ni ukweli usiofichika, kilio cha wananchi siku zote kimekuwa ufisadi ufisadi ufisadi pamoja na ujenzi wa uchumi ulio imara kwa sababu mali asili zimejaa lukuki. kuna shida moja kwamba kama Magufuli ataendelea hivi kwa speed hiii bila hata kununuliwa , basi wananchi kwa kauli moja tuamue tumpe muda wa zaida kwa kubadilisha katiba ili imruhusu awe rais hata kwa miaka 20. Mungu ampe afya njema. nina uhakika kama akiendelea hivi kwa miaka 20 nchi hii itakuwa imepaa kuwa na uchumi wa juu kabisa na sio wa kati tena.
lakini mambo ya demokrasia demokrasia ndio yanaturudisha nyuma , eti baada ya miaka 10 , basi tena. sasa akija rais bomu si ataturudisha nyuma miaka 10 tuanze upya tena. wananchi tuwe macho.
hii tabia ya upinzani eti kujifanya kungangania kutaka kwenda ikulu ni ya kutulotezea muda kama tunapata watu kama Magufi. imagine leo Lowasa ndie angekuwa rais. haya wengi wa wafanya biashara waliokwepa kodi ni marafiki zake. na wamemchangia kwenye kampeni za urais. angewezaje kuwakamata na kuwaambia walipe kodi ?????? sana sana angewaambia basi wajitahidi wasikwepe tena. lakini wangetafuta tuu mbinu nyingine za maufisadi hiyo ip kwenye damu jamani za hawa watu. wafanya biadhara always hawaridhikagi na mapato na wana hulka ya kutaka kukwepa kodi kwa namna yoyote na ku maximize faida ili wazidi kupanuka.
pia tumejifunza kuwa kumpeleka rais ikulu ambaye ni mfanya biashara au ana chain ya wafanya biashara mzigo mkubwa sana kwa nchi. wanaweza yumbisha nchi kwa kuamua watakavyo wao. wananchi maskini hawawezi pata fursa wala haki yoyote. haya angalia mfano mzuri ule ufukwe wa Coco beach. Manji ndio alishaubeba hivyo huku akinyima fursa na haki za watu wa manzese na tandale kwenda ufukweni walau nao wafurahie maisha yao kama binadamu wengine. lakini mifanya biashara mikubwa haijali hayo ni wabinafsi hawajali binadamu wenzao. Magufuli hapa kaonyesha ujamaa uliotukuka. angekuwa Lowasa walahi angesema mwacheni Manji maadam kashinfa kesi basi apaendeleze pale ili alipe kodi forodhani. pasikae burebure. asingewajali masikini. kwani ni lini alionyesha kuwajali .asikini. kwake Monduli kuna masikini wa kutupwa hawana hata maji mpaka leo hii pamoja na mipesa lukuki aliyonayo. sasa angewezaje kuendeleza taifa kwa mtaji huu. au ulikuwa utapeli wa kisiasa.
anyway nilikuwa najaribu kulinganisha na kupambanua aina ya watu ambao wanaweza kiukweli kupaisha nchi hii kimaendeleo kwa haraka. tusiende na upepo wa kuhongwa na kudhani eti fulani atafaa kuongoza nchi. ni hatari ukishauza utu wako basi ndio umekwisha hivyo. ni sawasawa bwana mwenyekiti wa chadema aalivyohusishwa na kashfa ya kuuza utu kwa kutoa nafasi ya ugombeaji urais kwa Lowasa bila kufuata utaratibu uliokuwa umepangwa awali. na hapo ndipo anguko kuu la chadema na ukawa lilipoanzia. hakuna mchawi mwingine. kwa nini utaratibu uliowekwa na viongozi wa vyama ulipindishwa kiujanjaujanja tuu mpaka kufanya makamanda Slaa na Lipumba kutimka. haikuwa haki lakini maadam uhuru uliuzwa kwa tamaa ya pesa basi matokeo ndio haya sasa. sasa kama ukawa tuliweza kupindisha mfumo mzuri uliowekwa kabla ya kuingia kwa kundi la mafisadi kutoka ccm, tulikuwa na uthubutu gani wa kusema mfumo wa ccm ndio mbaya ??? . ukawa ungewezaje sasa kujenga mfumo uliosimama kama wangechukua madaraka.??? wanasiasa mmetudanganya sana na safari hii ndio tumewafahamu vizuri sana.
mfano wanasiasa wa ukawa wamekuwa wakituaminisha kwa miaka 8 kuwa Lowasa na sumaye ni mafisadi kwa kupitia njia mbalimbali kama magazeti ya Mwanahalisi ya Kubenea, MP Ubungo na mikutano ya hadhara mingiiiii. lakini baada ya kununuliwa na kuuza utu wao waligeuza misemo yao na kusema wamewasafisha, kwa hiyo ajenda ya ufisadi ikawa imefia hapo. na Magufuli kwa sababu ni msafi akaibeba na sasa ajenda hiyo anaendelea kupambana nao mafisadi mpaka kieleweke.
Salam hizi kwa wanasiasa wetu. enzi za kufanyia siasa usanii zimeisha. tunataka tupaishe uchumi wetu sasa.
hongera Magufuli Mungu aendelee kukulinda