Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas jana ilitishia kusitisha uzalishaji wa umeme kutokana na deni la takribani shilingi bilioni 215 ikiwa ni malimbikizo ya malipo ambayo TANESCO walipaswa kuilipa kampuni tangu mwaka 2012.Hii ni kampuni moja na hatujui makampuni mengine yanaidai TANESCO kiasi gani cha fedha.
Mikataba mibovu baina ya TANESCO na makampuni haya ya kufua umeme bila shaka ndio chanzo kikubwa cha mzigo huu wa madeni kwa TANESCO.
Sasa kama serikali itahangaika na TRA na TPA katika kukusanya mapato wakati Taasisi nyingine ya umma ikiwa na mzigo huu wa madeni,kweli kutakuwa na tija ya ukusanyaji wa mapato?
Nani anaweza kututhibitishia hapa shirika hili linaloendeshwa kwa hasara linaweza kweli kulipa madeni haya makubwa bila msaada wa serikali?
Zoezi la kukusanya mapato litakuwa na tija tu iwapo Taasisi na mashirika ya umma kama TANESCO yataweza kujiendesha kibiashara.
Swali ni je,TANESCO itaweza kujiendesha kwa faida bila kwanza kufumua mikataba iliyoingia katika yake na makampuni ya kufua umeme?!
Kuna logic yoyote kuwawajibisha wafanyakazi wa TRA bila pia kuwawajibisha watumishi wa umma(wakiwemo wanasiasa) wanaotajwa kushiriki katika uingiaji wa mikataba hii?
Katika hili ni kama tu tumepoteza dira!