusoma elimu ya juu kwa kujilipia ada hii si ingekuwepo toka alipoanza kindagate.watu mnakurupuka na mawazo ya kuwabana watanzania hata sehemu zisizostahiki,leo hii unampatia mkopo mtoto wa kitanzania kwa ajili ya malazi na mlo tu na hali ya watanzania walio wengi hali mnazitambua.Haituingii akilini kama alishindwa kusoma shule zenye mazingira na elimu bora kwenye walimu bora kama inavyofikirika(private schools) itawezekanaje kulipa ada ya mamilioni kwa elimu ya juu ukizingatia mama na baba kipato ni duni.Kwa mwaka huu 2021elimu ya juu nadhani imelengwa kwa washua tuu mimi gharama ya mamilioni sidhani ka nitaimudu labda system ibadilike kwa mwendo huu hali ni mbaya.Mama aliangalie hili.
Rais mkweli asiyeyumhishwa,mifano ni mingi moja ni hili la machinga, Rais alisema Machinga ni mradi kamili
 
Waswahili Wana kamsemo: mnyonge mnyongeni, HAKI yake mpeni. Mama Samia Suluhu apongezwe kwa Miradi inavyoendelea kama ilivyoachwa na mtangulizi wake.

Nafurahia kuona barabara za Mwendokasi zinavyoendelea kujengwa kwa kasi nzuri, flyovers n. k.

NAWAS
 
Waswahili Wana kamsemo: mnyonge mnyongeni, HAKI yake mpeni. Mama Samia Suluhu apongezwe kwa Miradi inavyoendelea kama ilivyoachwa na mtangulizi wake.

Nafurahia kuona barabara za Mwendokasi zinavyoendelea kujengwa kwa kasi nzuri, flyovers n. k.

NAWAS
Fly over ya wapi mkuu?
 
Waswahili Wana kamsemo: mnyonge mnyongeni, HAKI yake mpeni. Mama Samia Suluhu apongezwe kwa Miradi inavyoendelea kama ilivyoachwa na mtangulizi wake.

Nafurahia kuona barabara za Mwendokasi zinavyoendelea kujengwa kwa kasi nzuri, flyovers n. k.

NAWAS
1. Miamala je
2. Machinga je
 
Haya usijeyaongea baadhi ya sehemu, unaweza shushiwa kichapo kitakatifu. Kuna watu hawamwelewi na hawajawahi kumwelewa
 
Mara ya mwisho kurudi kijijini kwenu lini, je Kuna mradi gani unaendelea,je ina dhamani kiasi gani
 
Back
Top Bottom