ITOSHE KUSEMA BASI KWA MJADALA HUU KWA MASLAHI MAPANA YA CHAMA, SERIKALI NA WATANZANIA KIUJUMLA.
Ni takribani wiki sasa inaelekea tukiwa na mijadala mizito juu ya ripoti ya CAG kwa mwaka 2019/2020. Ripoti hii imekuja kipindi ambapo tumeondokewa na Rais wa JMT mtangulizi wa Rais wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan Jemedari na PanAfrikalism ambae kwa imani ya wanapanAfrikalism wameamua kumuita Son of Afrika au Shuj
ITOSHE KUSEMA BASI KWA MJADALA HUU KWA MASLAHI MAPANA YA CHAMA, SERIKALI NA WATANZANIA KIUJUMLA.
Ni takribani wiki sasa inaelekea tukiwa na mijadala mizito juu ya ripoti ya CAG kwa mwaka 2019/2020. Ripoti hii imekuja kipindi ambapo tumeondokewa na Rais wa JMT mtangulizi wa Rais wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan Jemedari na PanAfrikalism ambae kwa imani ya wanapanAfrikalism wameamua kumuita Son of Afrika au Shujaa wa karne hii 21.
Mama Samia Suluhu Hassan wewe ndie Jemedari mkuu wa nchi hii kwa sasa kutokana na kurithi mikoba ya Dr JPM aliefariki Dunia tarehe 17 March 2021. Kutokana na hayo yote tunakuomba sasa mjadala huu utoe tamko kama Rais itoshe kuamua hatuhitaji kumzungumzia marehemu kwani huo sio utamaduni wa mtu mweusi katika maisha yetu na katika hoja hiyo nina haya ya kusema.
Kwenye ripoti hii ya CAG tumeyaona madudu mengi yaliyofanywa na watendaji wa serikali ya awamu ya tano kwa upotevu wa mabilioni ya fedha za walipa kodi huku wananchi tukibakia na wimbi la umaskini, uhakika wa lishe, upungufu wa madawati na vyumba vya madarasa pamoja na mambo mengi ambayo yanatupa sintofahamu kwenye taifa letu huku ripoti hii ikiwa inamapungufu mengi ambapo kimsingi wapiga kelele na wanaoimba mapambio wamekuwa wengi na waongeaji pasi na ukomo ambapo kabla ya kifo cha Dr JPM hatukuwaona wakiongea wala kushauri na katika hili hapa ndipo panpoleta utata na kuona tunatengeneza kizazi cha kinafiki, wasaka tonge na watu ambao wanasaka tonge kwa maslahi yao na wala sio kwa maslahi ya nchi. Mambo haya nitayabainisha hapa nasi sote tuyaone, tutajadili na kuona wapi tunakwama.
1. Katika ripoti hii ya mwaka 2019/2021 tumeona kutoka kwa CAG akiwa mtoa hukumu badala ya muwasilishaji na mtoa ushauri kwa serikali katika ripoti yake na kuyaona mapungufu ya ripoti hiyo pasipo kuonyesha ukweli halisi.
2. Katika ripoti hii tumeona mahesabu ya wizara na taasisi za serikali huku baadhi ya ofisi hizo kukosa mahesabu yake. Ikiwa mwaka 2019 -- 2021 mhe Mama Samia Suluhu Hassan alikuwa Makamu wa Rais katika serikali ya JMT lakini hatujaonyeshwa mahesabu ya ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na wizara zilizo chini ya ofisi hiyo ya Makamu wa Rais wala ofisi ya wizara ya fedha kwa mantiki hii inaonyesha wazi ripoti hii ina mapungufu ambayo tunashindwa kuyaelewa mambo haya yana ukweli kiasi gani.
2. CAG ametueleza ya kuwa stand ya mbezi imetuletea foleni na hakukuwa na maelewano kati ya TANRODS na TAMISEMI juu ya ujenzi huo hapa anapaswa atufafanulie wazi aliona nini na kitu gani kinafanya atueleze hayo anapaswa kufafanua badala ya kutoa lawama na maneno ambayo tumeshindwa kumuelewa hivyo kwa mantiki hiyo anatudhihirishia hafai kuwa kwenye nafasi hiyo kutokana na kutokuelewa kazi yake ipasavyo.
3. Ripoti hii imetueleza ofisi ya Rais kufanya maamuzi bila kushirikisha Bunge kwa ununuzi wa Ndege, Vivuko na maendeleo mengine tunataka kufahamu kama wizara ya fedha haikuhusika pesa hizo zimetokaje bila waziri wa fedha wa kipindi hicho kuhusika, bank kuu pamoja na hazina? Na kama ni amri ya mtu kwanini mshauri mkuu wa Rais na maafisa wakuu hamkujiuzuru ili kulinda heshima zenu kitaifa kama alivyofanya mzee Warioba mwaka 1987 na mzee Lowasa mwaka 2007 ili wananchi tuamini yaliyotokea ni ufisadi?
4. Ripoti ya CAG katika wizara ya mali asili na utalii kuna upotevu wa fedha nyingi bila ya kuwa na risiti jambo hili hapaswi kulaumiwa Dr Kigwangala peke yake bali tujiulize katika wizara zetu kati ya waziri na katibu mkuu nani anahusika na fedha za wizara? Kama Kigwangalla alilazimisha fedha hizo kutoka bila ridhaa ya Bunge na serikali kwanini Katibu Mkuu wa wizara husika hakujiuzuru, Kamishna wa Tanapa na ngorongoro waliruhusuje fedha bila ya kuzungumza na management pamoja na wizara ambapo mtendaji mkuu wa wizara ni katibu mkuu?
5. Hii ripoti inaonyesha mapungufu mengi ambapo kimsingi ndege zetu za ATCL zimenunuliwa mwaka 2017 lakini tumeona sote tunaambiwa ATCL imeisababishia taifa hasara ya Bill 60 kwa miaka 5 mfululizo tunapenda kupata majibu ya jambo hili ili kulinda heshima ya kiongozi mkuu na mkaguzi huyu.
6. Ripoti hii imekuwa kama inamtafuta mtu zaidi badala ya kuweka wazi matumizi mabaya ya rasilimali za serikali kwa kikundi cha watu na hivyo kuondoa radha halisi kwa kuwashambulia watu na kufanya serikali ya chama cha mapinduzi kutokuonyesha nia ya dhati ya kuondoa umaskini na usimamizi mzuri wa fedha za serikali.
MAONI
1. Chama cha mapinduzi na serikali yetu tukufu inayoundwa na chama cha mapinduzi ijitokeze hadharani na kuyakataa haya kwa hoja ili kulinda heshima ya kiongozi wetu mkuu wa nchi anaetokana na chama cha mapinduzi kwani yeye alikuwa afisa mwandamizi wa serikali iliyopita na alishiriki katika mipango na matumizi ya rasilimali za nchi yetu ukizingatia alikuwa msaidizi wa Rais wetu Marehemu JPM.
2. Makamu wa Rais na mtaalamu wa Mipango alietufanikisha kuingia katika mfumo wa nchi zilizopo katika uchumi wa Kati katika Dunia hii ajitokeze na kuhoji au kuizungumzia ripoti hii ili tuiamini serikali yetu yetu kwa kazi nzuri na wanaweza kutuvusha hapa ukizingatia yeye ndie mtu wa mipango nauchumi katika wizara fedha.
3. Ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri Mkuu watueleze upotevu wa kiwango cha juu kiasi hiki katika wizara ya TAMISEMI na wizara zote ukizingatia waziri mkuu ndio msimamizi mkuu wa shughuli za serikali Bungeni alikuwa wapi kulieleza Bunge juu ya hili ni vizuri apate kutupati a majibu.
4. Spika wa Bunge na Bunge zima mnapaswa kutueleza ni kwanini mlikuwa mnapiga makofi tu katika kila miradi inayozungumzwa ndani ya bunge na mawaziri waandamizi wa serikali badala ya kuhoji kwa maslahi ya nchi na wananchi kama tulivyowapigia kura ili kuwa wawakilishi wetu?
5. Mhe Rais tunaomba ujitokeze hadharani na kuchagua kamati yako itakayoshirikisha vyama vyote vya siasa, wawakilishi wa wananchi pamoja na taasisi nyingine ili kupitia ripoti hii vyema ili kuja na majibu stahiki katika ripoti hii ukizingatia ya kwamba kuna mtaalamu mmoja wa hesabu ametueleza hawezi kueleza mabaya ya mkataba wa Bagamoyo kwa kuwa hajaiona mikataba hiyo huku akitueleza kwenye ununuzi wa ATCL na SGR kuna upotevu wa fedha nyingi na hapo hapo anasema hakuwahi kupewa wala kuiona mikataba ya ujenzi au ununuzi hii inaleta ukakasi.
6. Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan tunaomba ujitokeze hadharani ukemee na ukatae udhalilishaji huu unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa watu kuendelea kumkashifu mtangulizi wako Dr John Pombe Joseph Magufuri na kumtukana huku akiwa hasikii wala kuweza kujibu hoja hizo zote na hii itakujengea nguvu na msimamo katika chama na serikali yako kwani sasa tunakoelekea kuna mpasuko ambapo tunawaona wasaidizi wengi wa Hayati wakimgeuka na kumsema vibaya na kujionyesha kwako wako nawe huku ni wanafiki kwa hili kaa nao macho ni wasakamatonge tu na wala sio wasaidizi wako ambao wanaweza kukusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo. Kuendelea kumsema Dr John Pombe Joseph hakusaidii bali wanakurudisha nyuma wewe na hukupoteza kwa jamii na kushindwa kuangalia mwenendo wa serikali yako na mpangilio wa kumaliza kero hizo.
7. Kuzuia mjadala huu usiendelee kutatufanya tuwe wamoja na kukijenga chama chetu kwa mustakabali wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuruhusu mjadala huu uendelee ni kujijengea chama chema chetu sintofahamu na imani ya chama kwa kukubali kuruhusu utaratibu huu wa kuchambana na mwisho kutengeneza magroup kwenye chama na kwa wananchi.
8. Mama Samia Suluhu Hassan tunaomba utafute maoni kwa wananchi kati yetu ni nini kitangulie kati ya katiba mpya na sera ya nchi.
Kwa upande wangu ningependa uruhusu sera ya nchi ili kuondoa dhana ya kila kiongozi anapoingia madarakani kuwa na manifesto yake bila kuangalia Dira ya nchi kwa utaratibu huu tutaondoa ubadhilifu wa mali za nchi na utunzaji wa rasilimali za nchi yetu kwa maendeleo ya nchi na taifa.
MWISHO
Natoa rai kwa watanzania wenzangu maoni ya mtu hayapigwi nyundo bali hupingwa kwa hoja kwa maarifa ya juu. Hivyo tushirikiane katika majumuisho ya kumsaidia mama katika utendaji wake badala ya kujipendekeza kwa kusifia na kulaumu pasipo kutoa dira na mwelekeo wa kumsaidia mama katika uongozi wake.
Mama na Rais wangu nakuomba utulie na upambanue haya yanayofanywa na wapinzani ni sawa na chawa kwani chama cha upinzani kukusifia huku miaka yote walikuwa wakikichafua chama cha mapinduzi nawe ni mmoja ya watu waliokuwa maafisa wakuu katika serikali iliyopita hii ni kujitafakali na kuenenda vyema maana kelele nyingi humuondoa muwindaji katika mstari halisi.
Naomba kuwasilisha
ASANTE JOHN
aa wa karne hii 21.