Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mambo yao waachie wenyewe, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Mods wabadili haraka kumnusuru ndugu Robert.
Relevance ya hii title haina sumu kwa Rais Hassan, inagusa uongozi wa Magufuli ndio ulijaa ushamba na ulimbukeni, na baadhi kama Mwigulu ndio washamba na limbukeni
 

Na assume wajanja unamaanisha watoto wa mjini na malimbukeni ni watoto wa kijijini...


Kwa maelezo yako ni hafdhali kuongozwa na huyo limbukeni/mshamba anauwezo wakuhoji kuliko mwerevu alieshikiliwa akili na mabeberu

Hao wajanja na werevu ignorance yao inatia kichefuchefu...kwanza ndio malimbukeni namba moja.....

Hv kwa mfano mtu akaja akaomba umpatie cheni ya dhahabu bure halafu in exchange yeye akupe chandarau ya mbu ujikinge na malaria maana inaua kweli...nani mwerevu hapo?!
 
Ifike wakati mkuu uwaonee huruma watanzania na kero za maji na umeme kukata marakwamara

Hao vijana wamechoka hasa huyo wa maji anakurubuni na misamiati kibao,asikuchanganye piga chini
 
Mpaka sasa Rais Samia anafanya vizuri katika sekta ambazo zinawagusa watu wengi, sekta kama ya kilimo, elimu na afya ni sekta muhimu na zinahudumia Watanzania wengi. Kwa kuonyesha kujali na kuwapenda watu anaowaongoza, Rais Samia baada ya kuapishwa aliamua kukazia fikra sekta hizo ili kuboresha maisha ya Watanzania na kutia chachu maendeleo ya nchi.

Shule na hospitali zimejengwa, madawati, vifaa tiba vimenunuliwa. Bei za mbolea zimeshushwa, yote hii ni kuhakikisha mazingira wezeshi kwa Mtanzania #mamayukokazini
 
Japo sitegemei afanye kama au style yake ya uongozi ifanane na ya Magufuli, hata hivo hajaharibu sana. Kama ingekuwa ni grade kati ya 0 (kufanya vibaya sana) na 100 (kufanya vizuri sana) nampa 61.
 
Japo sitegemei afanye kama au style yake ya uongozi ifanane na ya Magufuli, hata hivo hajaharibu sana. Kama ingekuwa ni grade kati ya 0 (kufanya vibaya sana) na 100 (kufanya vizuri sana) nampa 61.
Kweli kabisa kiongozi nae ni binadamu, sio mkamilifu
 
Huu uzi ni muhimu mheshimiwa anaupitia hapa Kama si yeye pia wasaidizi wake kikubwa naomba aendelee kugusia sekta za afya, usafirishaji, Ulinzi
Sina haja ya kuongea mengi ila humo akazie zaidi kuanzia vifaa bora,miundombinu yao, maslahi ya watumishi wa hizo sekta, na kwenye uzembe afumue na kuboresha
 
Mama pamoja na kuwa kwenye chama muda mrefu, ni mwanachama mwenye makovu ya chama. Iwe kwake mwenyewe ama kwa ndugu zake walioko kisiwa cha kisiwani.

Ndani ya moyo wake anajua kwa dhati kwamba pamoja na kwamba sasa ndiye dereva, lakini gari anayoiendesha haipendi.

Nina hakika, hawezi kumaliza safari pasi na kuibadilisha.

Yetu macho kuona kama ile nguvu ya ndani ya moyo itaizidi ile ya nje tunayoiona.

Kila la kheri mama kuelekea gari jipya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…