Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Ningeshauri kuwa, Mhe. Rais angelimchagua Mhe. J. Mbatia kuwa Waziri Mkuu, ingekaa vema sana. Ni vema kutoangalia uvyama, udini, ukabila na matabaka mengine kama anavyo fanya Mhe. Rais na watendaji wake wa karibu. Team hiyo ya watendaji wa Mhe. Rais ingependeza sana na kuwa na ufanisi mkubwa pasipo na shaka kama angeli kuwa na Mtendaji Mkuu anaye mtanguliza MUNGU WETU ALIYE MKUU, UZALENDO na sifa zingine za kututoa hapa tulipo na kutupeleka pazuri.

Amri kuu za MUNGU zinaonyesha wazi kuwa ya kwanza ni kumpenda MUNGU na ya pili ni JIRANI YAKO. Hiyo ni kinyume na ufisadi unaoumaliza Taifa letu.

...Mama Tanzania... utu.....Tunaomba MUNGU atupatie mawaziri wanao mtanguliza MUNGU NA WAZALENDO.

Nawasilisha.
 
Hawa watu ni wazalendo kwelikweli....wakipewa nafasi za wizara nyeti hasa uchumi na viwanda TZ itapaa na kuwa 5 bora Afrika.
Nchi hii ina kula kitu kasoro uongozi bora wenye tija ya mapinduzi ktk uchumi.
Pia yule kijana Polepole apewe nafasi nyeti katika chama ili kuweka misingi bora ya chama.
 
Ni maoni yako lakin kumbuka ni kigeugeu na mtetezi wa fisadi angekua na msimamo angefaa undumula kuwili ndo umemshusha hafhi kujali tumbo lake badala ya wananchi
 
Huyo jamaa unamuona yuko sawa kweli. Ni mtu ambaye hafai kuwa hata classmonitor achilia mbali ubunge...ana tamaa ya ajabu siumemuona alivyokuwa anakula hela ya mamvi...
 
Kwa hizo comments kama ni kweli, basi na withdraw my suggestion. Pia naomba kujua ni nani anafaa?
 
Hapana Dr.Slaa hana maarifa nayo, yeye kabobea kwenye masuala ya sheria za kanisa katoliki, kumteua Dr. Slaa itainekana ni kulipa "fadhila". Mawaziri wote inapendeza wawe na weledi wa sekta wanazosimamia. Lipumba anastahili kwa vile ana merits.
 
Katika toleo letu la jana ukurasa wa mbele, tulichapisha habari yenye kichwa cha habari `Duh! Maumivu, hivi ndivyo mashangingi yanavyofilisi.' Habari hiyo ambayo chanzo chake ni uchunguzi wa gazeti hili, ilijikita zaidi kueleza jinsi utitiri wa magari ya kifahari aina ya VX-V8 na mengineyo ya aina hiyo maarufu kama mashangingi yanayotumiwa na viongozi waandamizi serikalini yanavyoligharimu taifa mabilioni ya fedha kila mwaka.

Habari hiyo imeeleza kwa kina bei ya shangingi moja pamoja huduma zake kwa ujumla na kubainisha kuwa ni mamilioni ya fedha hutumika kila mwaka ambazo kama viongozi wakiamua, zinaweza kuelekezwa kwenye maeneo mengine ya huduma za kijamii. Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali lukuki yakiwamo madini, ardhi, vivutio vya watalii na sasa imegundulika gesi mkoani Mtwara, kuzitaja kwa uchache.

Rasilimali hizi zikitumika kwa maslahi mapana ya taifa, Tanzania haipaswi kuitwa maskini! Haipaswi kuitwa hivyo kwa sababu ina kila nyenzo muhimu ya kuundoa umaskini isipokuwa tatizo liko kwa wachache wanaopewa dhamana ya kuzisimamia. Lakini kwa bahati mbaya, baadhi ya viongozi wenye dhamana hizo, badala ya kuweka maslahi ya Taifa mbele, hutanguliza ubinafsi.

Tumeshuhudia baadhi ya viongozi baada ya muda mfupi wakishakabidhiwa madaraka hubadilika haraka kimaisha. Utakuta mahekalu yanasimamishwa mithili ya uyoga maeneo mbalimbali ya miji kama Masaki, Oysterbay, Mikocheni, Mbezi Beach na mengine kama hayo katika miji mingine maarufu hapa nchini.

Wengi wamegeuza utumishi wa umma kama `ulaji' na matanuzi tena bila kuwafikiria hata wananchi wanaowaongoza. Tunajiuliza kwa mfano, hivi gari inayomfaa waziri, naibu wake, wakurugenzi na vigogo wengine wa serikali, ni mashangingi tu? Inasikitisha kuona nchi kama Tanzania ambayo kila uchao tunaimba kuwa ni maskini, viongozi wake wanatanua kwa magari ya kifahari na kuendelea kuwaumiza walipa kodi ambao baadhi yao hushindia mlo mmoja kwa siku.

Shukrani za pekee zimwendee Rais Dk. John Magufuli, kwa hatua ambazo ameanza kuzichukua katika kukabiliana na hali hiyo.

Mara baada ya kuanza kazi mapema mwezi uliopita, Rais Dk. Magufuli amechukua katua kadhaa za kubana matumizi yasiyo na tija. Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kuzuia sherehe za wabunge kupongezana, iliyowezesha kuokoa zaidi ya Sh. milioni 200 zikanunua magodoro na vitanda 300 Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Vile vile, Rais Dk. Magufuli amepiga marufuku sherehe ya Siku ya Uhuru iliyokuwa ifanyike Desemba 9, mwaka huu na kuwezesha kupatikana kwa fedha za upanuzi wa barabara ya Morocco na Mwenge, Dar es Salaam. Aidha, amezuia maadhimisho ya Siku Ukimwi Duniani, yaliyokuwa yafanyike kitaifa mkoani Singida Desemba Mosi na kuagiza fedha za shughuli hiyo zitununue dawa za waathirika wa ukimwi.

Hayo yote yamefanyika katika kipindi kifupi kisichozidi mwezi mmoja tangu aingie madarakani. Tumejifunza kitu kikubwa kwamba, kumbe inawezekana isipokuwa kinachokosekana miongoni mwa watendaji wa serikali ni dhamira ya dhati ya kulijenga taifa.

Tungewaomba viongozi wetu serikalini, sasa muachane na kasumba ya kutaka kutumia magari ya kifahari na matumizi yasiyo na tija ili taifa hili liwe la asali na maziwa kwa wote.
Mungu Ibariki Tanzania.

Source: Nipashe
 
Umekuwa muhubiri mkuu wa umoja na utengamano tangu utangazwe kuwa Rais wa Tanzania, Naomba kutokana na utumishi uliotukuka wa Dr. W.P Slaa umpatie wizara ya TAMISEMI, Hii ni kutokana na kazi aliyofanya ya kutukuka kama makamu mwenyekiti wa kamati iliyosimamia TAMISEMI wakati wa bunge la Kasi na Viwango.

Kama ambavyo umekuwa ukihubiri Tanzania ni yetu sote, mpe Dr. Slaa wizara hii na hakika ataendana na kasi yako na PM.

Wasalimie Magogoni

MJ
 
dr slaa na lipumba hi hazina kwa serikali ya magufuri
 
Kwa mwendo anaokwenda nao makufuli asahau kabsa kupewa nafasi ya uenyekiti wa chama,nasema hivyo kwasabu mpaka sasa ccm kimeanza kuhofia kasi ya magufuli ikiwa ni pamoja na kugusa maslahi ya viongozi wa stafu wa chama cha mapinduzi.Chama kama mwenyekit wa ccm taifa wameshaanza kuhofia maslahi yao endapo watamkabidhi magufuli nafasi ya uenyekiti wa chama taifa.kuna kila dalili ya vikao vinaanza kufanyika ili kutengenisha kofia hizi mbili ili kumdhibiti magufuli
 
Raisi ameonyesha nia ya dhati kuhakikisha kila mwenye kustahili kulipa kodi analipa ana kila fedha ya kodi inayolipwa inatumika vizuri.

Mambo haya uyafutilia kwa kutumia akili ya wanadamu tu ni kubwa na ngumu lakini kama mifumo kama vile vitambulisho vya taifa itawekwa na kupiga marufukufu transactions kwa kutumia cash kila kitu kikawekwa in electronic na huduma zote ziktolewa kwa kutumia mifumo ya network inayolink na system za wakazi za taifa effiency katika kuhakikisha kila mmoja analipa kodi na pengine mtu hatumii fedha nyingi kuliko kipato chake itaondolewa.

Mfano kama kila mwajiri anatakiwa kweka data za wafanyakazi wake kwenye system ya mamlaka ya vitambulisho vya taifa pamoja na kiwango cha mshahara, mshahara lazima upite benki na kwenyewe kuna mawasiliano na system na kila kitu aachonunua mtu anatumia namba yake y utaifa na system inakusanya takwimu na kila mwisho wa mwezi system inalinganisha mapato na matumizi na kama ukitumia zaidi ya asilimia Fulani ya kipato chako kinachotambulika unaitwa kujieleza umetoa wapi fedha hiyo unadhani mafisadi, walarusha wangetoka wapi?

Kama taasisi ya serikali ikilipa mshahara kwa mtu abaye amekufa au system inaona mtu huyo anapokea mshahara kutoka sehemu nyingine system inatoa alart kwa mwajiri na benki ili malipo yazuiwe mpaka mhusia akatoe maelezo sehemu husika je mishahara hewa ingetoka wapi?
 
Watanzania wenzangu, napenda kuwaasa kuacha majungu, mtima nyongo tumwache Rais wetu achape kazi, watu wameanza kuleta majungu kumvunja nguvu, eti utawala bora, km ni utawala bora nenda kwa mkeo nyumbani kwako ukabembeleze. Mitanzania ilishazoea mwendo wa kinyonga na kuiba, ikiambiwa kuongeza mwendo inasema inaonewa harafu inalia lia eti hakuna maendeleo miaka 54 ya uhuru. Fungeni makasha yenu mtumie kula na maongozi na wake zenu kwisha.
 
Wadau heshima kwenu!

Nimekuwa nikipita pita kwenye maeneo mbalimbali ya nchi na kusikia wananchi wakitaka kuongea/kuwasiliana na mkuu wa nchi ambaye ndio rais MHE.DKT.J.P.MAGUFULI,wananchi wana mengi ya kumwandikia mh.rais na binafsi naamini yeye ni mtu wa kazi na anaweza kusoma mwenyewe emails na kuzifanyia kazi au kuwasiliana na watoa taarifa kupitia emails hizo ili ayafahamu madudu mengi ya nchi hii.

Kimsingi mheshimiwa rais anaweza kazi mwenyewe akishirikiana na waziri mkuu.

Naomba kurugenzi ya mawasiliano ikulu,watupe emails za mheshimiwa rais na mheshimiwa waziri mkuu,tunataka kuwasiliana nao directly bila kupitia kwa mtu kati.

Asanteni.
 
Katika sehemu inayo ongoza kwa rushwa tbs imo, Tanzania inaongoza kwa vitu visivyo kuwa na ubora kutoka nje hasa China, pamoja na vyakula vilivyo pitwa na wakati.
 
Naunga hoja, kuna mambo mengi na mazito watayapata kupitia kwetu, na utekelezaji wao utakua rahisi sana, Bravoo
 
Tafadhali uliza uwanja wa taifa unaingiza kiasi gani. Uliza pia kwanini zile mashine za kisasa za kukatia tiketi hazifanyi kazi. Crdb wali invest kwa millions mfumo ukafa na watu wanapiga dili. Just ask them kwasababu huu ni mchezo kama wa bandari unakataa technology kwa sababu nyepesi nyepesi.
 
Hoja ni nzuri, lakini tahadhari inahitajika - majungu yaepukwe
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…