Kwanza Madam President mie ni mwananchi wako,nakusalimia kwa salaam za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.#Kazi iendelee.Kwa kifupi nikupe ushauri/ujumbe/maoni ya kuwa uwe unatembelea nchi mbali mbali duniani ukiambatana na wafanyabiashara wa kwetu,pia uwaalike wenzio waje na wafanyabiashara wao ili sote,sisi na wao tunufaike. Uende kwenye mkutano wa uchumi Davos, uhudhurie Mikutano mbali mbali muhimu kama vile kulihutubia Mkutano wa UN,mikutano ya uchumi,uturudishe kwenye ramani ya dunia.
Turudishe uhusiano na nchi jirani,nchi za jumuia ya madola,nchi zilizoendelea,nchi za mashariki ya mbali kama Malaysia,South Korea n.k.Faida zake ni kuwa ushatangaza kuondoa urasimu kwa wawekezaji.hilo limefika na limewafurahisha wengi duniani zikiwemo nchi Tajiri na za Middle East. Tuanzishe Joint commision kwenye sekta mbali mbali na wenzetu.Mfano tembelea nchi ya Qatar ambayo wanazalisha Gesi kwa wingi Duniani.
Tuanzishe joint commision watatusaidia sana katika sekta hiyo.Pia la mwisho umeona ulivyoenda Uganda,wenzetu wamechukua tahadhari zote dhidi ya Covid 19 na ikakulazimu hata wewe, Your Excellency Madam President na Wasaidizi wako mvae Barakoa(Mask).Nasi huku utuundie hiyo tume haraka ili ije na ushauri ambao utaamua na timu yako.
Turudishe uhusiano na mashirika ya kimataifa kama vile Unesco, UNHCR, IMF, World Bank, ILO na hasa WHO. Namalizia kwa #Kazi iendelee.