Gerald .M Magembe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 2,496
- 1,800
Nchi zote duniani zenye chombo kinacho shugulika na usalama wa taifa lazima kitapata wa kukilaumu kwa muda tofauti tofauti kiutendaji.Enyi TISS, sisi raia wema huku mitaani tuna imani Sana na nyinyi,kusema kweli tunawapenda Sana,Sasa Mimi Lee kwa niaba ya Watanzania wema,tunawaomba mumshauri na mhakikishe amepokea ushauri huu mheshimiwa Samiha.
Nawe mama Samiha Rais wetu nakuomba upokee ushauri huu Ili kufanya Tanzania iwe na amani upendo raha furaha na haki,kwani haki huinua Taifa.
Ushauri wangu
Naomba TISS chombo chetu Watanzania,mshaurini Rais Samiha atengeneze taasisi imara ili zilete haki.
Baadhi ya taasisi imara Ni
Mahakama huru,
Bunge huru,
Polisi huru,
TISS huru,
Takukuru huru,
NEC huru,
N.k
Faida ya taassisi huru itamfanya atawale kwa haki,kwa urahisi,kwa raha na bila lawama.
Taasisi huru itawafanya TISS wawe na kazi nyepesi bila lawama kutoka upande wowote.
Polisi hawata onea raia,
Mahakama itaamua kwa Haki,
Bunge litafanya kazi kwa weledi,
Takukuru hawata mwonea mtu,
NEC haitalaumiwa,
TISS haita laumiwa,
Hivyo Mama ataongoza kwa raha bila lawama,yeye atasimamia kuleta maendeleo tu.
Mbali na hayo yote tunaomba Rais Samiha uruhusu katiba pendekezwa ya Jaji Warioba, ambayo wewe Rais ulikua Spika wa Bunge la katiba,tunaomba haya kwa Mustakabali wa Taifa.
Ukiruhusu hayo utatawala ka amani Sana.
Tunaomba Taasisi Imara.
Kazi kubwa:
Kukusanya taarifa muhimu za kisiasa za mtu, kundi, jamii au taifa na kuchakata.
kukusanya taarifa muhimu za kijamii za mtu, kundi, Jamii au taifa na kuzichakata.
Kukusanya taarifa muhimu za kiuchumi za mtu, kundi, jamii au taifa ziwe za ndani na nje ya nchi na kuzichakata.
Kukusanya taarifa muhimu za Kiusalama, za mtu, kundi, jamii au taifa na kuzichakata na kuhakikisha zinafanyiwa kazi ki uweledi na wote wenye kuhusika.
Na kukusanya taarifa zozote nyingene zitakazo onekana muhima mahala popote na kwa mtu, kundi au jamii yeyote ile ambazo Zita onekana zinazoweza kulisaidia taifa kwa maamuzi yeyote.
Kuhakikisha maslahi ya kitaifa kiujumla yanalindwa na kuchumgwa, ( to promote, preserve and protect national interests.).
Kuhakikisha kuna utabiri sahihi wa matokeo ya baadae ya Kisiasa, kiuchumi, kijamii, ki usalama na mambo yeyote Yale yatakayo lisaidia taifa.
Kuhakikisha kuna hafidhi ya kutosha ya taarifu zote muhimu na zimechakatwa na kufanyika kazi kiuweledi kwa matumizi ya taifa na zipatikane kiurahisi kila zinapo hitajika.
Wawe na uwezo wa ki ushawishi au nguvu za kisheria kupata msaada wa ki utaalamu wa taaluma yeyote ile kutoka kwa wabobozi ndani au nje ya nchi kwa malipo au ridhaa.
Taarifa yeyote ile ikusanywe, ichakatwe na ihifadhiwe kwa uwezo wa juu kabisa wa usahihi wa akili ya binadamu ikibidi kwa msaada wa vyombo vyote vile. Taarifa zisivuje na kutopungua thamani. Zipate uhifadi na ikibidi kuongezewa thamani kwa miaka isiyo pungua miaka 20.
Kwa hiyo lazima kuna sehemu ukizidi kiasi lazima utawakwaa tuu.