Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hawa manspaaa wa kufukuza wote ...Yaani kama kuna sehemu ya kutimua kabisa Basi ni Manispaa za Dar es salaam. Hawa ni zaidi ya TRA . Hawa ndio walio toa tenda kwa makampuni ya Ridhwani Masha na Silaa ambayo wamegawana wilaya.

Wameshindwa kuzoa taka na hakuna anaye wauliza. Ni wakati wa kumuondoa mkurugenzi kwa unafiki. kwani ukimuona mtu anahimiza usafi sasa utadhani wakati wa kikwete alizuiwa kufanya usafi? ni unafiki ..wanajipendekeza.

tunahitaji mawazo mapya katika kuliendesha hili jiji ,JPM futa ajira za hawa jamaa .
  • WAFANYA KAZI NI WENGI SANA WAMEPEANA NA WAPO WA HEWA.
  • MABANGO YA MATANGAZO YAPO KWA MALAKI NA MOJA DOGO LA 2X3 MTS BASI UNALIPA TSHS 250,000 KWA MWAKA . KUNA MABANGO ZAIDI YA 500,000 JIJINI. KILA NYUMBA MJINI INA MABANGO 30 KWENDA MBELE ..SEHEMU HII PEKEE INATOSHA KULIINGIZIA JIJI MAPATO YA KUTOSHA LAKINI ASILIMIA KUBWA YANAKWENDA MIFUKONI NA RUSHWA
  • MA BILLBOARD YAPO KIBAO MJINI. BILLBOAED MOJA KUTANGANZA KWA MWEZI NI TSHS 10,000,000 . KUNA YALE YA SCREEN BEI YAKE IPO JUU. HAYA NI YA WATU BINAFSI LAKINI CITY UKIWAULIZA KATIKA HIZO 10M WAO WANAPATA NGAPI BASI NI AIBU KWA WIZI .HAYA MAPATO YANGEWEZA KUONDOA MASHIMO YOTE MJINI NA BARA BARA ZETU ZIKABAKI NZIMA BILA YA MASHIMO MWAKA MZIMA NA IKAWA HIVO KUENDELA
  • CITY INA CHUKUA 0.3% KAMA CITY LENVY HII INALIPWA QUARTERLY. NA UNALIPA KWA TURNOVER YAKO ...NI FEDHA NYINGI MNO ...ANGALIA JIJI HILI BIASHARA ZOTE ZIPO HAPA...MA BANKS KIBAO, MAKAMPUNI YA INSURANCE , VIWANDA , UAGIZIAJI NA USAFIRISHAJI , MADUKA MAKUBWA YAPO DAR ...0.30 YA TURNOVER YA DAR ES SALAAM INAPEWA CITY YA DAR ES ALAM...HAKIKA ZINATOSHA KUONDOA KUJENGA BARA BARA ZOTE MPAKA ZA NDANI NA KUPANUA ZOTE KUBWA BILA YA KUOMBA..LAKINI WAPI HAKUNA KITU ZINAYAYUKA AU HAWAKUSANYI KWA KUPEWA KITU KIDODO.
  • HAWA WANAKUSANYA PESA ZA LESENI ZA BIASHARA ...BIASHARA NA MA OFFISI DAR NI KILA PEMBE ..LESENI YA CHINI NI 100,000 KWA MWAKA HEEBU JPM ANGALIA ..KUNA FAINI , VIBALI VYA KUJENGA, TAXI MAGARI , MADALADALA , MALORI , CANTERS WOTE WANALIPA CITY...
  • KUBWA LAO NI PARKING ....KWA WASTANI MAGARI 100,000( INAWEZA KUZIDI HAPO)YANA PARK HAPA NA KULE JIJINI , KUANZIA ASUBUHI MPAKA JIONI PARKING ALMOST ZOTE ZIPO FULLL..WASTANI WA 2000 KWA SIKU NA WANA KUSANYA 200, 000, 000 KWA SIKU ...KWA MWAKA FANYA HESABU JPM...MR MAGUFULI..NI NYINGI MNOO...JEE KWELI KUNA HAJA YA KUWALEA HAWA WATU WA CITY ? NA LEO WANAKUJA NA KUJIKOMBA ILI KUFICHA UOZO NA UFISADI ?
JPM VUNJA HII KURUGENZI . TUNAHITAJI WATU WACHACHE WASOMI NA WENYE MAWAZO YA KISASA KULIENDELEZA HILI JIJI. HAKIKA UNAHITAJI KUFIKA HAPA KUSAFISHA.
 
Kumekuwa na shakashaka kua tatizo la nchi ni uwepo wa mifumo inayolea wahalifu niwaombe wanajamvi tupendekeze mifumo ya kufumuliwa ili rais wetu apate pa kuanzia
 
NAPENDEKEZA: Katika kubana matumizi ya Ovyo serikalini, ingefaa sasa Viongozi/Watu Maarufu wanaopitaga VIP kabla ya kukwea Pipa walazimike kuchangia/kulipia kwa pesa zao za mfukoni (sio kulipiwa na ofisi zao kama ilivyokuwa awali) ili kutumia huduma hiyo. Hili litaingizia Serikali pesa nyingi badala ya kuwalipia viongoz hao gharama za kupitia VIP kila wasafiripo na Ndege!
 
Wazo ni zuri sana ila waanze kuwanyanga'anya Wabunge na viongozi wastaafu (Kuanzia Mawaziri Wastaafu, Makatibu wakuu wataafu) zile DIPLOMATIC PASSPORTS
 
VIP ni uchochoro wa kupitisha bidhaa haramu. ifungiwe kabisa
 
Kila chama kilikuwa na ilani yake, sasa kusema ampe ubunge then cheo anachostahili Serikalini una maana gani? Je akiwa serikalini atakuwa anatekeleza ilani ipi kati ya ile ya ACT ya kwake na hii yenu ya CCM?

Malim Seif anatekeleza ilani gani kwenye serikali ya mseto Zanzibar?
 
Kwa spidi hii miaka 5 itakatika na asilimia 70% ya majipu yatakuwa bado hayajatumbuliwa.
Unashauri spidi (mwendo kasi) gani utumike maana majipu na vijipu nchini kwetu ni mengi kinoma?
Au aturuhusu na sisi huku tuwe tunayatumbua?
 
Kwa spidi hii miaka 5 itakatika na asilimia 70% ya majipu yatakuwa bado hayajatumbuliwa.
Unashauri spidi (mwendo kasi) gani utumike maana majipu na vijipu nchini kwetu ni mengi kinoma?
Au aturuhusu na sisi huku tuwe tunayatumbua?

Thubutuu, mengine hayatumbuliki kirahisi.
 
Habari wana JF!

Kilio cha wananchi wengi watanzania na baadhi ya wafanyakazi wa umma na sekta binafsi wamekuwa wakizilalamikia sana baadhi ya halmashauri nazo zikiwa zikifanya madudu katika utendaji wao.

1. Kuna upigaji dili sana kwenye halmashauri hizi.

2. Watendaji wengi wamewekwa kwa maslahi ya chama na hawana elimu za kutosha kuwa wabunifu.

3. Rushwa imekithiri jamani.

4. Halmashauri zingine kuonana na watendaji wengine kama mkurugenzi au mafisa husika ni tatizo kubwa, wanakuwa kama Mungu maofisi.

5. Kupitisha document inakuradhimu uchukue miezi mitano wakati document ya muhimu inayohusu ugonjwa, likizo ya uzazi ama uamisho wa kubadilishana.

6. Wengi wana lugha chafu kwa wanaowahudumia, unyanyasaji wa kijinsia. Na ukiukwaji wa sheria.

7. Wengi wanajiamulia kukata mishahara ya wafanyakazi wakishirikiana na wafanyakazi wa benki husika bila hazina kuhusishwa ilisuala lina ufisadi ndani yake bila hata kupewa barua husika kwa mtumishi alie enda kinyume na sheria za kazi.

Najiuliza hivi ni kwanini haya? Help.
 
naunga mkono hoja. kwa mfano sekta ya ELIMU kuna wilaya nyingi ambazo maofisini kuna data zinaonyesha kwamba walimu wa shule za msingi wanatosha. lakini ukienda mashuleni unakuta hali ni tofauti. shule nyingi hasa za vijijini hazina walimu kabisa. maafisa wa elimu wanaopika data wawajibishwe...
 
Nhisi hakuna jipya utendaji wa Rais Magufuli. Huu ni wajibu wake tena hajatimiza ndoto za usawa, haki kudhibiti mauaji ya ovyoovyo, kujilimbikizia mali na mengine mengi. Kinacho tufanya tushangae sikioni. au tunashtushwa na matukio?

Anachokifanya ni kuuanika uozo uliomo serikalini. Hamna jipya bali yote haya yalipigiwa kelele na Slaa 2010. Tena mengine mengi bado hajayagusa. najaribu kuamini msemo wa Roma kwamba UCHAFU WA MRISHO UNAMFANYA MSAFI AONEKANE BENJA.

KUNA sehemu nyingi sana tunaporwa. kodi zinapotea, misamaha mikubwa ya kodi kwa makampuni, ukimbizwaji wa mbio za mwenge, mishahara minono kwa baadhi ya watumishi, katiba mbovu, madai ya walimu, mishahara hewa, undugu makazini.baadhi ya vyeo visivyo muhimu serikalini tena vya juu(mikoa na wilaya). Tanzania ni kichaka chenye kira mnyama, ukirusha jiwe utasikia ushamtungua mmoja.

Anaiacha uchi serikali iliyoongozwa na watangulizi wake, mda naye tutayasikia yake.
 
naungana na wewe!mfano mzuri ni halmashauri ya manispaa Morogoro,yaani kuna watu pale huwa hata sielewi wamewekwa pale kwa vigezo gani,ni nyodo mpaka basi,pale utumishi kuna miungu watu,kwa kweli hata mimi naonelea ni vyema mamlaka za juu zifanye uchunguzi kuhusu uhalali wa nafasi za wale vikalagosi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom