Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Huoni kua pengine hayo matatizo mengi uliyo yasema yanaweza kua yanasababishwa na hao wenye vyeti feki?
Watanzania wala hawahitaji kukusanyiwa vyeti feki, Watanzania wanahitaji huduma bora za kijamii na huduma muhimu. Unaongelea suala la vyeti ambalo mwananchi wa Sombanyasoko hajui faida yake!

Maisha ya wananchi ni kipaumbele cha kwanza kwa Rais yeyote yule aliyepo madarakani. Wanaoajiri watu wenye vyeti feki ni taasisi binafsi au serikali kama ni serikali yenyewe ndiyo inaajiri watu wa hivyo unataka kulaumu nani katika hili.
 
Tumshauri awavuruge wasukuma vinginevyo wata m sarbotage, ondo wale wote wa ngazi za juu na panga safu upya, wenye sifa warudishe, ila Doto james muulize alimpa kibali ya kutoa pesa bila utaratibu wa Bunge, na pia ukitaka ufanikiwe achana na Ndugai, mnafiki na mjinga
Habari za wakti huu;

Kwanza kabisa nimpe Pole mama yangu ,Samia Hassan Suluhu kwa kuondokewa na Boss wake,Lakini zaidi nimpe hongera kwa kupata fursa ya kuwa RAIS wa Jamhuri katika kipindi ambacho Jemadari mwendazake JPM alikuwa ameweka moja kati ya malengo makubwa sana(Most ambitious goals of the Modern Tanzania) ya kutaka kufanya Tanzania iwe nchi ya kisasa.Lakini Pia niseme tu kwamba Mwendazake JPM amemuachia TAIFA ambalo kwanza ni divided yet united.Lakini pia anayo kazi ya Pembeni ya kufanya Damage control and healing

Sasa nirudi kwenye mada kuhusu nzi.Kuna nzi wengi sana ambao wamezagaa na najua mpaka wakati huu wengi tayari wameshaanza kujisogeza karibu.Kuna nzi wa aina mbili ambao wanajisogeza kwa kasi sana karibu na RAIS wetu Mama Samia Suluhu Hasan

Nzi wa Aina ya kwanza ni wale ambao walinufaika na Mfumo uliokuwepo zama za Magufuli ambao wanatafuta kila namna kuhakikisha kwamba Maslahi na fursa walizokuwa nazo kisiasa,kijamii na kiuchumi zinaendelea kuwepo na kuna wale Nzi ambao hawakupendezwa na mfumo ule na wengine hata kama waliufaidi lakini hawakuupenda na wengine ambao waliumia na hawakunufaika nao na ambao nao wanasogea kwa kasi kabisa ili waweze kubadili uelekeo wa Upepo.Hawa nzi wote ni nzi hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.

Najua wachache wa nzi hawa unawajua ila pia najua kuna ambao huwajua au hujaweza kuwatambua ila jihadhari nao.Mheshimiwa RAIS ninapoandika waraka huu ninawaona jinsi wanavyoweka mikakati, wengine wanafuatilia historia yako kujua kama kuna kitu wanaweza kukitumia ili kukufikia kwa urahisi uweze kusikia ushauri wao. Mimi nakusisitizia waepuke hawa nzi.Kazi uliyo nayo ni kubwa sana.

Mheshimiwa RAIS, Wewe ni mrithi wa Magufuli na jamii haitakuelewa kama utaachia kusimamia yale mema ambayo Mwendazake Magufuli aliyasimamia.Usije kushawishika kudharau kukamilisha baadhi ya miradi ambayo ina tija ambayo iko katika hatua za utekelezaji kwani utajishushi heshima yako wewe na utakuwa umeitukana kumbukumbu ya mtangulizi wako JPM ambaye kifo chake kimekupa nafasi ya kuwa rais wa nchi.

Hata hivyo usiogope kuonesha tofauti hasa katika maeneo ambayo kwa hakika Mtangulizi wako hakuwa sahihi.Ndio hakuwa mkamilifu.Kuna baadhi ya mambo mengi sana yanahitaji kurekebishwa na usiogope kuwa tofauti kwani wewe unayo haki ya kuweka tone ya uongozi wako.

Naendelea kukusisitiza kwamba kwa sasa litazame Baraza la Mawaziri, kuna watu hawatakiwa kabisa kuwa humo,watakuvuruga.Kumbuka moja kati ya heshima kubwa uliyo nayo ni kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mpya.Nafasi hio inakupa jukumu moja kubwa nalo ni kuukamilisha mchakato ule na kuhakikisha sauti ya wananchi inasikiwa.

Mama Samia, Wewe ni Mzanzibari, tena Mzanzibari kweli kweli Usisahau hilo.Fanya Jambo kuhusu Zanzibar

Sitaki kusema zaidi ila kama nikajaliwa nitaongeza mengine ila kwa sasa nikutakie kila la heri katika kazi yako ya kuendesha nchi yetu

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu Mbariki Mh. Samia H. Suluhu

Rais wa JMT
 
Watanzania wala hawahitaji kukusanyiwa vyeti feki, Watanzania wanahitaji huduma bora za kijamii na huduma muhimu. Unaongelea suala la vyeti ambalo mwananchi wa Sombanyasoko hajui faida yake!

Maisha ya wananchi ni kipaumbele cha kwanza kwa Rais yeyote yule aliyepo madarakani. Wanaoajiri watu wenye vyeti feki ni taasisi binafsi au serikali kama ni serikali yenyewe ndiyo inaajiri watu wa hivyo unataka kulaumu nani katika hili.
Mkuu,nadhani kuna kitu unakimisi kwenye comment yangu,ipo hivi hao wahusika wanaotakiwa kushughulika na kutatua matatizo ya wananchi wanapokua na vyeti feki ina maana wapo kwenye hizo post kimagumashi,kwahiyo hata utendaji wao unaweza ukawa sio kivile.
 
Mkuu,nadhani kuna kitu unakimisi kwenye comment yangu,ipo hivi hao wahusika wanaotakiwa kushughulika na kutatua matatizo ya wananchi wanapokua na vyeti feki ina maana wapo kwenye hizo post kimagumashi,kwahiyo hata utendaji wao unaweza ukawa sio kivile.
Nani anaajiri hawa watumishi wenye vyeti feki?
 
Vyeti feki havikuwahi kuleta uchumi wa kati ndio maana walikimbilia kwenye uhujumu uchumi n.k vyeti feki watumishi hewa ilikuwa delaying strategy kuminya haki za watumishi. Imagine 5 years mtumishi anaimbiwa nyimbo za uhakiki vyeti feki watumishi hewa huku mshahara aliouacha jk ukiwa vilevile
Makampuni mengi ya kigeni barani Afrika yanafanya sana skill audit. Na hili inaanzia kwenye vyeti. Uchumi unaendeshwa na ujuzi sio credentials..

Ila kama organization lazima uwe na pakuanzia. Uwepo wa vyeti feki unayo impact kwenye uchumi.. nafasi zinakaliwa na non trained people, ambao wanaweza kuwa Kigingi kwenye ufanisi wa utoaji huduma.

Kuna watu trained majumbani ambao serikali imewakopesha fedha wasome na hawana kazi maana zimekaliwa na non trained people..hawa waliokopeshwa wanalazimika kulipa mikopo hiyo ili na wengine wasomeshwe.. hilo haliwezekani maana nafasi zao za kuajiriwa zimekaliwa tayari.

Swala la kuongezwa mishahara.. ni swala la kuzungumza.. serikali ilipaswa kuwajulisha wananchi tufunge mkanda. Ukweli huwezi kutaka kujenga nyumbani kwako ujikomboe na gharama na adha za kupanga. la pia ukataka ule Bata kila weekend, dinning out na wife na watoto, excessive spending kwenye maswala mengine mengi.

Lazima useme katika kipindi hiki tutaishi kwenye nyumba isiyozidi kodi kiasi fulani, na tutajitahidi kumaliza mwaka kwa bajeti isiyozidi kiasi hiki.. ili fedha nyingine tuwekeze kwenye ujenzi. Sawa sawa na nchi.. watu hatujakufa, na je miradi hii itatusaidia!? Ndio! Lazima tujifunze kujitoa hata kidogo. Tunataka kupata tu, ila kujenga kinachotupatia.. hapana!
 
Makampuni mengi ya kigeni barani Afrika yanafanya sana skill audit... Na hili inaanzia kwenye vyeti... Uchumi unaendeshwa na ujuzi sio credentials...
Swala la kuongezwa mishahara.. ni swala la kuzungumza.

Hilo sio la kuzungumza ni takwa la kisheria usitegemee upendwe na watu unao wakandamiza for 5yrs kwa kutoa sababu hizi na zile. Maendeleo ayaende na kujali future za unao waongoza.

Unadhani wanaokaribia kustaafu wameathiriwa kwa kiasi gani viinua mgongo vyao? Nitamsifu mama samia emdapo atadili na vyeti feki hulu akipandisha madaraja watumishi na kujali stahiki zao.

Na nitamuomgeza kwenye orodha ya watu wasio jali endapo atashupaza shingo na kufanya yale anayo ona yanafaa kinyume na sheria.
 
Dakitari namba moja wa Rais, Viongozi wetu na Taifa kwa ujumla ni Waziri wa Afya. Hivi ndivyo tunavyoelewa sisi Wananchi inawezekana kwa taratibu zingine sivyo.

Dunia inatushangaa, na itaendelea kutushangaa na huenda tukatengwa endapo hapatakuwepo na mabadiliko ya makusudi.

Ninashangaa ni kwa nini Waziri wetu wa Afya hasemi ukweli kuhusu hali halisi ya Ugonjwa huu wa Covid 19 na Kuelimisha Umma ipasavyo nini cha kufanya,na kiwe kinalandana na wanachofanya wenzetu nchi jirani na duniani kote!

Bila shaka katika kipindi hiki cha Mazishi ya Mpendwa wetu Rais Hayati Dr. Magufuli, tumepokea Viongozi toka nchi jirani wakiwamo Marais. Wooote walionekana wamevaa barakoa,isipokuwa wa kwetu hapa Nchini, je ni kwa nini.

Hivi sasa naangalia TBC, kinachoendelea pale Chato, jana pale Mwanza, Juzi Dodoma si cha viongozi wala wananchi waliovaa barakoa! Ni viongozi wachache sana wamevaa. Tukumbuke,dunia inatuangalia, na ndiyo tunayotegemea kwa mambo mengi.

Kwa haya yote, Waziri wa Afya yuko Kimyaaaa! Ni nani alistahili kusimamia hili?

Tutaendekea kupoteza viongozi wetu kwa uzembe hadi lini? Nani afe ndo tuwekeane msisitizo wa kuvaa barakoa katika misongamano?

Niombe ikiwezekana, Mrudishe Mama yetu Ummy na Msaidizi wake Ndugulile. Useriousness wao tuliuona japo wakitoka kwa mazingira yasiyoekeweka.

Ni maoni yangu kama Mtanzania huru. Mungu akubariki na ulioni hili kuwa ni jema.
 
Mh Rais katka mambo ya kufanya hakikisha unafanya yafuatayo:

1. Futa wilaya ya Chato ibaki kata
2. Futa Mpango wa kuipa Chato Mkoa.
Duh.... Wewe sio mzima.

So pesa iliyowekwa kwenye hiyo miradi hapo ipotelee hewani?

Badala ya kumalizia hiyo miradi yote ili iweze kufanya kazi na kurudisha pesa iliyotumika wewe unasema aifute?!
 
Mimi kama miongoni mwa watanzania wenye shauku ya kuonja uongozi wako, tunaomba uteue makamu wa rais mwanamke ili tuwe na uongozi kamili kutoka kwa mwanamke.

Tumeona hata katika familia mwanamke akiwa mvumilivu kwa kiwango kisichoweza kabisa kulinganishwa na mwanaume.
Mwanaume akilemewa sana na changamoto huwa ana tabia ya kujipiga ganzi kwa pombe ili asiyahisi maumivu ya familia yake au wengine hukimbia kabisa na kutokomea kabisa kusikojulikana tofauti na mwanamke ambaye hupambana kwa njia zote mpaka mwisho kuliko kukimbia watoto wake.

Hivyo katika mifano hii tunaomba serikali yako iwe na wanawake wengi kuliko wanaume, hasa katika kumteua makamu wako mwanamke kama wewe ili sisi kama wananchi tupate huruma ya mama katika kuwaletea maoni yetu kwa uhuru kama tulivyokuwa tukipeleka maoni kwa wazazi wetu wa kike.

Sisi watanzania ni mashahidi jinsi mama zetu walivyojinyima hata wasivyopaswa kujinyima ili watoto wao tuweze kuwa na afya njema, kucheza, kusoma na kutuweka kuwa safi muda wote kuanzia mavazi mpaka akili.
Sipingi kwamba baba zetu nao walipambana vya kutosha katika malezi yetu, ila najaribu kukumbusha tu namna tulivyokuwa na mama zetu muda wote katika shida na raha za nyumbani kitu ambacho ni kigumu sana kwa baba zetu kuweza kuyaishi yale maisha tuliyoishi na mama zetu.

Mama wewe ni rais!.
Nakuomba tumia mamlaka yako yote tupate makamu wa rais mwanamke, ili tuweze kupata ladha tofauti kabisa ya kiuongozi maana sisi wanaume tumetawala miaka zaidi ya 50 na tumeweza kuuona uongozi wa baba.

Safari hii naomba tupate uongozi wa mama angalau hata miaka hii mitano.

Hii ni nafasi ya mama. Tunaomba tupate uongozi kamili wa mwanamke ili sisi kama wananchi tuchape kazi na muda wa mapunziko tudeke 😇😇😇

Hii ni awamu ya mama! Yaacheni maoni yangu hapa maana hata kwa mama yangu nilikuwa huru kupeleka maoni yoyote tofauti na kwa baba ambapo nilikuwa nikitaka kupeleka maoni kwake lazima nipite kwa mama, alafu ndipo yeye mama ayafikishe kwa baba.

Nanyi wanawake wa humu msilale.

Pigeni kelele hadi ile furaha ya mama kwenye familia ionekane na kwenye uongozi wa nchi.

Wanawake wanaweza hata bila kuwezeshwa!

Hakuna kama mama duniani
 
Ninachomshauri Mhe. SSH ni mambo yafuatayo; Sijui kama yameshatajwa katika uzi huu kwa sababu sijaweza kusoma kila post.
Mambo hayo ni:

1. Aachane na watu wanaomwambia afanye copy and paste kutoka kwa the ate JPM.

2. Aunde serikali yake au regime yake ambayo itafanya kazi kwa kutengeneza legacy ya SSH. SSH kwa sasa ndio Rais na tutamhukumu yeye kama yeye. Rais aliyepokea kijiti kutoka kwa JPM na sio Rais aliyemsaidia JPM kumaliza legacy yake.

3. Awe na vision ya anavyotaka kutuongoza. Hata kama hakuwahi kuota kuwa Rais basi ndio imeshatokea hivyo. Yeye ni Rais wa JMT sasa.

4. Aachane na majibizano ya maneno, kila anapopata nafasi ya kuhutubia Taifa. Yeye ni Rais. Hana sababu ya kumjibu yeyote bali kutenda kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Ilani ya Chama chake.

5. Kila anapopata nafasi a kulihutubia Taifa, ahutubie kwa kutumia hotuba iliyoandaliwa na Taasisi ya Urais Tanzania. Aachane na zile hotuba za matukio. Hazitamsaidia kitu. Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, alitumia mbinu hii na hadi leo Kenya wanamrate kama most successfull president in Kenya.

6. Ateue Waziri Mkuu wake mara tu baada ya msiba. Hii itamsaidia yeye kuheshimiwa na huyo PM na kumsikiliza yeye kuliko atakvyosikiliza masalia ya mfumo wa Rais aliyepita.

7. Afanye mabadiliko ya baraza la mawaziri. Hata reshuffle ya kawaida tu na kisha kutoa maelekezo mapya ya Rais kwa mawaziri.

8. Afanye mabadiliko(reshufle inatosha) ya makatibu wakuu na wakuu wa taasisi ya Umma. Hii itamsaidia yeye na nchi kupata hisia za kweli kwamba sasa wapo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Hii pia itawasaidia watu kuanza kutenda kwa kujiamini. Kwa sasa hakuna anayejua hatima ya nafasi yake. Maanake mfumo wenyewe tayari una anticipate mabadiliko wakati wowote. anticipation hizo hazitakuwa na mwisho hadi SSH afanye mabadiliko na reshuffle mbali mbali.

9. Afuate ushauri wa kitaalam. Rais ni mkuu wa nchi. Haimaanishi ataweza kubuni kila kitu kizuri kwa nchi. Wasikilize wachumi wa vyuo vikuu, wachumi wa BOT, Wanadiplomasia wako katika wizara ya mambo ya nje. Wasikilize watu wa ofisi yako. WASIKILIZE KADA zote muhimu za kitaalam.

10. Uunde upya Taasisi iliyopo chini ya Ofisi yako. Ikibidi uivunje kuwepo na vipande viwili. Kwa sasa moyo wa Taasisi kwa sehemu kubwa imejikita kwenye usalama tu hasa wa serikali na viongozi wake. Ujasusi wa maswala muhimu kwa Taifa umekuwa ndogo sana kwake. namaanisha ujasusi wa kiuchumi na kiteknolojia. mgawanyo wake naacha kwa ajili ya mjadala wa siku nyingine.

11. Fanya mabadiliko makubwa katika jeshi la polisi. Sifa za ajira na mafunzo yao yanahitajika mabadiliko haraka sana. Hata jina tu libadilike. Sehemu nyingi, polisi imekuwa huduma na sio force tena.

12. Wakumbatie sekta binafsi. Nakuomba sana mama, wajamaa wasikudanganye. Relaxed na Developed private sector itakusaidia ukusanye kodi kubwa bila stress. Ukisikia Malyasia, Singapore, Taiwan, Indonesia, Thailand wanaendelea ni kwa sababu waliruhusu sekta binafsi kuendelea. Huwezi kujenga miradi mikubwa bila stress usiporuhusu sekta binafsi kuendelea. Sijamaanisha kuwepo kwa tax holidays or exception.

13. Fanya mabadiliko ndani ya chama chako ili kupata kamati kuu inayoiamini, inayokutii na mwaminifu kwako. Nchi yako hii sasa mama.

14. Usiwe mchoyo kwa watumishi wa umma. Usiwe mbahili kiasi kwamba pesa inakosekana mtaani.

15. Mambo ni mengi. Miaka minne ni michache mama.
 
Habari!

Sina hakika kama mama Samia Suluhu ni member wa Jamiiforums ila nina hakika kuwa wapo member humu ambao wako karibu na Mama Samia Suluhu.

Serikali hii ya awamu ya sita awali ya yote wapitie account kuu ya serikali watazame kilichoingia na kilichotoka kuanzia pale alipoanza kutawala Rais Magufuli mpaka alipoishia.

Hii sio kebehi kwa marehemu bali ni kanuni ya fedha.

Watakapobaini madudu wahusika haraka wapelekwe selo na kesi zipelekwe mahakamani.

Mama usikubali kuanza alipoishia mwenzako, bali anza pako rasmi . Hii itakusaidia sana maana miaka yako ikiisha anaweza kuja Kiongozi ambaye anaweza kukupa kesi ambayo hukuhusika.
 
Habari!

Sina hakika kama mama Samia Suluhu ni member wa Jamiiforums ila nina hakika kuwa wapo member humu ambao wako karibu na Mama Samia Suluhu.

Serikali hii ya awamu ya sita awali ya yote wapitie account kuu ya serikali watazame kilichoingia na kilichotoka kuanzia pale alipoanza kutawala Rais Magufuli mpaka alipoishia.

Hii sio kebehi kwa marehemu bali ni kanuni ya fedha.

Watakapobaini madudu wahusika haraka wapelekwe selo na kesi zipelekwe mahakamani.

Mama usikubali kuanza alipoishia mwenzako, bali anza pako rasmi . Hii itakusaidia sana maana miaka yako ikiisha anaweza kuja Kiongozi ambaye anaweza kukupa kesi ambayo hukuhusika.
Kuna post imefutwa muda si mrefu inasema kafanya ziara hazina na kukuta madudu ya kutisha.
 
1. Kama jina lake lilivyo awe mtu mwenye kupenda kupata Suluhu na wapinzani ili kama nchi tuwe wamoja.

2. Kitengo cha TISS akifanyie mabadiliko, Wanyarwanda waliokuwa wanamlida mtangulizi wako warudi kwao. Kwa kuwa Mama yetu wewe hauna maadui wengi, hata walinzi wa ndani watakuwa upande wako.

3. Mama nakushauri penda sana kufuata katiba na uongoze nchi kama Mama mlezi wa watoto. Ongoza nchi bila chuki na mtu, Watumishi wako wakikosea usiwatumbue majukwaani kwa kutaka misifa, fuata taratibu za kiutawala - ajieleze kisha mpe adhabu stahiki.

4. Malizia miradi yote aliyoianzisha mtangulizi wako.

5. Rudisha mahusiano mema na nchi za nje ili wafufue viwanda vyao walivyovifunga. Kisha usiwaite wao ni Mabeberu huo ni ubaguzi wa Kisukuma.

6. Shughulikia sana na mambo yanayowagusa mojakwamoja wananchi, mfano nyongeza za mishahara kila mwaka na ajira na mikopo nafuu kwa wajasiliamali wadogo.

*Nakutakia kheri kwenye majukumu yako ya Urais. (Niliwahi kumchukia mtangulizi wako, ila wewe wala sina sababu za kukuchukia). Najikuta nikikupenda bure nikiwa na furaha tele.
 
1.Kama jina lake lilivyo awe mtu mwenye kupenda kupata Suluhu na wapinzani ili kama nchi tuwe wamoja.

2. Kitengo cha TISS akifanyie mabadiliko, Wanyarwanda waliokuwa wanamlida mtangulizi wake warudi kwao. Kwa kuwa Mama yetu wewe hauna maadui wengi, hata walinzi wa ndani watakuwa upande wako.

3. Mama nakushauri penda sana kufuata katiba na uongoze nchi kama Mama mlezi wa watoto. Ongoza nchi bila chuki na mtu, Watumishi wako wakikosea usiwatumbue majukwaani kwa kutaka misifa, fuata taratibu za kiutawala - ajieleze kisha mpe adhabu stahiki.

4. Malizia miradi yote aliyoianzisha mtangulizi wako.

5. Rudisha mahusiano mema na nchi za nje ili wafufue viwanda vyao walivyovifunga. Kisha usiwaite wao ni Mabeberu huo ni ubaguzi wa Kisukuma.

6. Mwisho shughulikia sana na mambo yanayowagusa mojakwamoja wananchi, mfano nyongeza za mishahara kila mwaka na ajira kwa vijana na mikopo nafuu kwa wajasiliamali wadogo.

*Nakutakia kheri kwenye majukumu yako ya Urais. (Niliwahi kumchukia mtangulizi wako, ila wewe wala sina sababu za kukuchukia). Najikuta nikikupenda bure nikiwa na furaha tele.
Namba 4 hapana hyo namba 6 upo sawasawa.

We mtu gani hujali maslahi ya watumishi?

Mazuzu tu ndo wanaomshangilia
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Usimpangie mh nini Cha kufanya jiandae kupigwa chini mkuu, hivi mwamchukulia poa, mh sio lazima afanye yale ya mtangulizi wake, hoja hapa KWA mh apate kambi mzuri ya kumshauri, na afanye KWA mjibu wa taratibu zake, na hii ndo shida kwamba tz hatuna dira ya kitaifa kwamba kila kiongozi ajae huja KWA mtazamo wake ,ni simple kutawala USA kuliko TZ , tunahitaji katiba mpya kabla ya Mambo mengine
 
Back
Top Bottom