Elsa Marie
JF-Expert Member
- Jul 7, 2017
- 2,284
- 5,596
Kuna wengine hawaguswiUnamtukana jirani yako unaishi mtaa mmoja sembuse usiye muona wala kumkaribia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna wengine hawaguswiUnamtukana jirani yako unaishi mtaa mmoja sembuse usiye muona wala kumkaribia
Haguswi mungu tu na shetani wengine wote duniani sawaKuna wengine hawaguswi
Mods wabadili haraka kumnusuru ndugu Robert.Mods titile ianze Ni hatari kuongozwa na .......neno nchi lifutwe
Relevance ya hii title haina sumu kwa Rais Hassan, inagusa uongozi wa Magufuli ndio ulijaa ushamba na ulimbukeni, na baadhi kama Mwigulu ndio washamba na limbukeniMods wabadili haraka kumnusuru ndugu Robert.
Mshamba baba yako na mama yako.Ogopa ulimbukeni na ushamba.
Una ujinga mwingi.😂😂😂
Unahasira Kali Mzee.
Well said MkuuMkuu Mimi ngoja niwaachie Hii kesi. Kazi yangu ni kuandika tuu
NCHI INAPOONGOZWA NA LIMBUKENI NA MSHAMBA!
Anaandika, Robert Heriel
Hakuna Jambo baya kama kuongozwa na limbukeni na MTU mshamba, iwe ni kwenye Familia, taasisi au hata taifa Kwa ujumla.
Embu assume ni Mwanamke umeolewa na Mwanaume limbukeni na mshamba, akipata tuu, dharau zinaanza, matusi ya nguoni Mbele ya watoto wako na watu, yaani hajali chochote.
Limbukeni na mshamba akishaanza Kupata vijihela Wanawake si wataanza kujigonga kwake, Kwa vile ni limbukeni wa wanawake litaanza kumringia na kumsumbua Hadi MKE wake. Ulimbukeni na ushamba ni kitu kibaya Sana.
Ni Bora Mwanamke awe Limbukeni na mshamba kuliko mwanaume.
Ogopa kuongozwa kwenye taasisi au Kampuni na mtu limbukeni na mshamba. Hakuna rangi hutaacha kuziona.
Wakati tunasoma kuna Wale Viranja na Mamonita waliokuwaga na ulimbukeni na ushamba sijui sasa hivi wapo wapi, Ila Kwa Tabia zao wengi wao Nina uhakika wanapumulia Mashine, walioweza Kubadilika wanahali nzuri tuu. Ulimbukeni na ushamba sio mzuri.
Tatizo la Watu limbukeni na washamba wanaupeo mdogo wa kufikiri, hilo ni moja.
Pili, Kutokana na upeo kuwa mdogo wengi wao ni Watu wa Kutumia nguvu na Ubabe wa kijinga. Ni ngumu Sana ukute MTU mjanja mjanja, mtoto wa mjini akitumia nguvu kwenye mambo yake.
Lakini limbukeni na washamba wanatumia mabavu.
Tatu, Limbukeni na washamba wengi wanapenda masifa, kutukuzwa na kulazimisha kuheshimiwa.
Ogopa nchi ikiongozwa na mtu wa Aina hiyo. Pia ogopa kuolewa na Mwanaume wa Sampuli hiyo. Yeye muda wote anawaza heshima heshima hata kama haimstahili.
Nne, limbukeni na washamba wengi hujifanya wajuaji, Hii inapelekea kuingizwa kingi kirahisi. Kumbuka wanaupeo mdogo, kumbuka ni Watu wa Kutumia mababu alafu muda huohuo wanajiona wanaakili nyingi Hali hiyo inapelekea wengi kuingizwa kingi na kuibiwa kirahisi au kupoteza pambano kienyeji.
Angalia hata wanaotapeliwa kienyeji ni Watu wa Aina gani.
Tano, limbukeni na washamba ni wachoyo na wabinafsi. Yaani hupenda Kula peke Yao. Kama akiwa Kiranja shuleni, lenyewe ndio litataka liwe linakula vyakula vizuri vizuri na kampani yake. Huku likizuia wengine. Ngazi ya familia, utakuta mwanaume ndiye anataka apewe vitu vizuri vizuri kama mapaja na minofu mineneminene huku MKE na watoto wakiambulia funyago za vipapatio. Ni wabinafsi hujawahi kuona.
Mtu mjanja, hawezi fanya hivyo, huwezi lisha Watoto na MKE vipapatio alafu wewe ule mapaja tena Mbele Yao, Kwa Mwanaume mwenye Aibu na haya hawezi kitu kama hicho.
Limbukeni na washamba wanapenda kudhalilisha wengine Mbele za Watu ili yeye apate ujiko. Ni Watu wa kujilisha, kukuoshea mbele za Watu ili ajipatie pointi ni kitu cha kawaida. Ni Watu wa kujikosha.
Ni hatari Sana kucheza na Kiongozi mshamba na limbukeni Kwa sababu yeye haoni shida kukudhuru kiukwelikweli ikiwezekana kukupa ulemavu au Mauti kabisa.
Hii ni tofauti na watu wajanja na werevu, Kwanza MTU mwerevu anapenda michezo na anajua kutofautisha mchezo na Kazi. Sio rahisi Watu wajanja na werevu kukudhuru.
Tabia ya malimbukeni na washamba ya kupenda kujionyesha Kwa Watu ni Wema, na kupenda kusifiwa tuu inawafanya wasitake kupingwa wala kukosolewa. Yaani wao wanataka kila kizuri kiwe Chao tuu.
Limbukeni na washamba wanapenda Sana utani Ila wao hawapendi Kutaniwa, yaani wao wakikutania kwao ni burudani watacheka mpaka jino la mwisho, lakini watanie wao sasa, uone watakachokufanya.
Kimsingi ni hasara kubwa kuongozwa na watu wa Aina hiyo.
Faida yao kubwa ni kufanya mambo Kwa Sifa ili waonekane, yaani kama ni kujenga watajenga lakini Kwa gharama ya Kuwaabudu kama miungu Watu.
Jambo ambalo Kwa Watu Werevu hawawezi kuliafiki. Watu Werevu wao ni akheri waishi Maisha ya kimaskini lakini wawe huru kuliko kuijengewa majumba na miundombinu lakini wakiwa watumwa wakiabudu MTU kama MUNGU.
Huwezi fanya biashara au mapatano na MTU limbukeni au mshamba kwani muda wowote atakubadilikia na wanapenda Kutumia ubabe.
Wafanyabiashara kiasili ni Watu Werevu hivyo wakijua kiongozi Fulani ni limbukeni na mshamba huchukua hatua ya kufunga baadhi ya biashara ili kujihifadhi.
Limbukeni na mshamba akiongoza anafikiri Watu wote ni kama MKE na watoto wake. Hivyo atawa-treat vyovyote bila kujali ninyi sio Watoto na wala hamna uhusiano wowote kindugu. Isipokuwa mmeunganishwa labda katika taasisi au kazi Fulani au Taifa.
Siasa za ushamba na ulimbukeni ni hatari Sana. Yaani hapo kupasuka ni rahisi Sana. Kwa Vijana wadogo mnaoingia kwenye Siasa, Taikon anawashauri kuwa hakikisheni Kabla hamjafanya movement yoyote muwe mmeshajiridhisha Aina ya kiongozi aliyepo kuwa ni kiongozi wa namna gani. Kama ni limbukeni na mshamba au Mjanja na mwerevu
Kisha mtajua mfanye mambo yenu Kwa Njia ipi, Passive au Active, Direct au Indirect. Vinginevyo ni hatari Sana.
Mimi ngoja nipumzike Kwanza,
Wito wangu, Epuka kuwa Limbukeni na mshamba Kwa ngazi yoyote Ile.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mpaka sasa Rais Samia anafanya vizuri katika sekta ambazo zinawagusa watu wengi, sekta kama ya kilimo, elimu na afya ni sekta muhimu na zinahudumia Watanzania wengi. Kwa kuonyesha kujali na kuwapenda watu anaowaongoza, Rais Samia baada ya kuapishwa aliamua kukazia fikra sekta hizo ili kuboresha maisha ya Watanzania na kutia chachu maendeleo ya nchi.Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Japo sitegemei afanye kama au style yake ya uongozi ifanane na ya Magufuli, hata hivo hajaharibu sana. Kama ingekuwa ni grade kati ya 0 (kufanya vibaya sana) na 100 (kufanya vizuri sana) nampa 61.Mpaka sasa Rais Samia anafanya vizuri katika sekta ambazo zinawagusa watu wengi, sekta kama ya kilimo, elimu na afya ni sekta muhimu na zinahudumia Watanzania wengi. Kwa kuonyesha kujali na kuwapenda watu anaowaongoza, Rais Samia baada ya kuapishwa aliamua kukazia fikra sekta hizo ili kuboresha maisha ya Watanzania na kutia chachu maendeleo ya nchi.
Shule na hospitali zimejengwa, madawati, vifaa tiba vimenunuliwa. Bei za mbolea zimeshushwa, yote hii ni kuhakikisha mazingira wezeshi kwa Mtanzania #mamayukokazini
Kweli kabisa kiongozi nae ni binadamu, sio mkamilifuJapo sitegemei afanye kama au style yake ya uongozi ifanane na ya Magufuli, hata hivo hajaharibu sana. Kama ingekuwa ni grade kati ya 0 (kufanya vibaya sana) na 100 (kufanya vizuri sana) nampa 61.
Mungu aliona aingilie kwa kweliYah but wao walijiona watakua salama sababu ya backup yao!!