Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Na mimi nimshauri, mheshimiwa rais tumekuwa na chip politics kwa miongo mingi. Na yeye ameanza nayo kwa kuchukulia udhaifu wa aliyekutangulia. Mimi naamini sheria na utaratibu tuwekee sheria mama vizuri iliwatakaofuata nyuma yako wasipindishe ama kuzembea kwa kukosa mwelekezo wa kisheria. La pili tupe mwongozo wa nini tuamini wanini tufanye kama taifa. Uongozi ni kujua njia tupe lengo la taifa hili ujamaa na kujitegemea umekufa mmeuua, tutafutie mwelekeo mwingine na utufunze kutii sheria. Tuanze kuwa na mwelekeo ktk njia ya utii na uadirifu
 
Mh.Rais Aboreshe maslahi ya watumishi wa umma ngazi za chini kuleta morali kazini haswa vijijini. Watumish vijijini waboreshwe katika elimu na mafunzo mbalimbali kufikia malengo na kwenda na kasi ya Hapa kazi tu.
 
Kaka Magu kama kuna eneo limeliwa na ushahidi mgumu kupatikana ni kwa wauza mafuta,hamishia nguvu hapo na komaa kila depot wakupe hesabu zao utagundua TRA hatakiwi kubaki MTU,hao wamekula sana kodi zetu na bado mafuta bei juu hata yakipungua huko duniani,ewura pia piga chini wote anza upya

kuna siku nilishawahi kuandika thread humu kama swali, kuhusiana na utitiri wa vituo vya mafuta nje kidogo ya mji wa dar sikupata ushirikiano, haikua bahati mbaya ilikua na sababu yake. yapo yanayoendelea nyuma ya pazia.
 
Ni muda sasa nchi bado inaongozwa na KATIBA isiyokidhi viwango. Kwa kuwa JPM anaonekana kuthubutu kutenda kazi km rais wa nchi na kujitenga na itikadi ya kichama, sasa ni muda atengeneze katiba yenye viwango. Hii shida ya fukuzana itakoma km katiba ni nzur
 
Hatuhitaji katiba. Iliyopo ina kidhi. Tunachohitaji sasa ni kukuza uchumi. Hapa kazi tu. Hakuna siasa
 
Hatuhitaji katiba. Iliyopo ina kidhi. Tunachohitaji sasa ni kukuza uchumi. Hapa kazi tu. Hakuna siasa

Hamhitaji na nani toa maoni yako sio kutusemea, au ndo unawasemea ccm wenzako. Kumbuka Tanzania ni ya Watanzania wote usikulupuke kujibu hoja za msingi unajidhihirisha au ndo nyie majipu mlio baki kutumbuliwa
 
Ni muda sasa nchi bado inaongozwa na KATIBA isiyokidhi viwango. Kwa kuwa JPM anaonekana kuthubutu kutenda kazi km rais wa nchi na kujitenga na itikadi ya kichama, sasa ni muda atengeneze katiba yenye viwango. Hii shida ya fukuzana itakoma km katiba ni nzur

Kazi ya Raisi si kutengeneza katiba ni kusimamia katiba iliyotengenezwa.Katiba hutengenezwa na wananchi na bunge.Rasimu ya katiba ilishapitishwa na bunge la katiba inasubiri kupelekwa bungeni ijadiliwe na kisha ipelekwe kupigiwa kura na wananchi.

Raisi hata siku moja hatengenezi katiba ya nchi!!!! USHAURI UNAOMPA MAGUFULI MBOVU inaelekea hujui hata mchakato wa katiba hufanyikaje
 
mtihani wa kwanza utakaomshinda Mwalimu John Joseph Magufuli utakuwa ni katiba Mpya
 
Ni muda sasa nchi bado inaongozwa na KATIBA isiyokidhi viwango. Kwa kuwa JPM anaonekana kuthubutu kutenda kazi km rais wa nchi na kujitenga na itikadi ya kichama, sasa ni muda atengeneze katiba yenye viwango. Hii shida ya fukuzana itakoma km katiba ni nzur

Wewe endelea kusubiri hiyo katiba mpya. Kwani south Afrika hawana katiba nzuri sana? umeyaona maisha ya walalahoi na wafanyakazi migodini yalivyo? hiyo katiba nzuri kwao ukiwauliza ina maana gani? angalia ni nani anamiliki uchumi wakati ni kati ya nchi zenye katiba nzuri, hayo mambo ya katiba achana NATO. Mbona Nyerere aliiongoza nchi vizuri akitumia katiba hii hii tena wakati huo haijawa na mambo ya haki za binadamu, sasa iweje sahivi ndo iwe mbovu haifai?
 
Katiba bora itakayozingatia maoni ya wananchi yaliyoratibiwa na jaji Warioba ndio itakayotunbua jipu la CCM.
 
Magufuli be your own man and master -
Personality yako
unataka kiswahili halafu unachapia TUKUELEWEJE?
 
Leo nimepata taarifa kuwa eneo ilipokuwa kambi ya vijana Igumbilo MKoani Iringa Vigogo wa UVCCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wao taifa, wamegawana viwanja na vingine kuviuza. HIstoria ya eneo hilo inaonesha ilikuwa ni sehemu ya Mashamba makubwa ya Tumbaku ambayo yalitaifishwa na serikali toka wa Wagiriki.

Tukio hilo likanifikirisha juu ya "uhalali" wa hao viongozi wa UVCCM kugawana hivyo viwanja vya Igumbilo. Ikumbukwe kuwa kabla ya mwaka 1965 kulikuwa na vyama vingi vya siasa mpaka pale TANU ilipotumia madaraka ya kidola kuviua. Kwa maana nyingine TANU na ASP vilipoungana mwaka 1977 vilikuwa tayari ni vyama dola. Kwa maana hiyo viwanja hivyo vya Igumbilo asili yake ni Umma na wala si CCM

Baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, CCM kikiwa ndicho chama pekee cha siasa nchi, kilijichagulia jinsi kitakavyobakia ndani ya mfumo wa vyama vingi. Njia mojawapo ikaona ili kiwe salama ni kujimilikisha mali zote za umma zenye muelekeo wa kisiasa na kuzigeuza mali zake.

Lakini ni baada ya mwaka 1995 kwenye uchaguzi Mkuu ulioshirikisha vyama vingi vya siasa ulipofanyika, ndipo CCM ilipotanabahi kuwa ili iendelee kuwa madarakani ni lazima ipanue wigo wake wa kumiliki mali zilizokuwa za Umma ndani ya mfumo wa chama kimoja. Hapo sasa CCM ikapora haki ya umma ya kuvimiliki viwanja vyote vikubwa vya mpira na kuvifanya kuwa vyake. Nakumbuka Miaka michache iliyopita Amos Makala akiwa ni Mchumi wa CCM taifa aliwakumbusha wana CCM wenzake kuvitafutia viwanja hivyo hati za umiliki kwani CCCM haiwezi kukaa madarakani milele.

Kwa maneno ya Makala inaonesha kwamba CCM haikuwa inavimiliki viwanja hivyo kihalali, bali ilitumia mamlaka ya kidola kuvitangaza kuwa vyake bila hata aibu. Ukichanganya na eneo la SUKITA pale jangwani CCM imepora mali nyingi za umma bila haya wala huruma. Kama kweli Ndugu Rais, John Pombe Magufuli ni jasiri na anataka kupambana na uhalifu na uovu uliojaa katika jamii yetu, basi arudishe mali nyingi za umma zilizoporwa na CCM!
 
Shetani naye alikuwa na maswali ya dizaini hii, umenikumbusha ile muvi ya maisha ya Yesu

BTW be specific, arudishe viwanja vilivyoporwa na viongozi au vilivyoporwa na ccm?

La viongozi linaweza kutekelezwa haraka bila shida na halihusiani na chama, wamefanya hayo kwa matakwa yao si ya chama, kwa vikao vyao na familia zao au nafsi zao si vikao vya chama.

Issue ya chama ni habari tofauti sana na ni habari tete pia si kipaumbele cha wananchi kwa sasa,

Ndo maana nimeanza kwa kusema unanikumbusha majaribu ya shetani kwa Yesu
 
Hakuna asiyeshangilia anachofanya Magufuli sasa hivi, hakika ameonesha madudu mengi sana yalifanyika kipindi cha utawa uliopita.
Ninaamini pale bandarini na tra kuna watu wa usalama wa taifa, na waliona makontena yakipotea bila kusema neno, au walisema kwa wakubwa wao kuhusu makontena hayo, sasa kwa nini hii idara isisafishwe na Magufuli ili kuwaondoa watu hao, hawakutekeleza wajibu wao ipasavyo, kodi nyingi ilipotea.
Wapo wanaoishi kama vigogo wa TRA wana utajiri uliopitiliza. Washughulikiwe haraka.
 
Mkuu muleta mada. Nchi hii kuna majipu ya kumwagaaaaa ya kila aina. MAGU anaangalia Yale very serious ndo anaanza hayo. Akitumbua yale very serious, yasiyo serous yatajitumbua yenyewe automatically!
 
Ni vigumu kurejesha chochote ndani ya ccm,kwanza magufuli si mwenyekiti wa chama,pili juzi juzi tu wamegawana mabilioni yaliyosalia baada ya kampeni hajathubutu kuwauliza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom