Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Nakuhakikishia kuwa hiyo post yako itatafutwa sana na wana JF kukuuliza kuhusu UNABII wako.

Samia yuko kwa mapenzi ya Mungu kwa Taifa letu. Kifo cha Mwendazake kiitokea kwenye kipindi ambacho kama angekuja kiongozi mwingine tofauti na yeye basi utulivu wa Taifa ungekuwa mashakani. Heshima kwako Mkatoliki mwenzangu General Venance Salvarory Mabeyo kwa kuhakikisha peaceful transition
 
Ishaunganishwa mkuu
 
Huyo mabeyo kwasasa anajutia jambo fulani ambalo hawezi weka wazi!

Samiah katutoa Sana kweli lakini Kuna mambo yatatutafuna na kizazi chetu huko mbeleni!

Itafikia kipindi tutalipa Kodi ya ardhi Kwa wageni ndani ya ardhi yetu wenyewe!!

Ni hilo tu!!Ardhi,ardhi ,ardhi ,ardhi ya Tanganyika eeh Ardhi!
 
Leo morogoro ilikuwa balaa. Hata jpm hajawahi kulakiwa vile na nyomi ile.

Wakuluma wanainjoy sana chini ya utawala huu. Mazo mengi jpm aliua na soko kukosena sasa mama karudisha tabsamu. Kororosho, mbaazi, viazi nk
 
Kazi ipi nzuri unaiongelea ?

Kubinafsisha mali za Tanganyika

Kuchukua mikopo na kuipeleka Zanzibar huku walipaji wakiwa Watanganyika
 
Kazi ipi nzuri unaiongelea ?

Kubinafsisha mali za Tanganyika

Kuchukua mikopo na kuipeleka Zanzibar huku walipaji wakiwa Watanganyika
Kawaulize moro wanavyomshangilia utafikiri masihi. Wakulima wanajua samia anachowafanyia. Jpm aliua mazao yao. Mam karudisha tabasamu kwa masoko ya nje na ndani
 
Leo morogoro ilikuwa balaa. Hata jpm hajawahi kulakiwa vile na nyomi ile.

Wakuluma wanainjoy sana chini ya utawala huu. Mazo mengi jpm aliua na soko kukosena sasa mama karudisha tabsamu. Kororosho, mbaazi, viazi nk
Bado mnaamini kuna watu wanahadaika na hizo nyomi za mchongo? Kama mnajiamini kwa hizo nyomi za mchongo, ruhusuni tume huru ya uchaguzi muone mnavyojidanganya vibaya.
 
for sure wakulima wanaenjoy with very long smile na uongozi wa huyu rais kipenzi cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan...

uwekezaji uliochochea mapinduzi na mageuzi makubwa katika kilimo umeleta mabadiliko makubwa mno kwenye maisha ya waTanzania 🐒
 
Bado mnaamini kuna watu wanahadaika na hizo nyomi za mchongo? Kama mnajiamini kwa hizo nyomi za mchongo, ruhusuni tume huru ya uchaguzi muone mnavyojidanganya vibaya.
Wenzako kenya hawasubili serikali iruhusu tume huru ya uchaguzi bali wanaidai kwa nguvu na kufa wachache. Sasa wewe kama.unasubilia na unaogopa kufa basi endelea kusubili
 
Leo morogoro ilikuwa balaa. Hata jpm hajawahi kulakiwa vile na nyomi ile.

Wakuluma wanainjoy sana chini ya utawala huu. Mazo mengi jpm aliua na soko kukosena sasa mama karudisha tabsamu. Kororosho, mbaazi, viazi nk
Unaonaje umshauri bi mkubwa uchaguzi uwe fair and square kama kweli anapendwa watanzania waamue bila kuchakachua?
 
Hivi kuwa chawa (mpumbavu) inacost kihasi gani? Kuna fungu huwa linatengwa kwa haya mapambio?
 
Rais Samia Suluhu Hasan(Phd) kaongoza vizuri. Ni muda muafaka akapumzike kizimkazi kazi ya urais ni ngumu sana.
 
Mheshimiwa Rais, Shikamoo

Jukumu namba moja la Serikali yoyote duniani ni kuhakikisha nchi haina vurugu na inaendeshwa kwa utaratibu (Public Order). Serikali zote duniani lazima ziendelee kutekeleza kazi yake hii takatifu ambayo ni msingi wa mambo mengine yoyote yale kwenye nchi. Hata maisha hayatawezekana kama hakuna “public order”. Toka umeingia madararakani umeifanyia kazi hii kwa mafanikio makubwa. Umeliweka taifa letu salama, imara na kwenye njia sahihi.

Naandika ujumbe huu kukuomba na kukusihi kuendelea kutekeleza jukumu hilo kama ambavyo unafanya. Daima dawamu tusiruhusu uvunjifu wa sheria na amani yetu kwa kigezo cha uhuru wa kuzungumza. Tusiruhusu nchi yetu kuingia katika madhila yoyote kwa kigezo cha uhuru wa kukusanyika na kufanya siasa.

Wewe ni mtu mwema sana, mama na muumini wa mazungumzo na upatanishi, sote tunafahamu hilo. Tafadhali endelea kutumia njia zote unazopewa na Katiba, sheria na miongozo ya nchi yetu kuhakikisha kwamba wajasiriamali wa kisiasa ama mtu yoyote, popote ndani ya nchi yetu hapati mwanya wa kuvuruga Taifa hili. Uhuru wa kukusanyika na kufanya siasa lazima ufuate utaratibu na kama usipofuatwa basi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viingine kazini kuhakikisha public order inaheshimiwa na kudumishwa kwa faida ya kila mwananchi.

Ahsante kwa kusoma. Mungu Akubariki.
 
#MchapakaziSamia katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii
 
Attachments

  • IMG-20240818-WA0000.jpg
    146.5 KB · Views: 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…