Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Napenda kumshukuru Mungu kwa kutupatia Rais mwenye kuthubutu kuchukua maamuzi magumu yenye maslahi kwa Watanzania. Hasa hili la TRA na Bandari. Tunamwomba Mungu awalinde katika kila hatua umnayokanyaga wewe na waziri mkuu Majaliwa.
Mheshimiwa Rais Magufuli unastahili pongezi sana lakini kuna mambo bado magumu yenye makandokando mengi sana na yenye kuuzi kama sio kukera tena sana. Hili si geni bali yaliyotendeka katika wizara ya madini na maliasili huko ni shida tupu kama ya makontena na TRA. Huko kumejaa wezi na wahujumu uchumi wetu. Mungu akujalie afya hekima na busara uwapitia hao pia ili kunusuru taifa letu. Namuomba Mungu akulinde ulivyoanza umeonyesha unatosha. Watanzania wazalendo tupo nawe katika jahazi la ukombozi mpya wa Tanzania mpya. Mungu ibariki Tanzania Magufuli na Majaliwa.
 
Ndiyo atakuwa amerogwa, siyo bure haiwezekani mtu mwenye akili timamu afanye mambo kama anayoyafanya. Aliposema pesa za kutupongeza sisi wabunge zitumike kununulia vitanda nlishtuka kidogo ila nikasema mzee ulimi uliteleza. Nikanyamaza na nikahisi kuwa inawezekana kabla ya kuja kwenye kile kijikao alikuwa amekunywa au amevuta kitu maana katika hali ya kawaida mtu asingeamua maamuzi kama yale.

Imagine tumefanya kampeni miezi hiyo, kwa shida ,mateso n.k tumekoswa koswa kuuawa na kuua pia, leo mashirika haya kwa kutambua mchango wetu wametuchangia ili watupongeze kwa kazi kubwa tuliyofanya ya kuomba kuLA kwa wananchi na hatimaye wananchi hawa wametupatia kuLA na nyingine tumejichukulia wenyewe leo tunatakiwa kujipongeza kwa sisi tuliofanikiwa kurudi tena Bungeni anasema eti zikanunue vitanda muhimbili. Kweli? Hii ni akili sawa sawa? Muhimbili wagonjwa wapo miaka na miaka lakini sherehe yetu sisi ni mara moja kwa miaka mitano what was wrong with that? Huyu mzee anatumia kinywaji gani?

Miaka 10 wagonjwa wanalala chini muhimbili hakuna aliyelalamika. Ina maana yeye ndo amewaona sana kuliko sisi wabunge na raHis wetu aliyepita? Huu ni unafiki. Hawa wagonjwa hawaendi kustarehe kule mpaka kila mtu alale kitanda chake.kwani kule lodge? Tena amesababisha kwa hivi sasa wagonjwa wengi hata wakiambiwa wamepona hawataki kuondoka kurudi kwao kwa kuwa kule wakirudi wataenda tena kulala kwenye mikeka. Tumeanza kupata shida mtu hata akiumwa kichwa anakuja kuhimbili anasema sasa kuna huduma nzuri anataka alazwe hata week mbili.
Tena amesababisha hata manesi na madaktari wawe wazembe maana vitanda vingi mpaka vinabaki halafu manesi na madaktari wanalala. Na wengine wamepeleka vingine ofisin mwao.

Haya hilo likapita, leo siamini eti siku ya uhuru nipo home na wife ananambia siku ya usafi. Hajui usafi ushaanza kufanywa na Mh Magufuli huko Bandarini na TRA. Wife naye anashadadia tu leo siku ya usafi mimi roho yangu haijatulia hata nikiwaza usafi huu kwa Mh Magufuli asije akasafisha na kwenye hizi Kamati zetu za Bunge. Maana huku nako si haba kuna kauchafu kake. Wananchi hawashangai kuwa kwa nini tunagombea sana ubunge kwa hali na mali, kwa machozi ,jasho na damu..hata tukiambiwa tupeleke viu
 
Mifuko Ya Hifadhi Ya Jamii ni shida kuna LONGOLONGO sana kule. Asinganganie TRA na Bandari tu azungukie na Huku piaLAPF, PSPF ni shidaaaaa
 
Tehh!Tehh! Bado sana kutoka Mirembe. Ngoja niwaambie wakuongezee dozi
 
Safi sana ila ni wachache watakuelewa. Tatizo umetumia uandishi wa kumchosha msomaji.
 
Lazima wawepo wapinzani kwa kila jambo hata kama ni zuri. Maoni sahihi hapa ni, "TUMPE MUDA". Lkn kama mwendo wa magu utaendelea kuwa huu.... basi ni bora aongezewe muda. Kwani kwa muda mrefu tz kulikuwa na fumbo ambalo lililotolewa majibu mepesi kuwa hakuna ubaguzi wala upendeleo ktk kupeana vyeo vya wafanya maamuzi... na ajira serikalini kwa ujumla bali tulitetea kuwa vyeo hivyo hupewa si kytokana na kabila yake au dini yake wala ukanda bali hutegemea weledi wake.

Lkn mh Magu katufumbulia fumbo hilo kuwa hakukuwa naweledi wwt ktk kupeana vyeo hivyo zaidi ya ushkaji.

Kwa muono wangu kama ni weledi Mh mwenyewe ndio anaetuonyesha.

Tufike wakati tusimamie na kutekeleza yale tunayoyasema kwa kuwa tunayaamini. basi tuseme tu magufuli tulikuwa tunamsubiri miaka 20 iliyopita na hakutokea..... na leo katuonyesha kuwa udhaifu.wake ni mdogo kuliko weledi wake na hivyo "TUMPE MUDA" tujikinaishe thn kama ataweza kuibadili TZ kama alivyoweza kuibadili kagame rwanda. Basi Mh magu anastahili aongrweze muda wa kuwa madarakani.

Poleni wale wenye siasa kali wanaomini hadi leo kuwa LUWASSA Ndie RAIS, na wale wanaoamini kuwa nafasi kama ya urais si zaidi ya mihula miwili. Tulikariri huko nyuma kuwa TZ inahitaji Rais jasiri na mwenye maamuzi magumu. Kama mifumo haijasaidia basi tatizo ni mtu na sio mfumo.

Hivyo kama tunamchagua mtu kwa WELEDI #magufuliaongezewemihula
 

Wewe ulifaulu kiwango kizuri kwenye somo la fasihi. Hongera but siamini kama wengi watakuelewa
 
Oooh!umeona eeeh jinsi gani watu walivyokuwa wanakula kiulaini kama kumsukuma mlevi. Wenye ufahamu wamekuelewa ulikuwa unamaanisha nini. Huyu siyo chizi maarifa Bali anaona mbali.
 
Sasa vilaza wote wamekasirika kwa kuona mtu anafanya kazi, walizoea kuchekewa na kulalamika kutaka posho za kuonga vimada na kutoroka bungeni.
 
Umejitahid sana katika kuwasilisha ujumbe wako japo umetumia fasihi ya hali ya juu sana watu wanashindwa kukuelewa, hongera
 
kumbuka kuna sheria ya mtandao, huwez kumwambia rais wetu mpendwa karogwa, kuwa makin xn umu jukwaan, sifa za kijinga zitakuponza wenzio saa hz wako ndan wananyea debe,na ww pia co mbunge nakujua vzr xn sema umeamua kujifanya chiz kama id yako inavyoonyesha apo, hakuna mbunge mngese kama ww kwenye serikal hii ya awamu ya 5! take care xn kijana ili ndugu zako wasije wakakulilia baadae, uyu co rais wa kumbeza! mbwa we!!
 
u ar so inteligent!
only the briliant and the bright can manage to see at that angle.
 
Naunga mkono hoja ndugu haki kwanza, cku zote nyote njema huonekana asubuh, uko kote rais atapita tu, cha msingi ni kuomba mungu amalize majukum ya tra na bandar salama
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…