Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,943
Watanzania wala hawahitaji kukusanyiwa vyeti feki, Watanzania wanahitaji huduma bora za kijamii na huduma muhimu. Unaongelea suala la vyeti ambalo mwananchi wa Sombanyasoko hajui faida yake!Huoni kua pengine hayo matatizo mengi uliyo yasema yanaweza kua yanasababishwa na hao wenye vyeti feki?
Habari za wakti huu;
Kwanza kabisa nimpe Pole mama yangu ,Samia Hassan Suluhu kwa kuondokewa na Boss wake,Lakini zaidi nimpe hongera kwa kupata fursa ya kuwa RAIS wa Jamhuri katika kipindi ambacho Jemadari mwendazake JPM alikuwa ameweka moja kati ya malengo makubwa sana(Most ambitious goals of the Modern Tanzania) ya kutaka kufanya Tanzania iwe nchi ya kisasa.Lakini Pia niseme tu kwamba Mwendazake JPM amemuachia TAIFA ambalo kwanza ni divided yet united.Lakini pia anayo kazi ya Pembeni ya kufanya Damage control and healing
Sasa nirudi kwenye mada kuhusu nzi.Kuna nzi wengi sana ambao wamezagaa na najua mpaka wakati huu wengi tayari wameshaanza kujisogeza karibu.Kuna nzi wa aina mbili ambao wanajisogeza kwa kasi sana karibu na RAIS wetu Mama Samia Suluhu Hasan
Nzi wa Aina ya kwanza ni wale ambao walinufaika na Mfumo uliokuwepo zama za Magufuli ambao wanatafuta kila namna kuhakikisha kwamba Maslahi na fursa walizokuwa nazo kisiasa,kijamii na kiuchumi zinaendelea kuwepo na kuna wale Nzi ambao hawakupendezwa na mfumo ule na wengine hata kama waliufaidi lakini hawakuupenda na wengine ambao waliumia na hawakunufaika nao na ambao nao wanasogea kwa kasi kabisa ili waweze kubadili uelekeo wa Upepo.Hawa nzi wote ni nzi hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.
Najua wachache wa nzi hawa unawajua ila pia najua kuna ambao huwajua au hujaweza kuwatambua ila jihadhari nao.Mheshimiwa RAIS ninapoandika waraka huu ninawaona jinsi wanavyoweka mikakati, wengine wanafuatilia historia yako kujua kama kuna kitu wanaweza kukitumia ili kukufikia kwa urahisi uweze kusikia ushauri wao. Mimi nakusisitizia waepuke hawa nzi.Kazi uliyo nayo ni kubwa sana.
Mheshimiwa RAIS, Wewe ni mrithi wa Magufuli na jamii haitakuelewa kama utaachia kusimamia yale mema ambayo Mwendazake Magufuli aliyasimamia.Usije kushawishika kudharau kukamilisha baadhi ya miradi ambayo ina tija ambayo iko katika hatua za utekelezaji kwani utajishushi heshima yako wewe na utakuwa umeitukana kumbukumbu ya mtangulizi wako JPM ambaye kifo chake kimekupa nafasi ya kuwa rais wa nchi.
Hata hivyo usiogope kuonesha tofauti hasa katika maeneo ambayo kwa hakika Mtangulizi wako hakuwa sahihi.Ndio hakuwa mkamilifu.Kuna baadhi ya mambo mengi sana yanahitaji kurekebishwa na usiogope kuwa tofauti kwani wewe unayo haki ya kuweka tone ya uongozi wako.
Naendelea kukusisitiza kwamba kwa sasa litazame Baraza la Mawaziri, kuna watu hawatakiwa kabisa kuwa humo,watakuvuruga.Kumbuka moja kati ya heshima kubwa uliyo nayo ni kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mpya.Nafasi hio inakupa jukumu moja kubwa nalo ni kuukamilisha mchakato ule na kuhakikisha sauti ya wananchi inasikiwa.
Mama Samia, Wewe ni Mzanzibari, tena Mzanzibari kweli kweli Usisahau hilo.Fanya Jambo kuhusu Zanzibar
Sitaki kusema zaidi ila kama nikajaliwa nitaongeza mengine ila kwa sasa nikutakie kila la heri katika kazi yako ya kuendesha nchi yetu
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Mh. Samia H. Suluhu
Rais wa JMT
Mkuu,nadhani kuna kitu unakimisi kwenye comment yangu,ipo hivi hao wahusika wanaotakiwa kushughulika na kutatua matatizo ya wananchi wanapokua na vyeti feki ina maana wapo kwenye hizo post kimagumashi,kwahiyo hata utendaji wao unaweza ukawa sio kivile.Watanzania wala hawahitaji kukusanyiwa vyeti feki, Watanzania wanahitaji huduma bora za kijamii na huduma muhimu. Unaongelea suala la vyeti ambalo mwananchi wa Sombanyasoko hajui faida yake!
Maisha ya wananchi ni kipaumbele cha kwanza kwa Rais yeyote yule aliyepo madarakani. Wanaoajiri watu wenye vyeti feki ni taasisi binafsi au serikali kama ni serikali yenyewe ndiyo inaajiri watu wa hivyo unataka kulaumu nani katika hili.
Nani anaajiri hawa watumishi wenye vyeti feki?Mkuu,nadhani kuna kitu unakimisi kwenye comment yangu,ipo hivi hao wahusika wanaotakiwa kushughulika na kutatua matatizo ya wananchi wanapokua na vyeti feki ina maana wapo kwenye hizo post kimagumashi,kwahiyo hata utendaji wao unaweza ukawa sio kivile.
Makampuni mengi ya kigeni barani Afrika yanafanya sana skill audit. Na hili inaanzia kwenye vyeti. Uchumi unaendeshwa na ujuzi sio credentials..Vyeti feki havikuwahi kuleta uchumi wa kati ndio maana walikimbilia kwenye uhujumu uchumi n.k vyeti feki watumishi hewa ilikuwa delaying strategy kuminya haki za watumishi. Imagine 5 years mtumishi anaimbiwa nyimbo za uhakiki vyeti feki watumishi hewa huku mshahara aliouacha jk ukiwa vilevile
Swala la kuongezwa mishahara.. ni swala la kuzungumza.Makampuni mengi ya kigeni barani Afrika yanafanya sana skill audit... Na hili inaanzia kwenye vyeti... Uchumi unaendeshwa na ujuzi sio credentials...
Duh.... Wewe sio mzima.Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:
1. Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2. Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa.
Serikali iliyopita ndiyo ipi mkuu?
CCM haitakiwa wahamiaji haramu, imerudi kwa wenyewe.Dr Slaa ni jembe. Yaani Magufuli atakuwa amefufuka na rais atapata usaidizi usio na shaka maana makundi ya ccm hayatawasumbua. Ilani itatekelezwa bila figisu.
Kuna post imefutwa muda si mrefu inasema kafanya ziara hazina na kukuta madudu ya kutisha.Habari!
Sina hakika kama mama Samia Suluhu ni member wa Jamiiforums ila nina hakika kuwa wapo member humu ambao wako karibu na Mama Samia Suluhu.
Serikali hii ya awamu ya sita awali ya yote wapitie account kuu ya serikali watazame kilichoingia na kilichotoka kuanzia pale alipoanza kutawala Rais Magufuli mpaka alipoishia.
Hii sio kebehi kwa marehemu bali ni kanuni ya fedha.
Watakapobaini madudu wahusika haraka wapelekwe selo na kesi zipelekwe mahakamani.
Mama usikubali kuanza alipoishia mwenzako, bali anza pako rasmi . Hii itakusaidia sana maana miaka yako ikiisha anaweza kuja Kiongozi ambaye anaweza kukupa kesi ambayo hukuhusika.
Namba 4 hapana hyo namba 6 upo sawasawa.1.Kama jina lake lilivyo awe mtu mwenye kupenda kupata Suluhu na wapinzani ili kama nchi tuwe wamoja.
2. Kitengo cha TISS akifanyie mabadiliko, Wanyarwanda waliokuwa wanamlida mtangulizi wake warudi kwao. Kwa kuwa Mama yetu wewe hauna maadui wengi, hata walinzi wa ndani watakuwa upande wako.
3. Mama nakushauri penda sana kufuata katiba na uongoze nchi kama Mama mlezi wa watoto. Ongoza nchi bila chuki na mtu, Watumishi wako wakikosea usiwatumbue majukwaani kwa kutaka misifa, fuata taratibu za kiutawala - ajieleze kisha mpe adhabu stahiki.
4. Malizia miradi yote aliyoianzisha mtangulizi wako.
5. Rudisha mahusiano mema na nchi za nje ili wafufue viwanda vyao walivyovifunga. Kisha usiwaite wao ni Mabeberu huo ni ubaguzi wa Kisukuma.
6. Mwisho shughulikia sana na mambo yanayowagusa mojakwamoja wananchi, mfano nyongeza za mishahara kila mwaka na ajira kwa vijana na mikopo nafuu kwa wajasiliamali wadogo.
*Nakutakia kheri kwenye majukumu yako ya Urais. (Niliwahi kumchukia mtangulizi wako, ila wewe wala sina sababu za kukuchukia). Najikuta nikikupenda bure nikiwa na furaha tele.
Usimpangie mh nini Cha kufanya jiandae kupigwa chini mkuu, hivi mwamchukulia poa, mh sio lazima afanye yale ya mtangulizi wake, hoja hapa KWA mh apate kambi mzuri ya kumshauri, na afanye KWA mjibu wa taratibu zake, na hii ndo shida kwamba tz hatuna dira ya kitaifa kwamba kila kiongozi ajae huja KWA mtazamo wake ,ni simple kutawala USA kuliko TZ , tunahitaji katiba mpya kabla ya Mambo mengineHongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli