Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Siyo Mzalendo Wewe Mwenyewe

Miradi Mingi Ipo Kwenye Hatua Nzuri

Unaifutaje. Bwawa La Nyerere Lipo Asilimia Hamsini Unalifutaje? SGR Imefika Morogoro

Unaifutaje. Labda Ambayo Haijaanza
 
Nadhani hii ndio nafasi ya kunogesha Muungano na kupima kama kweli tunaapenda aina hii ya Muungano kwa vitendo na si kwa maneno matupu.

Hivyo nakuomba, ikikupendeza, safari hii iwe ni zamu ya Wazanzibar kushika nyazifa hizo ambazo kwa miaka mingi tangu uhuru, zimekuwa zikishikwa na watanzania bara huku tukidai sisi ni nchi moja.

Tumekuwa watetezi wa Katiba na Muungano wa aina hii bila kujua kuwa kuna siku Raisi wa Muungano atafariki akiwa madarakani, hivyo tuwe tayari kupokea matokeo ya kuwa na katiba ya aina hii na Muungano wa aina hii.

Muungano wa Serikali mbili oyeeee!!

Ukipenda boga, penda na ua lake.

Mungu ni mwema sana.
 
Ha ha ..weeeeeh ..lazima Watanganyika lazima wapandishe mashetani ..hapo umesahau Katibu Mkuu ..Jaji Mkuu ..Gavana BOT ...katibu Mkuu CCM...N.K
 
Kwa nchi za kiafrika, mwanamke kukiongoza kiti cha uraisi kwa weledi inakuwa ngumu. Kwa sababu zifuatazo,
1: Sheria za utawala ni mbovu, katiba ni duni.
2: Vitengo vya ki-usalama na nyeti vya serikali na taifa kwa asilimia kubwa vimeshikiliwa na wanaume (Jeshi, Polisi, taasisi za intelligentsia, taasisi za ujasusi, taasisi za ushushu).
3: Mihimili ya serikali (Bunge na mahakama) vimeshikiliwa na wanaume.
4: Mitazamo dume kwa wanaume (Kuwa hatuwezi kutawaliwa na mwanamke).
5: Maamuzi ya wanawake (Mfano: Mama Banda kule Malawi, ndani ya miaka miwili kaanza kusema Ziwa nyasa ni lake).

Mwisho wa siku, unakuta mwanamke kiti Cha uraisi amekalia kama pambo nchi inaongozwa na wanaume vile vile.
 


Nakukumbusha mama wakati unaanza kurekebisha baraza la mawaziri anza na Wizara ya Afya. Wizara imeyumba sana imekuwa na waziri asiye na msaada wowote. Hii ni wizara serious sana lakini waziri wake aligeuka kuwa comedian na kuacha sayansi. Ikukupendeza mheshimiwa huyu atenguliwe hata ubunge maana ni hasara tu.

Hatuwezi kuwa na watu wanafiki wa kumfuatisha rais anachopenda badala ya kuwa mshauri asiyeyumba katika kusimamia fani yake kwa weledi
 
Eti "mtatamani aendelee kutawala mda mrefu!"
Utatamani ww, Deo sanga, Nkamia, na wote wa ccm.
Kazi kujipendekeza tu lkn nakuambia mama atawanyoosha mpaka mkome kenge nyie.
Mliye tamani atawale milele yuko wapi? Mnataka kumponza mama kwa kumkufuru Mungu?
 
Kwa muda sasa, udhibiti wa mada hapa JF umekuwa ukiongezaka kupita kiasi na kuondoa kabisa maana ya slogan inayotumiwa na huu mtandao( inafahamika kwa member humu).

Inafika hatua mtu unaandika mada huku unajiuliza hii mada itabaki au itafutwa. Tumefika hatua mbaya.

Sasa leo nimelata mada ya kuwashauri Mama Samia ateua IGP,CDF na Boss wa TISS kutoka Zanzibar eti nayo imeondolewa. This is too much!
 
Sawa, hawajibiki kutenda kila alichotenda mtangulizi wake, ana room ya kufanyia kazi mapungufu ya mtangulizi wake.

Namkumbusha tu asitupe jongoo na mti wake. Tupo makini sana katika hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…