Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cc. Lucas mwashambwaHeshima kwenu wanajamvi.
Nisiwachoshe naenda moja kwa kwenye mada.
Zimekuwepo tabia za ajabu ajabu kama si kushangaza za kupenda kutoa sifa za kijinga hata zisizokuwa na maana.
Utasikia tunamshukuru Rais Samia katuletea fedha za kujenga matundu sita ya choo.
Rais ametoa Tsh bilion 15 za mbolea kwa wakulima wa Tumbaku Kaliua.
Rais ametoa Tsh milion 300 za upimaji wa makazi Kimanzichana.
Hizi fedha zote tunazoambiwa Rais ametoa ili tumshukuru,tumwabudu,tumnyenyekee,tumtukuze ni kodi zetu,mikopo ambayo tutakuja kuilipa na misaada.Fedha hizi upitishwa na Bunge letu kibogoyo.Sasa tunapoambiwa Rais katoa ni ushamba wa kiwango cha kusikitisha.
Kwakuwa watanganyika tumeendekeza ushamba,ujinga na uzwazwa nimeona si vibaya nikamshukuru Rais wa JMT nimeamka salama buheri wa afya.
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Je, Kimeshindikana nini kupatikana kwa haya yote uliyotaja kwa kipindi cha miaka zaidi ya 60 ya Uhuru wa nchi hii chini ya Utawala wa CCM???Katıka kutambua kuwa kila nafasi, cheo, uongozi hutoka kwa Muumba Mbingu na Nchi;
Nachukua nafasi hii kumpongeza Amiri Jeshi Mkuu na Raisi wetu Samia S. Hassan kwa uongozi wake mzuri na hivyo kulifanya Taifa liwe kwenye Amani.
Amani ni msingi wa maendeleo yote.
Binafsi naendelea kumuombea afya njema na Mungu amsimamie ili atimize ndoto za kutuletea maendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu ya barabara, maji, utawala bora, nk.
Watanzania tuna kila sababu ya kuishi maisha bora zaidi bila makasiriko.
- Tanzania yenye barabara bora, inawezekana
- Tanzania bila wafanyakazi wababaishaji, inawezekana
- Tanzania yenye kutii sheria bila shuruti, inawezekana
- Tanzania yenye umeme wa uhakika na wa bei nafuu, inawezekana.
- Tanzania yenye elimu bora, inawezekana
- Tanzania yenye huduma bora hospitalini, inawezekana.
- Tanzania bila wazembe, inawezekana
- Tanzania bila njaa, inawezekana
- Tanzania yenye ajira tele, inawezekana.
- Tanzania yenye watu wanaolipwa vizuri, inawekana.
Tanzania bora inawezekana chini ya uongozi wako.
Pambana Rais wetu, na Mungu akutie nguvu. Najua urais siyo kazi rahisi.
NINAKUBALIANA NAWE KWA MENGI, KASORO HILO LA MWISHO.Sina tabia ya uchawa!
Namuona Rais Samia akifanikiwa na akifanikisha maswala mbalimbali kwa weledi mkubwa.namuona kama mwamba wa kutoa majibu (decision maker) kwa maswala magumu bila kigugumizi.
Mdogo mdogo anatatua kero za nchi kwa kutazama kiini cha kero.
Mungu ampe maisha marefu na uongozi mwema.
Anatoa suluhisho kwenye maswala magumu bila uoga wa kukosea.
Anaamua pale panapohitaji uamuzi ili tusonge mbele.
Hakika hatukukosea kumpa hatamu.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!