Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kama kuna ufisadi upo kwa wakuu wa shule za serikali, wamehodhi shule na kuwa mali zao binafsi, elimu imekufa wanaendekeza majungu makazini ADA imekuwa vitega uchumi vyao hali ni mbaya wamekuwa malord father hawaambiliki, serikali tupia jicho hawa jamaa wanabagua walimu mashuleni. Kuna makundi ya team mkuu hao ni watu WA NDIO MKUU ILI WAPATE NIGHT PIA LIPO KUNDI LA ISOLATED YAANI HAWAKO GROUP LA MKUU. TAFADHALI WAMULIKE NI KIKWAZO KINGINE CHA ELIMU BORA TANZANIA.
 
Aaanze na halmashauri ya ngorongoro

kweli mkuu..huko Mara nasikia ndio kumeoza...nasikia kuna mkuu wa hr pale bunda yeye anapiga madili ya kujihamisha...mara mbeya,nzega afu anarudi tena bunda...tena anahama tena...nimetuma vijana wangu kuchunguza...nimetoka kulipua wa halmashauri ya hai majuzi
 
[h=1]Wadau;

BAADHI ya kampuni za uuzaji mafuta zinatuhumiwa kujihusisha na wizi mkubwa wa shehena yenye thamani ya sh. bilioni 18 ya mafuta yanayoagizwa nchini, imefahamika.
[/h]Uchunguzi umebaini njia kuu mbili zinazotumika kuiba mafuta na kusabababisha hasara kubwa kwa Taifa.

NJIA YA KWANZA

Ni mfumo wa mabomba ya mafuta uliounganishwa na vituo vingi vya kuhifadhi na kusambaza mafuta yaani DEPOTS ambavyo havidhibitiwi na kukosekana kwa miundombinu imara ambayo inaruhusu kuvuja kwa mafuta na wizi mkubwa bila wasimamizi kujua yaani surveyers. Mifumo hii ya mafuta haijawahi kugaliwa kwa miaka mingi na wakala wa vipimo WMA HIVYKUIKOSESHA SERIKALI MAPATO MAKUBWA. Matanki haya ya mafuta hayajafanyiwa CALIBRATION kwa muda mrefu sasa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya wataalamu, baadhi ya kampuni hizo (majina tunayo) zimekutwa zimeunganisha kiholela mabomba kwa ajili ya kupeleka mafuta kwenye matanki ya kuhifadhia, hivyo kutoa mwanya kwa mafuta hayo kuhujumiwa.

NJIA YA PILI

Matenki mengine yamewekewa valvu ambazo sio sahii na nyingine zimewekewa valvu ambazo ni rahisi kufanya hujuma,? ilieleza sehemu ya ripoti hiyo. Ripoti imebaini zaidi kuwa valvu nyingi zilizofungwa kwenda na kutoka kwenye matanki ya kuhifadhi mafuta sio imara na zimelegezwa kwa makusudi kiasi cha kuruhusu nishati hiyo kuchanganyika na maji na kuwa hilo ni moja ya eneo kunakoibiwa mafuta kwa wingi.

Tunaomba makapuni yafuatayo yachunguzwe kwa ukaribu na ikidhibitika basi hatua stahiki zichukuliwe haraka iwezekanavyo;

1. Lake Oil - Hii ni kampuni ya kitanzania, wana DEPOT yao huko Kigamboni.

2. MOIL - Hii kampuni inamilikiwa na Mbunge Mmoja wa CCM huko Mwanza. Wana Depot yao Huko Kigamboni

3. Hass Petroleum - Hii ni kampuni inayomilikiwa na wakenya wenye asili ya kisomali. Wana Depot yao Huko Kigamboni.

4. World Oil - Hii ni kampuni inayomilikiwa na shemeji yako Raisi wa Congo Joseph Kabila. Wana Depot yako Huko Kigamboni

Tunaomba USALAMA WA TAIFA wasaidie kumulika WAHUJUMU UCHUMI hao ili sheria ifuate mkondo wake.

WISOBLOWA
 
Kama kuna ufisadi upo kwa wakuu wa shule za serikali, wamehodhi shule na kuwa mali zao binafsi, elimu imekufa wanaendekeza majungu makazini ADA imekuwa vitega uchumi vyao hali ni mbaya wamekuwa malord father hawaambiliki, serikali tupia jicho hawa jamaa wanabagua walimu mashuleni. Kuna makundi ya team mkuu hao ni watu WA NDIO MKUU ILI WAPATE NIGHT PIA LIPO KUNDI LA ISOLATED YAANI HAWAKO GROUP LA MKUU. TAFADHALI WAMULIKE NI KIKWAZO KINGINE CHA ELIMU BORA TANZANIA.

shule yenye wanafunzi 1000 mkuu wa shule anapiga kama ifuatavyo,

dawati 70,000 x 1000 = 70,000,000/=
lebo 2000 x 1000 = 2,000,000/=
mlinzi 50000 x 1000 = 5,000,000/=
real ya karatasi 15,000 x 1000 = 15,000,000/=
mchango wa mwenge 5000 x 1000 = 5,000,000/=
mahafali 5000 x 1000 = 5,000,000/=
maabara 50,000 x 1000 = 50,000,000/=

kwanini asinunue prado?
 
Ndio hali halisi hyo, wanasema alienacho huongezewa, asienacho ht kile kidgo alichonacho huchukuliwa.. Kwakwel hil suala la Maguful kufuta hii michango shulen kafanya jambo la msingi sn. Maana hii michango ilijenga chuki miongon mwa walimu, ilitenga walimu. Walioshika michango ndio walioneemeka huku wengne wakibaki kutegemea mishahara, na ilihali wakijua mwenzao ana hela ya ziada anapata. Na ubaya hyo michango ilikuwa haifanyi hizo kazi wanazosemea. Utaona kila mwaka mchango wa madawati, mara ukarabati, na madawati gn hayo kila mwk hayatoshelez tu. Na wazazi wakijitahid kuulizia hayo madawati wanaishia kupigwa maneno tu ooh ela bado haitoshi wazazi bado hawatoi, kumbe uongo kila anaekuja ataambiwa hvyo hvyo tu. Na hamtakaa muujue ukweli.. Aah afadhali Magufuli umefuta hayo, wote wategemee mishahara. Kusiwe na matabaka
 
Jamani mtu ana mwezi mmoja tu katika safari ya miaka 5 hadi 10 lakini mnaanza kuzungumza kuongeza muda??

Hebu twendeni taratibu na sio kuserereka na kusimamia baiskeli mteremkoni
 
Watanzania wanaomsifia magufuli wana akili ndogo, na kwa watu kama hawa itachukua karne nyingi sana nchi kuendelea mpaka kizazi hiki chenye wajinga wengi kimalizike, kazi ipi ambayo ameifanya ambayo mtanzania wa kawaida hawezi kuifanya?nani hajui wizi ulioko tra,bandarini, banks, rushwa mahakamani,police,afya?nk, ni rahisi kuwashika wezi wako pale wanafika asubuhi na kufunga milango jioni hata kipofu anaweza kuwashika kama anataka kuwashika, kusifia hili ni ujinga. Tujiulize swali moja kwa nini ameshindwa kutatua tatizo la umeme kwa siku 30, na tuna gesi imeshafika dar, mvua inanyesha, kuna generators zilizokua zinatumika kwenye mgawo wa umeme, kila siku ni mgao kazi zimesimama alafu wenye akili ndogo wanasifia. hii inaonyesha watz wanafikiri vitu vidogo ambavyo kimsingi hawawezi kunufaika navyo.
 
Nchi hii inataka kuendeshwa kwa hisia.

nimeelewa kwa nini kuanzia viongozi hadi watu maskini kabisa walifurika kwa BABU WA LOLIONDO kunywa juice ya mizizi ambayo hata wanapotoka ipo.

uvumilivu ukichukuliwa na Kuridhika na vitu vya juujuu, utapata raia wengi wenye mawazo kama yako.
kipimo cha Magufuli ni miaka mitano.
 
Muda bado na tuone bidhaa zikishuka bei n.k.

bidhaa zote zinazotoka nje zitapanda bei mara dufu, wafanyabiashara wanaoenda china kwa mitaji midogo watakatia, upepo mbaya kibiashara upo mbele yetu.
 
Watanzania wanaomsifia magufuli wana akili ndogo, na kwa watu kama hawa itachukua karne nyingi sana nchi kuendelea mpaka kizazi hiki chenye wajinga wengi kimalizike, kazi ipi ambayo ameifanya ambayo mtanzania wa kawaida hawezi kuifanya?nani hajui wizi ulioko tra,bandarini, banks, rushwa mahakamani,police,afya?nk, ni rahisi kuwashika wezi wako pale wanafika asubuhi na kufunga milango jioni hata kipofu anaweza kuwashika kama anataka kuwashika, kusifia hili ni ujinga. Tujiulize swali moja kwa nini ameshindwa kutatua tatizo la umeme kwa siku 30, na tuna gesi imeshafika dar, mvua inanyesha, kuna generators zilizokua zinatumika kwenye mgawo wa umeme, kila siku ni mgao kazi zimesimama alafu wenye akili ndogo wanasifia. hii inaonyesha watz wanafikiri vitu vidogo ambavyo kimsingi hawawezi kunufaika navyo.

Mkuu sidhani kama una ufahamu wa kutosha kuhusu uzalishaji umeme, it's not that easy, it's not that straight, there is alot of technical issues in it
 
nachukua, fursa hii kumpongeza sana MH MAGUFULI. kwa utendaji mzuri wa kuwawajibisha michwa ambayo ilikuwa inalitafuna taifa hili kwa kasi na hari kubwa. Wito wangu kwako ni kulifumua shirika la umeme tanesco. Maana kuna migao ambayo haina kichwa wala miguu. Na imekuwa kero kubwa sana kwetu wananchi. Tunaomba ulifumue kabisa shirika hili na kulisuka upya.
 
Wakati taasisi nyingine zipo kwenye mchakamchaka wa hapa Kazi tu, Hawa LAPF sijui kama Hili somo la hapa kazi tu wanalielewa vyema.

Mke wangu anafuatilia mafao Ya uzazi toka mwezi June lkn kila siku anaambiwa check yako tayari ila inasubiri tu kupelekwa benki.

Ukikaa wiki moja bila kufuatilia basi wanakupotezea kabisa Ukienda tena siku nyingine inakuwa kama mnaanza Upya hivi.

Utawala mpya umulike utendaji wa mifuko Ya jamii.
Nyie Watu Wa LAPF mlio Hapo Mkwepu Street jengo la Diplomatic House, mbadilike.

Hii ni serikali Ya Magufuli
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom