Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas jana ilitishia kusitisha uzalishaji wa umeme kutokana na deni la takribani shilingi bilioni 215 ikiwa ni malimbikizo ya malipo ambayo TANESCO walipaswa kuilipa kampuni tangu mwaka 2012.Hii ni kampuni moja na hatujui makampuni mengine yanaidai TANESCO kiasi gani cha fedha.

Mikataba mibovu baina ya TANESCO na makampuni haya ya kufua umeme bila shaka ndio chanzo kikubwa cha mzigo huu wa madeni kwa TANESCO.

Sasa kama serikali itahangaika na TRA na TPA katika kukusanya mapato wakati Taasisi nyingine ya umma ikiwa na mzigo huu wa madeni,kweli kutakuwa na tija ya ukusanyaji wa mapato?

Nani anaweza kututhibitishia hapa shirika hili linaloendeshwa kwa hasara linaweza kweli kulipa madeni haya makubwa bila msaada wa serikali?

Zoezi la kukusanya mapato litakuwa na tija tu iwapo Taasisi na mashirika ya umma kama TANESCO yataweza kujiendesha kibiashara.

Swali ni je,TANESCO itaweza kujiendesha kwa faida bila kwanza kufumua mikataba iliyoingia katika yake na makampuni ya kufua umeme?!

Kuna logic yoyote kuwawajibisha wafanyakazi wa TRA bila pia kuwawajibisha watumishi wa umma(wakiwemo wanasiasa) wanaotajwa kushiriki katika uingiaji wa mikataba hii?

Katika hili ni kama tu tumepoteza dira!
 
..kwa kweli umeniwahi kuandika haya.

..JPM anapaswa kutumbua majibu Tanesco.

..Tanzania ya viwanda haiwezekani kama tatizo la uhaba wa umeme halitapatiwa ufumbuzi.

..mimi naamini kwamba ukiritimba wa Tanesco lazima uendelezwe ile tuweze kuwa na influence na control zaidi ktk muelekeo wa uchumi Tanzania.

..nakubaliana na wewe 100% kwamba mikataba ya kifisadi iliyosainiwa baina ya Tanesco na makampuni ya kufua umeme imesababisha hasara kuliko faida. bila kuifumua mikataba hiyo basi "Tanzania ya viwanda" itabaki kuwa kauli mbiu za uchaguzi tu.

cc NasDaz, Mdondoaji, Kimweri
 
Last edited by a moderator:
Nadhani haya yote yapo kwenye pipeline. Kila kitu na mda wake, mheshimiwa raisi na wanaomshauri wameona ni vizuri kuanza na TRA, TPA...kuhakikisha kila kinachostahili kinakusanywa kama kodi, na kuweka misingi ya uongozi na uadilifu.
Tanesco kuna uozo mkubwa. Serikali itapita huko tu. One step at a time.
 
Inasikitisha Moderator hawajaona umuhimu wa huu zi kusimama peke yake.

Uhuru wa maoni hapa JF unaathiriwa sana na hii tabia ya kuunganisha thread.

Sometimes huwa inataka moyo kuanzisha mada hapa kwa hofu ya mada yako kugeuzwa comment na kuizika kabisa.

Mods hawajui uchungu wa mtu kukaa chini na kuandika maada alafu inageuzwa comment ts tena kwenye thread ambayo teyari ina pages nyingi kiasi cha kutia watu uvivu wa kusoma comments zilizopo.

Ni kweli kuna topic za kuunganisha ila hapa JF this is getting too much!Siuji wamezidiwa?!

Hata huyo Magufuli na wasaidizi wake sijui kama wataweza kusoma comments zote hizi katika huu uzi maana sasa zinatia hata uvivu.

Mods, kumbekeni kuwa "too much of everything is harmful."
 
Last edited by a moderator:
Wandugu,

Natumai mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku. Nimeanzisha thread hii ili iwe maalum kwa members wa JF kupost kero mbali mbali wanazokumbana nazo kwenye taasisi za umma.

Sababu za kuweka uzi huu maalum ni kwakuwa naamini JF inatembelewa na watu wengi ikiwemo viongozi wa serikali. Kwa hivyo itarahisisha upatikanaji wa habari kero na hivyo kusaidia viongozi wa eneo husika kurekebisha kwa haraka kabla mambo hayajaharibika.

Kero mbali mbali namaanisha issues kama vile kuombwa rushwa na watoa huduma, uchache wa watoa huduma, kukosekana kwa vitendea kazi sehemu husika, majibu ya hovyo, kucheleweshwa bila sababu n.k
 
Ni vyema mheshimiwa Rais akarudisha utaratibu wa kulala katika Ikulu ndogo zilizopo kwenye mikoa mbalimbali badala ya kutumia hoteli za kifahari ambazo baadhi hazilipi kodi.
 
Huu ni mwendo wa kupunguza matumizi yasiyolazimishwa!
 
Jamani hii foleni ya dah inakera kweli kweli aaahh!!!! Rais wetu plz plz plzzzzzz.........
 
Nazishauri mamlaka zinazoshughulikia hawa wahujumu uchumi waje mikoani naaeneo ya Borders waone mali za umma zinavyotafunwa! Hawa maafisa wa TRA huku mikoani wamegeuka miungu watu, Inabidi mamlaka nzima ya TRA ifumuliwe maana kila kona ya nchi ni uozo mtupu.
 
Mpwa hilo nizoezi linalofwata naomba ntarudi badae niko kwenye kikao kinamaji na karanga tu..
 
Ungejua ni fedha ngapi inapatikana bandari na laiti kama ungejua ni fedha ngapi inapotea bandari (serikali kukosa mapato yake) naamini ungesisitiza mkazo zaidi utiliwe bandarini kuliko sehemu nyingine yoyote ile.

Bandari ni moyo wa nchi. Mapato ya bandari yakidhibitiwa vizuri...basi Tanzania nzima itaendeshwa na bandari peke yake bila kugusa vitega uchumi vingine. Hivyo mtoa post naomba uache TRA iweke mambo sawa bandarini...huko kwingine tutakuja.
 

Niliambiwa kuwa wewe ni mjinga lakini leo nimethibitisha rasmi. Kutangaza kifo cha mheshimiwa humu kwenye ukumbi wakati hujui lolote. Alikwambia nani, ulithibitisha? Sasa uombe radhi humu au sheria ya mtandao inakufata. Kazi kwako. Ulitumwa au ulitaka sifa uonekane wewe ndio wa mwanzo kuleta habari humu jamvini. Pumbafu mkubwa!
 
Mkuu najua TRA Bandari ndiyo inayotakiwa kukusanya mapato mengi kuliko sehemu yeyote ile nchini,lakini hata mikoani nako TRA imeoza isiachwe kwa maana huko pia kuna mapato mengi sana.Fanya uchunguzi hasa maeneo ya Borders uone maafisa forodha wanavyotafuna pesa za umma.
 
Mheshimiwa Magufuli Rais wangu niliye na imani na wewe kulingana na kufanya kazi kujitofautisha na mkwere JK ambapo alikuwa akichekacheka huku taifa linatafunwa...Kwa muda wote huu pamoja na watu wengine naamini wanafanya upembuzi watu gani wanafaa na hawafai kwenye baraza lako lijalo....katika hili naomba ulitambue na wengine wajue pia hasa hsa suala la makontena bandarini na issue ya TRL na mabehewa makuukuu toka INDIA...Mh. Magufuli hawezi kushughulikia vidagaa kama kina Masamaki wakati wa kina Mwigulu Nchemba, Dr. Mwakyembe na wengineo kuwaruhusu watambe kwenye baraza lijalo hasa kwenye wizara walizokuwepo zikiwa zimefanya madudu...Tuanze na Dr Mwakyembe alihujumu sana kwenye mabehewa apate pesa za kampeni za kutosha ndicho kilichotokea huko wilayani Kyela mbeya mikopo ambayo wamama walipewa kwa riba ndogo kwa kianzio kidogo wakiwa kwenye vikundi wenyewe huita VICOBA ndio maana alipata kiburi sana na kujiapiza kwa wanakyela kwamba atakuwa waziri mkuu wa serikali ya MAGUFULI kilichotokea ni contrary kabisa....nijikite kwenye hoja ya ufisadi wake dr. mwakyembe hana usafi kwa jinsi magufuli alivyoanza maana ana kashfa za huko bandarini kipindi akiwa huko wizarani, kingine akiwa uchukuzi alishiriki ununuzi mabehewa chakavu ambayo kila mtu anajua...HIVYO HAFAI Hta kupata wizara (ikumbukwe sina chuki naye ila uhujumu uchumi na wizi ndicho ninachokichukia)

MWIGULU NCHEMBA hakuna kilichofanyika TRA hakjui huyu alikuwa naibu waziri anajua kila kitu Magufuli aanze na hawa mafirauni wanaoitafuna nchi yao bila kujali chama chao hicho ambacho magufuli hafuati mambo ya kijinga ya CCM na nimeona wanamchukia sana sana kama January makamba n.k hawa hawafai kurudi tena kwenye wizara MAPAPA YAPO MAGUFULI YACHOME HAYOOO HAPO NI KAZI TUUUU
 
Nilipoandika kwamba Magufuli anahangaika na vidagaa huku manyangumi yanalala fofo, watu walidhani ni masihara. Mimi kwa kweli magufuli asipowashughulikia hawa ma vampires sita muelewa, mi sio kichwa cha mwendawazimu bwana.. Hawa watu wanalindana huku wakicheza na akili za watanzania wanaowaita wavivu wa kufikiri! I real hate politicians's dramas.
 
Acha matusi wewe, hebu jiheshimu
 
Tunduma Rushwa imekithiri sana,wafanyabiashara wa South Africa wanaikimbia kwa kubambikia kodi kubwa ili mtu afanye plan B ambayo ni kutoa Rushwa..ukikubali kulipa kodi bila rushwa utachukiwa sana..
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…