Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Napenda kumshukuru Mungu kwa kutupatia Rais mwenye kuthubutu kuchukua maamuzi magumu yenye maslahi kwa Watanzania. Hasa hili la TRA na Bandari. Tunamwomba Mungu awalinde katika kila hatua umnayokanyaga wewe na waziri mkuu Majaliwa.
Mheshimiwa Rais Magufuli unastahili pongezi sana lakini kuna mambo bado magumu yenye makandokando mengi sana na yenye kuuzi kama sio kukera tena sana. Hili si geni bali yaliyotendeka katika wizara ya madini na maliasili huko ni shida tupu kama ya makontena na TRA. Huko kumejaa wezi na wahujumu uchumi wetu. Mungu akujalie afya hekima na busara uwapitia hao pia ili kunusuru taifa letu. Namuomba Mungu akulinde ulivyoanza umeonyesha unatosha. Watanzania wazalendo tupo nawe katika jahazi la ukombozi mpya wa Tanzania mpya. Mungu ibariki Tanzania Magufuli na Majaliwa.
 
Ndiyo atakuwa amerogwa, siyo bure haiwezekani mtu mwenye akili timamu afanye mambo kama anayoyafanya. Aliposema pesa za kutupongeza sisi wabunge zitumike kununulia vitanda nlishtuka kidogo ila nikasema mzee ulimi uliteleza. Nikanyamaza na nikahisi kuwa inawezekana kabla ya kuja kwenye kile kijikao alikuwa amekunywa au amevuta kitu maana katika hali ya kawaida mtu asingeamua maamuzi kama yale.

Imagine tumefanya kampeni miezi hiyo, kwa shida ,mateso n.k tumekoswa koswa kuuawa na kuua pia, leo mashirika haya kwa kutambua mchango wetu wametuchangia ili watupongeze kwa kazi kubwa tuliyofanya ya kuomba kuLA kwa wananchi na hatimaye wananchi hawa wametupatia kuLA na nyingine tumejichukulia wenyewe leo tunatakiwa kujipongeza kwa sisi tuliofanikiwa kurudi tena Bungeni anasema eti zikanunue vitanda muhimbili. Kweli? Hii ni akili sawa sawa? Muhimbili wagonjwa wapo miaka na miaka lakini sherehe yetu sisi ni mara moja kwa miaka mitano what was wrong with that? Huyu mzee anatumia kinywaji gani?

Miaka 10 wagonjwa wanalala chini muhimbili hakuna aliyelalamika. Ina maana yeye ndo amewaona sana kuliko sisi wabunge na raHis wetu aliyepita? Huu ni unafiki. Hawa wagonjwa hawaendi kustarehe kule mpaka kila mtu alale kitanda chake.kwani kule lodge? Tena amesababisha kwa hivi sasa wagonjwa wengi hata wakiambiwa wamepona hawataki kuondoka kurudi kwao kwa kuwa kule wakirudi wataenda tena kulala kwenye mikeka. Tumeanza kupata shida mtu hata akiumwa kichwa anakuja kuhimbili anasema sasa kuna huduma nzuri anataka alazwe hata week mbili.
Tena amesababisha hata manesi na madaktari wawe wazembe maana vitanda vingi mpaka vinabaki halafu manesi na madaktari wanalala. Na wengine wamepeleka vingine ofisin mwao.

Haya hilo likapita, leo siamini eti siku ya uhuru nipo home na wife ananambia siku ya usafi. Hajui usafi ushaanza kufanywa na Mh Magufuli huko Bandarini na TRA. Wife naye anashadadia tu leo siku ya usafi mimi roho yangu haijatulia hata nikiwaza usafi huu kwa Mh Magufuli asije akasafisha na kwenye hizi Kamati zetu za Bunge. Maana huku nako si haba kuna kauchafu kake. Wananchi hawashangai kuwa kwa nini tunagombea sana ubunge kwa hali na mali, kwa machozi ,jasho na damu..hata tukiambiwa tupeleke viu
 
Mifuko Ya Hifadhi Ya Jamii ni shida kuna LONGOLONGO sana kule. Asinganganie TRA na Bandari tu azungukie na Huku piaLAPF, PSPF ni shidaaaaa
 
Tehh!Tehh! Bado sana kutoka Mirembe. Ngoja niwaambie wakuongezee dozi
 
Safi sana ila ni wachache watakuelewa. Tatizo umetumia uandishi wa kumchosha msomaji.
 
Lazima wawepo wapinzani kwa kila jambo hata kama ni zuri. Maoni sahihi hapa ni, "TUMPE MUDA". Lkn kama mwendo wa magu utaendelea kuwa huu.... basi ni bora aongezewe muda. Kwani kwa muda mrefu tz kulikuwa na fumbo ambalo lililotolewa majibu mepesi kuwa hakuna ubaguzi wala upendeleo ktk kupeana vyeo vya wafanya maamuzi... na ajira serikalini kwa ujumla bali tulitetea kuwa vyeo hivyo hupewa si kytokana na kabila yake au dini yake wala ukanda bali hutegemea weledi wake.

Lkn mh Magu katufumbulia fumbo hilo kuwa hakukuwa naweledi wwt ktk kupeana vyeo hivyo zaidi ya ushkaji.

Kwa muono wangu kama ni weledi Mh mwenyewe ndio anaetuonyesha.

Tufike wakati tusimamie na kutekeleza yale tunayoyasema kwa kuwa tunayaamini. basi tuseme tu magufuli tulikuwa tunamsubiri miaka 20 iliyopita na hakutokea..... na leo katuonyesha kuwa udhaifu.wake ni mdogo kuliko weledi wake na hivyo "TUMPE MUDA" tujikinaishe thn kama ataweza kuibadili TZ kama alivyoweza kuibadili kagame rwanda. Basi Mh magu anastahili aongrweze muda wa kuwa madarakani.

Poleni wale wenye siasa kali wanaomini hadi leo kuwa LUWASSA Ndie RAIS, na wale wanaoamini kuwa nafasi kama ya urais si zaidi ya mihula miwili. Tulikariri huko nyuma kuwa TZ inahitaji Rais jasiri na mwenye maamuzi magumu. Kama mifumo haijasaidia basi tatizo ni mtu na sio mfumo.

Hivyo kama tunamchagua mtu kwa WELEDI #magufuliaongezewemihula
 
Ndiyo atakuwa amerogwa, siyo bure haiwezekani mtu mwenye akili timamu afanye mambo kama anayoyafanya. Aliposema pesa za kutupongeza sisi wabunge zitumike kununulia vitanda nlishtuka kidogo ila nikasema mzee ulimi uliteleza. Nikanyamaza na nikahisi kuwa inawezekana kabla ya kuja kwenye kile kijikao alikuwa amekunywa au amevuta kitu maana katika hali ya kawaida mtu asingeamua maamuzi kama yale.
Imagine tumefanya kampeni miezi hiyo, kwa shida ,mateso n.k tumekoswa koswa kuuawa na kuua pia, leo mashirika haya kwa kutambua mchango wetu wametuchangia ili watupongeze kwa kazi kubwa tuliyofanya ya kuomba kuLA kwa wananchi na hatimaye wananchi hawa wametupatia kuLA na nyingine tumejichukulia wenyewe leo tunatakiwa kujipongeza kwa sisi tuliofanikiwa kurudi tena Bungeni anasema eti zikanunue vitanda muhimbili. Kweli? Hii ni akili sawa sawa? Muhimbili wagonjwa wapo miaka na miaka lakini sherehe yetu sisi ni mara moja kwa miaka mitano what was wrong with that? Huyu mzee anatumia kinywaji gani?
Miaka 10 wagonjwa wanalala chini muhimbili hakuna aliyelalamika. Ina maana yeye ndo amewaona sana kuliko sisi wabunge na raHis wetu aliyepita? Huu ni unafiki. Hawa wagonjwa hawaendi kustarehe kule mpaka kila mtu alale kitanda chake.kwani kule lodge? Tena amesababisha kwa hivi sasa wagonjwa wengi hata wakiambiwa wamepona hawataki kuondoka kurudi kwao kwa kuwa kule wakirudi wataenda tena kulala kwenye mikeka. Tumeanza kupata shida mtu hata akiumwa kichwa anakuja kuhimbili anasema sasa kuna huduma nzuri anataka alazwe hata week mbili.
Tena amesababisha hata manesi na madaktari wawe wazembe maana vitanda vingi mpaka vinabaki halafu manesi na madaktari wanalala. Na wengine wamepeleka vingine ofisin mwao.
Haya hilo likapita, leo siamini eti siku ya uhuru nipo home na wife ananambia siku ya usafi. Hajui usafi ushaanza kufanywa na Mh Magufuli huko Bandarini na TRA. Wife naye anashadadia tu leo siku ya usafi mimi roho yangu haijatulia hata nikiwaza usafi huu kwa Mh Magufuli asije akasafisha na kwenye hizi Kamati zetu za Bunge. Maana huku nako si haba kuna kauchafu kake. Wananchi hawashangai kuwa kwa nini tunagombea sana ubunge kwa hali na mali, kwa machozi ,jasho na damu..hata tukiambiwa tupeleke viungo tunapeleka. Sisi wabunge jaman tunawatumikia ninyi wananchi hivyo hamna budi kutupa kula. Tunajitolea kusikiliza matatizo yenu na kuyafanya kama yetu, mnapotuona tunalala bungeni ni kwakuwa usiku kucha tunakuwa tumekesha tukiwaza na pengine kujadaliana na mwananchi mmoja aliyechaguliwa kuja kuleta matatizo yenu kwangu mimi mbunge. mara nying akina mama wanakuwa na matatizo mengi hivyo naweza chagua sample moja ije inambie matatizo ya akina mama jimboni kwangu.
Kesho nikiamka nimechoka na nikienda bungeni wakati mwingine nalala kwa sababu ya uchovu. Wananchi wengine kwa ulofa na upumbavu wanasema sisi hatufanyi kitu. Wana uhakika? Tunafanya kitu na vitu vingi sana. Msidhani kupitisha kila bajeti ni jambo rahisi. Ukiangalia jambo hili naweka angalizo maana hatujui Mh Rais atakunywa pombe gani tena ikamtuma apunguze au afute posho hizi kidogo tunazopata. We piga hesabu Dodoma chumba cha kawaida kabisa ni tsh 120,000 hapo hujala hujanywa,hujaweka bajeti ya kuwapa omba omba huko njiani, pia hujawasaidia watu mbalimbali. Posho tunayopewa ni ndogo angalau mwaka huu ipande iwe hata 500,000 kwa siku.
Nisisahau leo eti siku ya Uhuru? Nipo home just imagine?hivi huyu Mh anajua uchungu wa wazee wetu kupata Uhuru? Leo tulipaswa kupongezana kwa kupata uhuru na kuangalia gwaride, kuangalia jamaa wakivunja matofali kwa vichwa na wakirusha mateke kuonesha uimara wa jeshi letu. Leo ilitakiwa jioni twende Serena Hotel na Pia ikulu kumpongeza kwa yeye kushiriki nasi siku ya uhuru. Anasema ameokoa billion 4 zikajenge barabara., Huyu mzee karogwa siyo bure. Barabara kitu gani? Nani aliwah shindwa kwenda mjini kwa sababu hakuna barabara? Barabara zipo za kutosha tu na kama mtu anasema foleni kwa nini asiondoke kwake saa nane usiku kwenda kazini barabara inakuwa nyeupeee haina hata folen.
Huyu Mh anadhani yeye ana uchungu sana kuliko waliopita? Wao wamekuwa na haya mambo kwa miaka 10 wamevumilia tu yeye anakosa uvumilivu ndani ya mwezi mmoja? Kama rahis kikwete amekaa madarakani miaka 10 amevumilia kuona wananchi wanalala chini yeye ameshindwa kuvumilia mwezi mmoja tu? Anaonekana ni Rais asiye na uvumilivu. Wenzake wamevumilia mambo mengi sana na pia wamekuwa na roho za kusamehe watu kulipa kodi. Yeye anakuja na sijui roho gani analazimisha watu walipe kodi. Walipe hawa wananchi wadogo wadogo tu mbona inatosha, kwa nini kuwasumbua wawekezaji wa ndani na wa nje? Je wakisusa kuwekeza? Mbona miaka yote hawajalipa na pesa ilikuwa inapatikana nying hata rahisi aliyepita alikuwa ana uwezo wa kusafiri na mamia ya watu bila shida mchana na usiku? Yeye ana nini kinachomfanya asitake kwenda nje ya nchi? Mpaka sasa alipaswa aende nchi nyingi akajitambulishe kuwa yeye ndo rais wa Tanzania..naona ameganda tu humu nchini.
Tunataka maisha yetu yarudi pale pale. Na huyu aliye mroga Mh atafutwe kabla hajafa.maana akifa ikafika miaka mitano hivi hivi atasababisha ndoa zetu za kando zivunje na hivyo kusababisha akina mama wengi kukosa waume n.k
SIAMINI LEO ni siku ya UHURU hata kidogo. Wenyewe tulipanga bajeti kuwa tungeadhinisha sherehe hii kwa kumsifu na kumpongeza sana. Ila si mbaya ingawa leo nitashinda home lakini nakumbuka bajeti tuliyopiga Ijumaa ya vifaa vya usafi kwa siku ya leo. Mfagio mmoja ni tsh 10,000 ile original siyo ya kichina na inatakiwa iwe 100. Ili ofisini kila mfanyakazi ashike miwili miwili wakati wa usafi. Ndoo za maji tsh 25,000 moja, nazo tutanunua orijina siyo used au za kichina. zinatakiwa hata 50 si mbaya sana. Matambala ya kupigia deki yale mazuri kabisa ni tsh 15,000 moja nayo yawe 50. Gum boot pair 50 nliambiwa zile orijino ni tsh 50,000 moja. Ya kuzolea taka yawe 25 na kila moja ni tsh 10,000. Dawa za kuoshea vyoo chupa za lita moja kwa bei ya manunuzi zile orijina chupa moja ni tsh 15,000. Gloves pair 100 kila moja tsh 10,000. Mask 50. Kila moja ths 20,000. Hiyo ndo bajeti ndogo tuliyopiga tukasema tuletewe hizo pesa nasubiria alhamisi niende kusikia kama pesa hiyo ililetwa na ikatumika ipasavyo ili angalau nasi tusikose kabisa kubakiza chenji.
Hamna shida sisi TUTAPIGA kazi tu ila nasisitiza kwa hali hii Mh anatukatisha Tamaa tuliyo nayo ya kujiletea maendeleo. Najiuliza ni nani Kamroga huyu Mheshimiwa? Maana ni kweli amerogwa mambo anayoyafanya si ya mtu ?mwenye akili timamu? anawafikiria sana wananchi kuliko sisi tunaopatiwa Kula na wananchi hawa tena katka mazingira yao magumu sana na bado wameweza kutuchagua mwaka huu tena ili tuanze kutimiza ahadi za mwaka 2010. Tumehangaika kurudisha imani yao kwetu baada ya kuwa walianza kupoteza baada ile miaka 5 ya mwanzo kuisha. Tumewashawishi kwa khanga.tshirt na kofia wametuelewa sasa anapaswa raisi naye atuelewe aache mambo ya kale na kutupunguzia kasi,ari na nguvu zaidi tulivyokuwa navyo. Kazi tu, KAZI MY FOOT. Anyway nasi tutapiga kazi tu hamna shida. Ila tusiingiliane

Wewe ulifaulu kiwango kizuri kwenye somo la fasihi. Hongera but siamini kama wengi watakuelewa
 
Oooh!umeona eeeh jinsi gani watu walivyokuwa wanakula kiulaini kama kumsukuma mlevi. Wenye ufahamu wamekuelewa ulikuwa unamaanisha nini. Huyu siyo chizi maarifa Bali anaona mbali.
 
Sasa vilaza wote wamekasirika kwa kuona mtu anafanya kazi, walizoea kuchekewa na kulalamika kutaka posho za kuonga vimada na kutoroka bungeni.
 
Umejitahid sana katika kuwasilisha ujumbe wako japo umetumia fasihi ya hali ya juu sana watu wanashindwa kukuelewa, hongera
 
kumbuka kuna sheria ya mtandao, huwez kumwambia rais wetu mpendwa karogwa, kuwa makin xn umu jukwaan, sifa za kijinga zitakuponza wenzio saa hz wako ndan wananyea debe,na ww pia co mbunge nakujua vzr xn sema umeamua kujifanya chiz kama id yako inavyoonyesha apo, hakuna mbunge mngese kama ww kwenye serikal hii ya awamu ya 5! take care xn kijana ili ndugu zako wasije wakakulilia baadae, uyu co rais wa kumbeza! mbwa we!!
 
u ar so inteligent!
only the briliant and the bright can manage to see at that angle.
 
Naunga mkono hoja ndugu haki kwanza, cku zote nyote njema huonekana asubuh, uko kote rais atapita tu, cha msingi ni kuomba mungu amalize majukum ya tra na bandar salama
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom