Ni mradi gani rasmi tutakaokukumbuka nao!
Hela ulizokwisha kopa,hazilingani na tunachokiona site.
Ulianza na Ndugai ukamla kichwa!
Kosa amehoji kuhusu Mikopo!
Akaja mbunge wa kisesa Luhaga Mpina mkamla kicha U-Nec CCM!
Kisa amehoji kuhusu mikopo!
Leo umesema wazi kwamba atakayehoji kuhusu Mikopo ajiandae kudeal na Mwenye Serikali yake.
Gerald Hando amepoteza kazi EFM- Radio.
Kisa Mmiliki wa Radio ametishika na kauli yako uliyoitoa live kwa wanasiasa ukiwa Ikulu.
Kama unakopa mikopo nje,kumbuka pia ulipewa pia mabilioni ya Uviko!
Wananchi wanalipa kodi zote stahiki.
Tozo kwenye Miamala yetu inaendelea.
Ebu tuambie tofauti na miradi ya ujenzi wa mashule,ambao pia ni muendezo wa serikali ya JPM.
Ni kipi ambacho ndio mradi mkubwa uliobuniwa na serikali yako wewe kama wewe!
Maana!
SGR,JNHP,Daraja la Tanzanite,
Daraja la Busisi Mwanza.
Madawati nchi nzima,
Meli ziwa Nyasa,
Meli ziwa Victoria,
Masoko makubwa Mwanza,
Morogoro na Stendi za mabasi kubwa zote,Daresalaam mwanza na kwingineko.
Ujenzi wa Ikulu ya Dodoma.
Ni mawazo na miradi iliyoanzishwa na JPM.ingawa sasa mnasema watu wazuri hawafi.
Maisha mtaani yanazidi kuwa Magumu.
Bei hadi ya bidhaa za humuhumu mfano kama nyama ya ngombe ziko juu.
Wewe kila uchao ni.... safari,Makongamano,warsha na mikutano kila idara ya serikali ikiendelea ili tu waweze kula urefu wa kamba zao.
Hilo bwawa la Nyerere tuliambiwa mkandarasi alikwisha lipwa awamu ya tano.
Na hadi sasa yeye mkandarasi ndie alipaswa kutulipa fidia ya 1.5 trilioni kwa kuchelewesha kazi.
Lakini hatumsikii Makamba wala Maharage wakiliongelea hilo.
Pamoja na kuhojiwa hadi huko bungeni.
Usitutishe maana walipaji ni sisi wala sio wewe.
Wakati tukilipa,wewe utakuwa ukifaidi kiinua mgongo chako cha 80% ya mshahara wa rais atakayekuwa madarakani kwa wakati huo.
Vinginevyo tutahisi kwamba kuna namna hiyo mikopo haitumiki sahihi.
Kuliko kutisha wahoji mikopo,wewe ungedhibiti ufisadi uliotamalaki huko kwenye miradi inayoendelea.
Dhibiti wizi kwenye Force Account s za ujenzi wa miradi.
Sio kujifanya msafi kumbe na wewe unao upande wako.
Kwa sababu umeruhusu mikutano,subiri uanze kupewa za uso.
Machawa wamejaa humu sababu wewe unaleta na wao wanaiba!
Kwa nini wasikusifie.......