Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Wakati tuko mbioni kupata Rais mpya wa sita katika awamu ya tano. Tunamsihi sana apate kutekeleza majukumu yake katika Maslahi Mapana ya taifa. Na apate kutambua pia maana ya kauli ya Maslahi Mapana ya taifa. Maana viongozi wengi huamini Maslahi ya taifa Ni katika vitu tu hususa (miundo mbinu, rasili Mali vitu, n.k) na hukomea hapo.

Kiuhalisia si hivyo, Maslahi Mapana ya taifa huanzia kuunganisha taifa lipate kuwa kitu moja bila kujali itkadi za aina yoyote si za kisiasa na si za kiimani na si kikabila wala za kijinsia. Lengo hapa ni taifa lipate kushikamana na kushirikiana bila chuki Wala ubaguzi. Utawala uliopita ndani yake ulikuwa na chuki na ubaguzi wa wazi wazi.

Pili Maslahi Mapana ya taifa ni upande wa kuindaa rasili Mali watu (wananchi), katika fikra na mawazo ya kisasa na kuwaondolea ujinga (kiufupi ni kuwekeza taasisi za elimu katika elimu ya kisasa ya kuendana na Karne ya 21). Elimu ya Sasa iliyipo nchini Ni duni, maana kwa asilimia zaidi ya 80 Ni theory oriented. Wananchi ndio taifa lenyewe, hawa wananchi hutegemea wameandaliwa na elimu ya ubora aina gani.

Kwa uchumi wetu hatuwezi kutoa elimu bure, na tukitoa elimu basi itakuwa Bora na si elimu Bora. Elimu Bora ni gharama.
Sasa Ni Bora tukawa wananchi elfu 20 wenye elimu Bora (quality education, compatible with 21 century environment) na tukawa wananchi million 60 wanaoujua kusoma na kuandika?

Tatu Maslahi Mapana ya taifa ni pamoja na Sera na Sheria wezeshi kwa wananchi wake. Mfano utawala uliopita Sera za Kodi Ni kandamizi, hazimuinui mwananchi. Tukumbuke mwananchi nae anapaswa kuendelea kiuchumi, na serikali inapaswa kuendelea kiuchumi. Sera za Kodi za Sasa so rafiki kwa mwananchi, Bali Ni rafiki kwa serikali. Kwa biashara za watanzania wengi hususa wa mtaji mdogo baada ya makato ya Kodi na Kodi ya pango hujikuta wamepata pesa ya kula, kuvaa, n.k hapati faida ya kumfanya hafungue biashara nyingine, kiufupi apigi hatua nyingine.

4: Maslahi Mapana ya taifa Ni pamoja na utawala Bora na taasisi imara. Tanzania haitaji kiongozi imara inahitaji taasisi imara za kiserikali. Maana taasisi hudumu Karne na Karne, lakini kiongozi ufa au humaliza muda wake. Ndio maana baada Magufuli alivyokufa watu wametandwa na hofu, yote Ni tokana hatuna taasisi imara, serikali ya awamu tano ilisimama si tokana na taasisi imara Bali raisi imara.

Taasisi imara husimikwa na katiba na Sheria za. Nchi, maanake ya Sasa katiba inapaswa kubadilishwa.
Iuwiiiiiiiiu uwiiiiiiiiiiihhhhh!!!! Mama hapana hapana Mama Kikokotooo kinaumiza Mama😭😭😭Kinaumiza Mama, kitatuua mama Wazee wenzako. Imagine Officer wa Serikali miaka ,38. Anaishia kulipwa 41m. Ana Madeni kibao Mama huyu Mzee ataishije?? Uwiiiiiiiiiiih!!??Kikokotooo Mama Mbona Umekikubali???
 
Mamii kwani Wazee ni wangapi wanastaafu Kwa Kwa Mwaka hadi wapunjwe hivi? Mama TuCTA wameshindwa kutetea Wazee Wastaafu. Kumbuka hatukuwahi kuongezwa Mshahara miaka 6. Huo Mshahara Mdogo ndio unalimwa Kikokotooo. Mama Inauma sana 40m utaifanyia Nini na Madeni juu. Mama please inaumiza.
 
Wameanza kukiri wenyewe bila shuruti kuwa nchi inaongozwa na mbumbumbu
 
Ushauri wangu kwa Rais Samia na watakao mfuatia taifa lianze kupima na kujenga miji kimkakati badala ya hii holela. Maeneo mkakati mfano beach plots zote zichukuliwe na serikali kwa manufaa ya umma kwa ujenzi wa mahoteli makubwa ya kitalii. Tuhanishe maeneo ambayo maji ya bahari ya tazunguka na kurudi baharini kwa kuimarisha utalii wa maji na pembeni ya tujenge majengo mkakati hotels,migahawa na bar kubwa. Tuanze kujenga flyovers ambazo hakuna gari linalo simama. Taa za barabarani zibakie ktkt ya miji siyo nje. Barabara zetu ziwe za kisasa kwa fly overs,taa za barabani na camera kuzibiti madereva wahuni na usalama.
 
Kama utafatilia Aya Mambo kwa umakini mkubwa na kufatilia kiundani siku Hadi siku tangu zilivyoanza hizi taarifa mpaka kufikia hii leo kwa namna ilivyo pande zote mbili alafu ukasoma text yangu vizuri na kwa utulivu mkubwa Utagundua kwamba mimi Sina Lakusema Asanteni sana.


Pangua ila usisahau wakuu wa idara
 
Kuanzia kitengo kikuu kabisa amuondoe bosi la mabosi maana kama vile mchongo wa kumchogoa aliyefariki kwa sababu ya ubaya wake hivyo na watoa amri ni hao hao wazee hata kama yeye alishiriki ila inabidi awageuke ili aweze kuendelea kuishi na kutawala lasivyo hahahahah
Endelea kidogo...
 
Siku hizi vijana mnachefua sana kwa uandishi wa kuacha h;
Aya =haya
Alafu=halafu.
Hivi mnaacha hii 'h' yanini?
 
Shikamoo Rais wetu!!

Pole kwa kazi nyingi za kiutendaji hapo ikulu. Ndugu Rais kama walivyo binadamu wote mahali popote duniani. Haijalishi tabia, tamaduni, hulka, kanuni na miongozo inaweza kuwa tofauti, dhamira huwa ni kujenga jamii yenye ustawi.

Naomba nishauri machache yenye lengo la kufanikisha utendaji wenye kuvuna ustawi taifa na jamii kwa ujumla.
1. Toa maagizo ya wakuu wa mikoa, Wilaya na Kata kusimamia kila kaya ipande miti mi4 kuzunguka eneo la Nyumba husika au ndani ya fence.

2. Usafi wa mazingira ujengeke kama kanuni ya msingi kwenye jamii, hapa niombe waziri mwenye dhamana utumie fursa ya celebrities kuonesha njia ya hio kampeni, hapa ni proper disposal ya garbages nyumbani, ndani ya vyombo vya Usafiri, sokoni, mitaani, sehemu za huduma etc.

3. Kutoa maelezo ya kina ya uchumi fungamishi unaochochewa na ujenzi wa miundo mbinu hasa barabara, reli, madaraja, nishat zote etc,

4. Ufuatiliaji wa matokeo ya utekelezaji maelekezo unayoyatoa mara kwa mara. Implementation, monitoring, evaluation na review intervention ni muhimu sana katika uongozi.

5. Toa maagizo ya kukomesha uzembe wa kiutendaji hasa katika mambo yasiyo ya kifedha ama kibajeti, ambayo kimsingi ndio dhana ya uwepo wa kiongozi, utawala na weledi wake, viongozi wengi wanafeli hata kwenye mambo yasiyo ya kibajeti mfano kuimarisha nidhamu, mashirikiano, haki kutendeka, upendo na umoja miongoni mwa watumishi.

6. Managing the unexpected as a leader ( kumudu mambo yasiyo tarajiwa) hapa panashida kubwa, mathalani projections of unexpected on every dimensions katika taasisi ama idara na etc
hili eneo naweka kiporo ntakuja na ufafanuzi wenye visa mafunzo vya kutosha kwa viongozi ama ngazi kadhaa.

7. Mazoea ya viongozi kutumia akili ndogo kwenye kwenye mambo makubwa, viongozi hawana hofu, wala aibu mbele ya umma, their responses are less informative and insightful. Hili eneo ni muhimu pia Kwa kuwa linajenga taswira mbaya ya nchi na jamii katika nyanja ya kimataifa.

8. Anza kujenga tabia ama taswira ya kuchukia usiyoyapenda na uyakemee na kukemea haina tafsiri ya ukali au kubwatuka, inherently human being are born lazy.

9. Chochea dhana ya ubunifu iendane na utendaji katika uzalishaji taasisi zenye maeneo ya mashamba zilime na uzalishaji wenye tija uonekane, tuachane na Utamaduni wa mashamba ya mafunzo ya mfano, taasisi Ina ekari 70, 100, 200 etc halafu zimelala hii hapana.

10. Tuanzie sasa kama nchi kiongozi wa kitaifa utuongoze katika kila eneo, iwe wizara, taasisi, shirika na etc. Tujiulize what can be done here that has not been done before, the eyes that can see potentials on varied aspects on local economy particularized cases and universally cases.

11. Kama kiongozi ikikupendeza ikianza na wewe ebu msijifungie kuna umuhimu wa kufungua milango kwa majungu rasmi na yasiyo rasmi. Make access easier to ur offices, kumekuwa na ongezeko la viongozi kujiweka mbali na vyanzo muhimu vya taarifa lishe za kimaendeleo na kiungozi. Taasisi nyingi viongozi wakuu hawaitishi mikutano ya wafanyakazi wote, fursa za mawazo mapya na ubunifu zinakufa kisa viongozi wapo ndani ya wigo mfinyu wa mawazo. Hii dhana ya kiongozi ndie mwenye akili na anajua kila kitu ni sumu katika taifa hili.

Naomba kuwasilisha haya machache.

Napokea uboreshaji

Wako mtiifu katika ujenzi wa taifa wenye tija jumuishi.

Ndimi kijana wako Wadiz mpenda fikra mtambuka.

Mungu abariki kazi zako na ufanisi wa Ikulu.
 
Mama yetu awe mkali sisi wa chini tunaumia Sana.

Kwa njia yyte unayoweza kulitafakari we are suffering huku chini.

Mama Samia ni tumaini sana
 
Mkuu

Ni vigumu Sana kukabidhiwa ghafla kijiti uka perform!

Anajitahidi MNO LAKINI kutokuwa na uhakika KWAKE juu ya hatma yake kitini, kuna mfanya aharakishe kula Angalau asije chekwa baadae!

Sasa HUWEZI kula huku ukizuia wenzako!

"Labda mambo yaharibike Sana"by JK!
 
Back
Top Bottom