Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mungu aliona mbali akasema wakae nyumbani watupikie na kulea watoto mwanamke hakuumbwa kuwa kiongozi na haya ndo matokeo yake anaropoka kama mkuu wa mkoa vile kumbe yy ndio raisi wa nchi tufunge mikanda tutafika.
Kweli mkuu mambo mengine hayafai kufosi, ni asili.
 
Mama unataka tukukumbushe hili mara ngapi ili utuelewe Wanao tunaokupenda na kukutakia mema? Wengine hatujaumbwa na Unafiki wa Kukupamba ( Kukusifia ) tu hata kama kuna mahala Unaharibu ila maana yetu halisi ya Kumpenda Mtu ni Kumkosoa kwa Kumjenga pale akikosea ( akikengeuka ) mahala.

Sasa kama Wewe ( Rais ) tunayeamini kuwa una Taarifa zote na Ufahamu mwingi wa Kimaarifa iwe ni Binafsi au kupitia Wasaidizi wako kila mara ukizungumza au ukitolea Ufafanuzi Jambo muhimu ni lazima useme Neno I think ( Unadhani ) je, Sisi Watu wa kawaida mno nchini Tanzania akina MINOCYCLINE tusemeje au tutumie neno gani?

Mbele ya Watu very Serious na Werevu ndani na nje ya nchi nina uhakika ukiwa unasema ( unalitumia ) neno hili la Unadhani ( I think ) huwa Wanakudharau na hupoteza pia imani nawe na hata Credibility yako vile vile hushuka ( inashuka )

Binafsi neno Nadhani ( I think ) silipendi na hata huku Kimtaa Mtaa ( Mtaani ) nikiwa naongea na Mtu ( hasa kwa Jambo Muhimu ) halafu akiwa anasema Nadhani ( I think ) huwa namdharau na hata kutamani Nimzabe tu Kibao kwani huwa nahisi ni Mtu asiye Knowledgeable and Well Informed katika Mambo ( Masuala Mtambuka ) mengi ya Tanzania na nje ya Mipaka ya Tanzania.

Wasaidizi wa Rais msaidieni katika hili.
Aise mkuu upo makini sanaa, nimemfatilia nimeona hili tatizo nilibaya sana, kwenye hi Royal tour kuna swali aliulizwa, nikipindi gani kizuri cha kutembelea Tanzania kufanya utalii kwamba ni mwezi gani akajibu vile vile nadhani ( I think) June.

Ukishajibu swali kwa kusema nadhani ( I think) inamaana huna uwakika na ulichojibu pia wazungu hawapendi hilo jibu la I think unaonekana hujui kitu wala hukujipanga. Mwalimu wangu aliniambia ni kosa kubwa kusimama mbele za watu kufanya representation then unaulizwa swali kutoka kwenye issue iliyo present unajibu nadhani (I think) kosa kubwa sana
 
Ndio nitasema Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ni Mama Samia, katika kipindi cha mwaka mmoja na kidogo amefanya Tanzania ifungue njia ngumu zilizoasisiwa ili kuifanya Tanzania kama kisiwa katikati ya jangwa

Nitasema yeye ndiye ameamua kufungua minyororo ya demokrasia na utu Tanzania
Ndio nitasema yeah ndiye aliyefanikisha mpango kamambe wa kutangaza vivutio vya utalii Tanzania kuliko mwingine yeyote

Nitasema kupanda kwa madaraja kwa walimu, ajira mpya ni mpango wake,
Narudia nitasema kuruhusu demokrasia na uhuru wa kuongea,

Tena tena haki ya kutoa maoni, na zaidi, uwezo wa kujua lila na fila,
Tumuunge mkono, (hata mimi konyagi natumia)
 
Huna akili, kichwa umebeba kama begi la kutunzia meno. Aibu kukopa pesa halafu ukaishia kuzigawa kwa wahuni wachache, unanunua software kwa bilions of money hapo TANESCO halafu zoezi la postikodi unashindwa kulitengea bajeti ya kueleweka.
 
Kwani Rais Samia anatekeleza ilani ya ccm au kuendeleza miradi aliyoanzisha mtangulizi wake? Kiukwel yote yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika ni sehemu ya ilani ya ccm.
 
mnamo tarehe 22 ililipotiwa kutoka vyanzo mbalimbli vya habari kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amezindua filamu ya kukuza utalii nchini inayokwenda kwa jina la ROYAL TOUR moja filamu inayosemekana kuwa ni bora ila pia kulingana na ofisi ya mawasiliano ikulu ililipoti kuwa safari ya hii filamu imeleta neema kuwa ya mikataba kutoka nchini marekani.Ni sawa tumepata mikataba ila umeniangusha Suluhu kwani wizara ya mambo ya nje na Afrika mashariki chini ya waziri wake lakini pia Balozi zilizopo nje ya nchi zinamaanisha au kazi gani ipi kubwa zinafanya?

how much cost us kwa Rais wa nchi kuzunguka sehemu mbalimbali katika nchi na kurekodi(si vibaya) ila ubaya unakuja misafara ya nje ya nchi unazali limetugharimu kiasi gani? au kuna mtu ameoteshwa kuwa utalii utafanikwa kuwa mpaka Rais ukazunguke nje kwa kupromote hiyo filamu yani kwa hili ulofanya inaonesha umeniangusha.Naomba nimsubiri CAG atasemaje kuhusu bajeti na matumizi ya hiii filamu.

Nakutakia sikukuu njema ya muungano.
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo...
Mkuu nakupongeza sana kwa kuwa na idea nzuri ya kuanzisha mada hii ili watu waweze kutoa maoni yao juu ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan na kujaribu kumpa ushauri wa mambo ambayo wadau wangependelea kwa kutumia serikali yake ayafanye. Kwa hali hiyo naomba kuchangia mada yako kama ifuatavyo:

Mimi binafsi namwona Mama Samia sio mwanasayansi na wala hana DNA ambazo zina embrace elements za kisanyansi. Katika maswala ya sayansi yeye kusema ukweli anaonyesha kuwa hajui kitu wala hana maarifa mapana ya kiutawala. Fikra zake bado ni za mtu mkongwe na asiye jiamini. Kwa hali hiyo mkuu tusitegemee kuwa ataweza kuiongoza hii nchi kisayansi na kitechnolojia ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi kulingana na mazingira ya kisasa ya dunia. Uwezo na ubavu huo hana.

Sababu zinazo nifanya niwe na mtazamo huu ni mwenendo wake wa utawala. Toka alipotwaa madaraka ya kuitawala hii nchi ameonyesha udhaifu mkubwa katika utekelezaji wa mawazo yake mwenywewe kwa kutojiamini. Rais ambaye hata mwaka hajamaliza anaanza kutoa kauli kuhusu uchaguzi wa 2025 na hivyo kuanza kuweka mikakati ya maandalizi ya uchaguzi huo kwa kuwateua viongozi wa serikali yake ambao ni incompetent katika vision, thinking capacity na utoaji wa maamuzi ya haraka ya kutatua matatizo na kero ambazo watanzania wengi wanakabiliana nazo kama; ajira, nishati na huduma mbali mbali za maisha ya kijamii na mambo yanayo husu miundombinu ya usafiri na maji taka, huyo hawezi kuwa Rais mbaye yuko madarakani kwa manufaa ya wananchi, bali ni Rais ambaye yuko madarakani kwa manufaa yake mwenyewe, familia yake, ndugu zake na marafiki zake wa karibu.

Watu kama; Januari Makamba, Nape Nnauye na Ridhiwani Kikwete kuwaweka kwenye baraza lake la mawaziri na kuwapa wizara nyeti kama wizara ya Nishati na kadhalika kunaweza kukagarantii huduma bora za mahitaji muhimu ya maisha ya wananchi na maendeleo ya nchi kweli? For the heven´s sake, hawa watu wanauwezo gani wa kukabiliana na challenges za ulimwengu huu wa sasa katika kuleta ideas nzuri zitakazo saidia kurahisisha maisha ya wananchi na kuleta maendeleo ya haraka?

Mifano mingine tumeiona hivi karibuni katika mabadiliko aliyoyafanya kwenye chama chake cha CCM kwa kuwarudisha viongozi wakongwe kama akina Kinana na wengineo kwenye positions za juu za chama ili waweze kumlinda na kurahisisha uchaguzi wake wa 2025. Rais mwenye mawazo na fikra za namna hii ni dalili ya Rais dhaifu na incompetent kwenye uongozi. Na ndiyo maana tunaona jinsi gani ambavyo amefeli kwenye kuweka mikakati madhubuti ya kuipaisha nchi yetu kwenda kwenye uchumi wa juu na badala yake tumeporomoka kurudi kule kule tuliko kuwepo kwenye nchi ya uchumi masikini duniani. Na hiyo ni katika kipindi cha mwaka mmoja tu. Sina uhakika kama ni dalili nzuri hizo!

Nilitegemea Rais wa nchi yenye rasilimali kubwa kama Tanzania na yenye vijana wengi wenye elimu ya kutosha ya nje na ndani na uzoefu mkubwa wa utendaji kazi kuwa na watendaji ambao ni competent katika ku-think na kutoa maamuzi ya haraka na strategic ya kutumia rasilimali zetu hizo kuusukuma uchumi wetu kwenda juu na hivyo kuboresha maisha ya wananchi na vijana wetu kuwa na matumaini ya kupata ajira.

Ni masikitiko yangu makubwa sana kuona Rais wetu anatilia mkazo mkubwa kwenye mipango ya kuwarahisishia mazingira ya kufanya biashara wafanya biashara wakubwa na wawekezaji kutoka nje ambao matokeo yake tumeshayaona huko nyuma kuwa hayakutusaidia sisi chochote. Wawekezaji na wafanya biashara duniani kwote hawana malengo ya kupunguza tatizo la ajira bali priority yao iko kwenye Profit maximization.

Hivi karibuni nimeona na kuzisikia jitihada za Rais Samia kwa kuwa mstari wa mbele katika ku-act na kuifanyia marketing documentary film yake ya Royal Tour ili ku-promote utalii wa nchi yetu. Any way, sioni kama ni kitu kibaya ila tu nina wasi wasi mkubwa katika kuyaona matokeo yake. Ndiyo tutapata matokeo mazuri kidogo ya kuongezeka kwa watalii nchini, hiyo nina uhakika, lakini je, is it going to be sustainable na kuongeza pato la Taiafa kwa kiasi kikubwa ambacho kitatuwezesha sisi kuanzisha miradi mingine mipya ya maendeleo?

Kwangu mimi jitihada kama hizi sizioni kama ni jitihada kubwa sana katika malengo ya kumfanya mtanzania akomae kifikra strategically, kwani hii ni mikakati ambayo inatufanya sisi tusiwe taifa lenye watu wanaojiamini na badala yake kuwa taifa lenye watu tegemezi kwa watu wa mataifa tajiri duniani na hasa wazungu. Hivyo sioni kama ni mikakati mizuri na yenye afya njema kwa jamii. Taifa lenye watu wenye fikra za namna hii ni Taifa lenye watu dhaifu na incompetent na in the long run haliwezi kustahimili kwa mda mrefu, litakufa tu na kusubiri kuzikwa.

Kwa utajiri ambao nchi yetu unao kwenye rasilimali kubwa za madini nilitegemea Rais Samia kuweka mikakati thabiti ya maendeleo kwa kuwekeza kwenye skills za vijana wetu kwa kuchukua mikopo mikubwa ambayo itawawezesha vijana hao kutumia hizo skills zao kutatua matatizo ya maisha ya wananchi na hivyo kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Ziara zake za nje zingekuwa ziara za kuwashawishi na kuwa-motivate diaspora kuleta nchini maarifa yao waliyo yapata kwenye nchi zilizo endelea ili kujenga na kuimarisha uchumi wetu wa kilimo, viwanda na teknolojia, badala ya kuwa ziara za kuomba remittances kutoka kwao. Hii inaonyesha kuwa Mama hayuko serious na maisha ya watu katika nchi yake na hayuko tayari kuwasaidia watanzania katika kutatua matatizo yao ya kiuchumi kwa kutumia uwezo wao.

Hata hivyo namshukuru sana na kumpa pongezi kubwa Rais wetu kwa kuendelea kuitekeleza kwa ufanisi mkubwa miradi yetu ya kimkakati ambayo ilianzishwa na kipenzi chetu Hayati Magufuli. Miradi hiyo itakapo malizika itakukwa na impact kubwa sana katika shughuli za kibiashara kati yetu na nchi jirani na vile vile kwenye kusaidia kukuza uchumi wetu na nchi jirani na vile vile kuleta maendeleo ya watu.

Mbali na hayo ningemwomba Mama Samia kuzingatia sana katika uwekezaji wa mtambo wa kuoka chuma ili tuweze kutumia mali ghafi yetu ya chuma na mtambo wa kuchakachua NG yetu kuwa LNG kwa matumizi yetu. Hasa kwenye kipindi hiki kigumu cha uhaba wa fossil energy kilicho sababishwa na vita huko Ulaya.

Kulingana na utafiti wangu na uzoefu nilioupata kwenye nchi za wenzetu ningependa kumwakikishia Mama kuwa Miradi hii itakuwa ndiyo muarobaini wetu wa utatuzi wa matatizo yetu ya ajira kwa vijana na upande mwingine kupanua wigo wetu wa maarifa kwa kuwa wabunifu na wavumbuzi wa vitu kunako kosekana, kwani multiplier effect yake itakuwa very very huge kuliko haya mambo madogo madogo anayo yafanya ya kuwaridhisha wafanya biashara wakubwa na kupromote uchuuzi nchini.

Bila uchumi wa viwanda nchini Rais Samia hatutatoboa hata mara moja na hili tatizo la ajira halita tatuliwa kirahisi hivyo. Naomba akumbuke kwamba uchumi huu wa viwanda utaletwa na watanzania wenyewe tu kwa creativeness yao na sio vingine. Asidanganywe na mtu. Serikali iwekekeze tu kwenye general conditions za kuwawezesha watanzania hao ku-operate.

Ningependa kumwuuliza swali Rais Samia, je, serikali yake imechukua hatua gani la kulijadili na kuhamasisha swala la creativity la mtanzania Masudi Kipanya katika activities zake za utengenezaji wa gari lake linalotumia umeme?
Hapo ndipo mahali ambapo mimi nina m-disqualify yeye kuwa hana DNA ya sayansi, kwa sababu natambua kuwa yeye haamini sayansi kuwa ndiyo mkombozi wa maendeleo ya binadam. Na hivyo hana imani kwa watanzania kuwa wao wako capable kufanya mambo makubwa yatakayo leta maendeleo ya uchumi wa hii nchi. Naona, amejikita sana kwenye wawekezaji wa nje na wafanya biashara wakubwa ambao wana wahonga politicians wake kwa pesa zao ili kumpa ushauri ambao una wa-favour wao. Kwa mtindo huu hata jenga taifa lenye vijana ambao ni creative na wenye vision. Na yeye mwenyewe hata jiwekea legacy nzuri kwa watanzania.

Ushauri wangu kwake Rais Samia, naomba ajiamini na aingie risk ya kuchukua mikopo mikubwa itakayo tuwezesha kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya miundombinu ya kimkakati katika sekta za viwanda, kilimo utalii na kadhalika kwa;

1. kuwashirikisha na kuwawezesha watu wenye asili ya kitanzania wa nje na ndani ya nchi kuwekeza kwenye makampuni na viwanda vikubwa vya kuoka chuma, aluminium na bidhaa nyingine, na viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza biza zinazotokana na products hizo na nyinginezo ikiwemo pia viwanda vya kufanya galvanization kutengeneza magari na kadhalika,

2. kuwashirikisha na kuwawezesha watu wenye asili ya kitanzania wa nje na ndani ya nchi kuwekeza kwenye makampuni ya usambazaji wa gas asilia NG na plant ya kuchakachua LNG na vingeinevyo vinavyo tumia mali ghafi zetu.

3. kuwashirikisha na kuwawezesha watu wenye asili ya kitanzania wa nje na ndani ya nchi kuwekeza kwenye miundo mbinu mbali mbali ya usafiri kama SGR , treni za angani Skytrain na kufungua karakana za ufundi na kadhalika,

4. kwa kuwahamasisha vijana na watanzania kwa ujumla katika ubunifu na uvumbuzi wa utengenezaji wa vitu tofauti ambavyo tuta vitumia sisi wenyewe kwa mahitaji yetu na vingine kuuza nje kwa kuwajengea mazingira ya kuwa na special soft ware tools za CAD (Computer Aided Design) kama; CATIA V5/6, Siemens NX, SolidWorks, CLEO Parametric na nyinginezo ambazo Design Engineers, Product Desgners na Technicians wetu wanaweza kuzitumia katika creation of functional parts, sub-assemblies and assemblies za mechanichal products na vile vile Hard ware kama; CNC Milling Machines, Lathe Machines na Lasser Cutting Machines pia Injection Moulding Machines ambazo vijana wetu wanaweza kuzitumia katika kutekeleza malengo yao ya manufacturing of different steel and plastic products.

Asiwawafanye vijana wetu kuwa washamba wa kushangaa vitu ambavyo vina tengenezwa na wazungu na wa asia kwa ukosefu wa vifaa na maarifa kwa sababu ya kuwa na viongozi na watu washamba wasio jua nini maana ya maisha ya taifa letu la kesho kwa kukosa maarifa na maono.

Katika hili ninge mwomba asing'ang'ane na ma-theoretician wake wa vitabu ambao hawana uzoefu wowote wa practical works. Atafute watu ambao wameenda darasani na pia kupata experience kwenye really industrial activities kwa wenzetu ili waje kutusaidia kuwajenga vijana wetu. Awajengee vijana wetu Workshop kubwa sana Chang'ombe ambayo itakuwa equipt na tools mbali mbali za kufanya creation/construction na manufacturing processes ya vitu mbali mbali ili vijana waweze kuamsha bongo zao kwa kuleta ideas zao kutengeneza vitu tofauti, badala ya kuwafanya wawe wachuuzi wa products za wa asia.

Lile bonde la msimbazi alifukue lote ili liwe bahari na pembeni kutoka upande mmoja wa Surrender Bridge mpaka upande mwingine kulizunguka hilo Bonde atengeneze barabara na awajengee wamachinga na mama ntilie vibanda vizuri ili waweze uza bidhaa zao na vyakula 24/7 kwa mpangilio mzuri na mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Kwa kufanya hivi Mama atakuwa umeliweka jiji katika hali nzuri ya kuvutia. Na hivyo kuwavutia watalii kutoka nje. Hayo ndiyo maboresho ambayo wana mipango miji yetu wanatakiwa wawe nayo ili kusaidia kupunguza matatizo ya ajira kwa vijana wetu na kwa watu wasio na elimu kubwa ya kuajiliwa viwandani, maofisini na katika utumishi wa umma.
 
Sisi tunaenda zetu awamu ya saba na Rais Samia huku yeye akiwa ameshawaacha wafanyakazi wake na watumishi wa umma awamu ya tano
 
MUNGU tu atusaidie naona tumeshadumbukia shimoni tena gizani...hatujui mustakabali wa baadae.. Walkingdead kabisa..
 
N
UVCCM TAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na makamu wa Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr Philip Mpango katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam wakati akielekea nchini Marekani kwa ziara ya kikazi leo tarehe 13 Aprili 2022,...

Nashauri tu, ingependeza sana mama anapokuwa kwenye safari za kikazi hasa zile za mbali aidha ndani au nje ya nchi, AONGOZANE NA MUME WAKE!!

Hayo ni matumizi sahihi ya kodi yetu!! Mume ni mlinzi wa uhakika, si mnajua? Au nasema uongo ndugu zangu! Kwani huwa hamuoni marais wengine kama Obama au Trump hawawaachi mbali wenza wao. Obama ndo kabisa hata watoto wake anafuatana nao!!
 
Ndani ya miezi miwili ametoa kauli zinazokinzana na 'tata' zihusuzo gharama na bei ya vitu na mafuta.

Mfano,mwezi jana huku akiwa amefura aliagiza tozo zirejeshwe kwenye mafuta kwa sababu ya eti zipo kikodi na naksi yake haijaziliki na akasisitiza lazima vitu vipande bei!

AJABU LEO ETI KIPARA ANATUAMBIA ETI MAMA AMESONONESHWA SANA NA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA NA VITU 😄!

Samia,usitufanye wote wajukuu zako bwana tafadhari eleweka na tofauti na hivyo-HUELEWEKI!
 
Leo 11/5/2022, chadema Iko live!

Ni muujiza Kwa kweli. Tumetoka gizani Kwa miaka sita nchi ilijaa Giza Totoro.

Leo cloud Media wako live mlimani city. Wananchi wengi wamefurahi kuona na kusikiliza kinachoendelea.

Mama huitaji kupiga compaign 2025, sisi wapenda hoja kinzani tutakuchagua tu.

Watoe waliofungwa magerezani Kwa hila na yule mwovu.

Anga la Tanzania sasa linang'aa Kwa busara zako

Mungu akupe maisha marefu mama yetu.
 
Miaka kadhaa huko nyuma tulikuwa tunakimbia kusikiliza TBC kwakuwa ilikuwa na vishindo vya habari zenye ubaguzi kitaluma.
Leo mwandishi wa TBC ameripoti taarifa zenye mizania kupitia VOA kuhusu siasa za Tanzania hasa upinzani.Heko kwako mtangazaji Mgeni was TBC.

Waandishi wa TBC mmeanza kutupapasa wananchi tuliokuwa tumefichama kusikiliza mapambo ya kumsifu mtu mmoja asubuhi hadi jioni.
 
Back
Top Bottom