Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Leo ni siku nyingine tena Rais Samia Suluhu aka Mama amepata wasaa wa kuhutubia wateuzi na taifa kwa ujumla.

Hotuba yake imesheheni matumaini mapya, lugha laini na rahisi kueleweka na kila mtu.

Mama ameonyesha kuifahamu nchi na matatizo yake kwa ujumla.
Amegusia karibu nyanja zote za kijamii, kiuchumi nakadhalika.
Huko kote ameonyesha kuwa naye anahitaji kuona mabadiliko hasa katika huduma bora.

Jambo lingine muhimu zaidi amwonyesha kuwa pamoja na kufukua cv za wateule wake pia hufuatilia sana maoni ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii, hii ni habari njema kabisa kuwa wengine tusiokuwa na access naye moja kwa moja tutakutana mitandaoni.

Jambo lingine muhimu ni kuqgiza vyombo vya habari vilivyofungwa vifunguliwe ili asionekane anakandamiza uhuru wa habari...hongera nyingi.

*******

Nimetumia kauli hii (kuwa ni mtamu) nikimaanisha kuwa Mama amevuta hisia za wengi kumaikiliza, lugha yake na lugha ya mwili/body language vinafufua matumaini mapya kwa wengi wafanyabiaahara, wakulima na wafanyakazi.

Tangu aapishwe kuwa rais wa JMT anga la Tanzania limekuwa jepesi mno, kuna tumaini jipya, mwelekeo mpya na amani ya moyo.

Mambo haya machache yamwnifanya nimuone kuwa huyu mama ni Mtamu.

ANGALIZO KWA MAMA
1. Utaimbiwa kila nyimbo tamu/praise and worship na kila kada hadi nyumba za ibada

2. Utaitwa mteule wa Mungu

3. Tutajikomba sana

Nakuomba usilewe sifa zetu.
Sisi hawahawa tunaokusifu ipo siku tutakupeleka msalabani kukusulubu uchi na viboko juu.
Kukwepa hili jitahidi kuyaishi haya unayoyahubiri itakusaidia usisulubiwe sana.

Mungu akutie nguvu

Namuombea hekima katika kutekeleza majukumu yake mazito. Asiyumbishwe na hoja zenye nia ya kuleta mtengano kwenye jamii. Asikubali wajanja wachache wakapenyeza agenda zao mbaya
 
Huenda Tanzania ikaangukia kua nchi yenye Watu wenye FURAHA chini ya huyu MAMA ,kila ninaemiona anaonesha sura ya Matumaini !???
 
Dunia hii kweli tunapita tu. Magu ndio basi tena. Utapiga kelele wee ila ukishakufa ndio basi tena
 
Yale macho kama amekula kungu toka Tanga kwa wadigo [emoji23]

Tafadhali kuwa na heshima yule ni Rais wa Tanzania.

Ingekuwa mama yako ungefurahia kuambiwa hivyo?

Uhuru wa kusema usizidi mipaka na kukiuka heshima na tamaduni zetu.
 
Kwanza kabisa lazima tutambue jambo la msingi ni kumshukuru raisi wetu anajua matatizo mengi sana kwenye hii nchi ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka sana na tayari ameanza kujikita hasa katika suala zima la uchumi wa taifa kuzidi kusonga mbele lakini pia kwa uchumi wa mtanzania mmoja mmoja kwa kutizama zaidi katika kuvutia wawekezaji waje kuwekeza katika sekta ya viwanda na madini na sehemu nyinginezo ili kutatua tatizo la ajira kwa watanzania na kupaisha uchumi wa nchi, hivyo naimani pesa itakuwa ya kutosha kwa watanzania wanaopenda kufanya kazi na suala la kuongea lazima awe huru sisi tunachotaka tuyafurahie maisha ya Tanzania basi kwani mtoa mada una uhakika gani lugha uliyotumia kwenye uzi wako kama kila msomaji kuridhishwa na maneno yako.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Binafsi naanza kuona vijembe na mizaha jukwaani. Mara mwenye jinsia ya kike, Mara macho yamelegea, hii yote ya nini? Kweli hadi hapo bado unataka sifa za maumbile? Rais akumbuke kuna kundi pembeni linaangalia kama kabadilika tabia.

Tabia wanayoifahamu tangu akiwa waziri na baadaye Makamu wa Rais. Sasa kama kuna tabia hataziacha, huo ndo upenyo wa kuingilia kuharibu mambo. Tutaanza kuona tena nchi inaendeshwa kwa vimemo vya ikulu.

Mtangulizi alikomesha tabia fulani za mitaani kwa tabia yake ya kutotabilika. Dakika moja mzaha mara mtu katumbuliwa. Sasa huyu rais mpya akataposhindwa kuachana na tabia zake walizozizoea huko maofisini, itakuwa ni kuwaangusha akina mama wote wanaofuata nyayo. Asidhani hazitembei huku mitaani. Amepanda jukwaa, soon tutaanza kuambiwa hata yasiyofaa kwenye jamii hii yenye masculinity.

Unapoteza muda.
Leo kasema kuwa anakeshaga mpaka alfajiri akiw amtandaoni.
ila nachojiuliza hivi huwa anatumia VPN.
 
Utasababisha jiwe atoke kaburini aje atuchambe alafu arudi kaburini kwake
 
Back
Top Bottom