Habari za wakti huu;
Kwanza kabisa nimpe Pole mama yangu ,Samia Hassan Suluhu kwa kuondokewa na Boss wake,Lakini zaidi nimpe hongera kwa kupata fursa ya kuwa RAIS wa Jamhuri katika kipindi ambacho Jemadari mwendazake JPM alikuwa ameweka moja kati ya malengo makubwa sana(Most ambitious goals of the Modern Tanzania) ya kutaka kufanya Tanzania iwe nchi ya kisasa.Lakini Pia niseme tu kwamba Mwendazake JPM amemuachia TAIFA ambalo kwanza ni divided yet united.Lakini pia anayo kazi ya Pembeni ya kufanya Damage control and healing
Sasa nirudi kwenye mada kuhusu nzi.Kuna nzi wengi sana ambao wamezagaa na najua mpaka wakati huu wengi tayari wameshaanza kujisogeza karibu.Kuna nzi wa aina mbili ambao wanajisogeza kwa kasi sana karibu na RAIS wetu Mama Samia Suluhu Hasan
Nzi wa Aina ya kwanza ni wale ambao walinufaika na Mfumo uliokuwepo zama za Magufuli ambao wanatafuta kila namna kuhakikisha kwamba Maslahi na fursa walizokuwa nazo kisiasa,kijamii na kiuchumi zinaendelea kuwepo na kuna wale Nzi ambao hawakupendezwa na mfumo ule na wengine hata kama waliufaidi lakini hawakuupenda na wengine ambao waliumia na hawakunufaika nao na ambao nao wanasogea kwa kasi kabisa ili waweze kubadili uelekeo wa Upepo.Hawa nzi wote ni nzi hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.
Najua wachache wa nzi hawa unawajua ila pia najua kuna ambao huwajua au hujaweza kuwatambua ila jihadhari nao.Mheshimiwa RAIS ninapoandika waraka huu ninawaona jinsi wanavyoweka mikakati, wengine wanafuatilia historia yako kujua kama kuna kitu wanaweza kukitumia ili kukufikia kwa urahisi uweze kusikia ushauri wao. Mimi nakusisitizia waepuke hawa nzi.Kazi uliyo nayo ni kubwa sana.
Mheshimiwa RAIS, Wewe ni mrithi wa Magufuli na jamii haitakuelewa kama utaachia kusimamia yale mema ambayo Mwendazake Magufuli aliyasimamia.Usije kushawishika kudharau kukamilisha baadhi ya miradi ambayo ina tija ambayo iko katika hatua za utekelezaji kwani utajishushi heshima yako wewe na utakuwa umeitukana kumbukumbu ya mtangulizi wako JPM ambaye kifo chake kimekupa nafasi ya kuwa rais wa nchi.
Hata hivyo usiogope kuonesha tofauti hasa katika maeneo ambayo kwa hakika Mtangulizi wako hakuwa sahihi.Ndio hakuwa mkamilifu.Kuna baadhi ya mambo mengi sana yanahitaji kurekebishwa na usiogope kuwa tofauti kwani wewe unayo haki ya kuweka tone ya uongozi wako.
Naendelea kukusisitiza kwamba kwa sasa litazame Baraza la Mawaziri, kuna watu hawatakiwa kabisa kuwa humo,watakuvuruga.Kumbuka moja kati ya heshima kubwa uliyo nayo ni kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mpya.Nafasi hio inakupa jukumu moja kubwa nalo ni kuukamilisha mchakato ule na kuhakikisha sauti ya wananchi inasikiwa.
Mama Samia, Wewe ni Mzanzibari, tena Mzanzibari kweli kweli Usisahau hilo.Fanya Jambo kuhusu Zanzibar
Sitaki kusema zaidi ila kama nikajaliwa nitaongeza mengine ila kwa sasa nikutakie kila la heri katika kazi yako ya kuendesha nchi yetu
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Mh. Samia H. Suluhu
Rais wa JMT