Niliandika kwa kuchangia sehemu fulani, lakini naona ni muhimu niiweke hapa pia kama threat, kuna uwezekano ikatatua mgogoro huu. Jambo la kwanza, kabla hatujasoma hapa chini, tujue hakuna nchi isiyokuwa na serikali, hatuwezi kuishi tu kama wanyama kila mtu anajiamulia cha kufanya, na kupinga serikali hata inapofanya kitu cha maana tu. naomba msitukane, leteni hoja tujibizane.
1. Mwaka 1960 inasemekana Ngorongoro kulikuwa na raia 10,000 serikali serikali ililitwaa eneo lile, ikaamua wabaki tu humo humo. (mamlaka ya ngorongoro wapo wapi kufafanua hili?)
2. kufikia Mwaka huu, kuna masai zaidi ya 200,000 wanaishi na wanyama. tumeambiwa zaidi ya 100,000 wameenda msomela na pale wamebaki zaidi ya laki, hatujui idadi yao kwasababu wengine wanaenda na kurudi Kenya, wakiwa hapa ni watanzania, wakivuka ni wakenya.
3. Masai wanazaliana sana, kama mwaka huu wapo 100,000 ndani ya mbuga, kwa miaka 10 au 20 ijayo wanaweza kufikia 400,000, wote hawa wanaishi na wanyama. pia, kama wanahama toka kenya kienyeji, wanaozaliana na wanaohamia kwetu wataongeza idadi itakuwa kubwa sana ndani ya mbuga.
4. kwa miaka 30 au 40 ijayo, wanaweza kuzidi 700,000 ndani ya mbuga, hawa ni wanadamu zaidi ya wakazi wote wa jiji la Dodoma. wataishi na wanyama mbugani.
5. swali tujiulize, hawa watu wote wakiishi ndani ya mbuga, wanyama watakubali kuishi pamoja nao au watakimbia, na watakakokimbilia ni wapi kama sio kenya?
6. mbuga za kenya kuna wanadamu wanaishi na wanyama namna hii? jiulize, wanyama wakikimbia wananchi,wataenda hapahapa tz au wataenda nchi nyingine?
7. ndani ya ngorongoro hakuna hospitali na kwa tuliofika, hatuoni kuna maeneo ya mazishi, inamaana masai akifa wanazika wapi? au makaburi yapo kila watakapopenda kuchimba popote, hata mle watalii wanatembelea ni makaburi kwasababu mtu akifa wanachimba popote au nini, au tuamini ile tuhuma kwamba wanaachia fisi? (sina uhakika ni tuhuma).
8. Ardhi yote nchi hii kisheria ni mali ya uma, ipo mikononi mwa Rais, akiamua eneo lolote hapa analipora na kukupa fidia, kama ulikuwa unamiliki. ardhi ya ngorongoro kiumiliki sio ya masai kwasababu masai waliruhusiwa kuchunga ndani ya ardhi ya mamlaka tu baada ya mamlaka kuitwaa na kuimiliki, badala ya kuwafukuza wakasema wabaki ndio kosa lililofanyika, huruma zilizidi. ni sawa na wewe una shamba, mtu akasema naomba niwe nalisha ng'omba humo ukamruhusu, miaka nenda rudi ukataka aondoke akagoma, ukamjengea nyumba msomela hataki kwenda anasema pale ni pake.
9. mikoa mingine kwenye mbuga, makabila mengine yamenyang'anywa ardhi sana, ardhi za vijiji, na misitu ya hifadhi, watu hawatakiwi kugusa kabisa humo. kwanini makabila mengine waporwe ardhi ili mbuga ziendelee ila masai wagome, ni watanzania zaidi ya wengine?
10. tukiweka ushabiki pembeni, fikiria kama mtu mwenye akili timamu bila mihemko, kweli kwa miaka 20 ijayo bado patakuwa na mbuga pale wakati watu wanazidi kuzaliana namna ile na wanajenga nyumba za kudumu? au tumeamua kuteketeza mbuga ife kabisa ili ardhi waendelee nayo wamasai. ni uamuzi tu kwasababu ngorongoro ni ya kwetu, mali yako unaweza kuamua kuiteketeza au kuihifadhi, ndio maana watu wanabomoa nyumba ya kuishi wanajenga duka. je? bado tunaihitaji? kama jibu ni ndio, masai waondoke haraka sana na wawe na adabu kwa serikali.
11. kwani wamasai hiyo ardhi ikigeuka jangwa (majani huwa yanaisha), wataendelea kuishi hapo, si wafugaji wa kuhamahama,wakiona malisho yameisha pale watahamia kwengine? hoja hasa ya wanaosema masai wabaki pale ni nini?
12. kama fidia hata kama hawamiliki ile ardhi (hawana titles/hati ile ngorongoro conservation authority wana hati), si wamepewa fidia hivyo hivyo hata kama hawastahili kujengewa nyumba ambazo hawajawahi kumiliki maisha yao yote kule msomela?
13. au wanataka wakae pale ili iwe rahisi kwenda na kurudi kenya? masai tunaishi nao tumesoma nao, mbona wengi ni wakenya na wamesoma hadi shule za msingi kenya na wengine tunao humu makazini, ni wakenya. hatusemi wote wakenya ila substantial number yao huwa wana makazi kote na wanapita tu mpakani kama wakenya na wakirudi watanzania.
FIKIRIA!