Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
nina swali. kama tanzania tunaweza kuprint pesa feki na kuziweka katika system. bas ushaur wangu wenye technlojia hii ya printing tunge waongezea ujuzi na vifaa wawe wana print kwa ajili ya nchi yetu. na sio kwenda kuprint nje ya nchi na kulipa mabilioni ya hela, kuna watu inawalipa ndio. lakini naomba ufafanuzi juu ya ushauri huu. Ni lazima serikali kuprint fedha nchi za nje.
 

mkuu hizo noti feki hata kwa macho unaijua kirahisi.....ndio maana amesema mara nyingi wanawapiga wakulima minadani watu ambao mara chache sana wanatumia noti ya 10,000....ila ni feki kabisaa.

ila hao wanaoziingiza BOT au NMB kama anavyosema mleta mada wanaleta janga kwenye uchumi
 

Hakuna cha mitambo wala nini, wana Scan na kuprint hamna cha ziada
 
Ni jambo zuri sana kwa uchumi wa nchi ila nina wasiwasi endapo tutapiga marufuku uagizaji wa vitu hivyo tutakuwa na uwezo wa kujitosheleza wenyewe...!?isije ikawa ndio tukavipoteza madukani na vikaanza kupatikana kwa magendo.
ni wasiwassi tu.:A S 109::A S 109::A S 109:
 
Ondoa wasiwasi hatuwezi kuvikosa kwakuwa wawekezaji wote wanatafuta nafasi kama hizo ili wazitumie kutanua wigo wa kukuza mitaji yao, ila kile wanachotaka uwahakikishie ni uwepo wa umeme usiokatikakatika ovyo; wakishajilizisha kuwa umeme ni wauhakika, tena kuna amani nchini; watajenga viwanda vingi mno vitakavyo zalisha utoshelevu wa mahitaji ya nchi na kisha kutafuta soko ng' ambo, tena watajitahidi kuzalisha bidhaa za kiwango cha kimataifa. Kwahiyo nchi hatatumia fedha za kigeni kuagiza bidhaa kama zile zilizoorozeshwa hapo juu, na hii ndo itakuwa Tanzania mpya ya Magufuli

Endapo hili halitafanyika, tusiregemee mabadiliko ya uchumi chanya kwakuwa siku zote tutabaki kuwa consumer jambo ambalo siyo zuri kwa nchi inayotaka kuendelea
 

ungebahatika kuishi miaka ya 80-90, ukiwa na utambuzi wa mazingira yanayokuzunguka usingeandika hayo.
 

Kuzipiga marufuku sio solution, dawa hapa ni kuziongezea kodi maradufu au zaidi kisha kusimamia hizo kodi zilipwe. Maana ukiongeza kodi bila kusimamia ndio unawapa nafasi kina Tiagi Masamaki kuchakachua.

Kodi ikishaongezeka automatically importer atalazimika kuweka bei kubwa ili kufidia kodi kubwa aliyolipa. Bidhaa hizo zikikumbana na bidhaa za hapa zenye bei nafuu automatically zetu zitauzika zaidi.
 
Mtoa mada ni mpuuzi tu, hivi Tanapa wana ufisadi gani/upi? Toa hata mfano wa ufisadi mmoja basi tujue, sio kuunga unga story

Wewe kama hujui kitu kaa kimya wenye akili waweke mambo hadharani! Unatetea ujinga mtupu, Kwa Mtanzania mwenye akili hawezi kusema TANAPA hakuna ufisadi! Tafadhali tupeane muda halafu urudi humu kujitetea, inawezekana kabisa wewe na familia yako ni wanufaika na rasirimali za Taifa na siku zinahesabika wapuuzi nyinyi! Huwezi kusema kusema eti TANAPA hawahusiki na utoroshwaji wa Twiga hai! Wewe unafikiri watu wako kimya hawaelewi?
 
Unafikiri bado kuna mambo ya kuundiwa tume tena! Siku zenu zinahesabika hata kama nmajiandaa kudanganya.
 
Tunakupongeza na tunakuombea Mungu akulinde katika kazi hii uliyoianza ya kutumbua majipu. Mheshimiwa Rais Pombe John Magufufuli, sisi wananchi wako tuna hamu kubwa sana ya kujua juu ya utajiri wetu mkubwa unaotokana na gesi iliyogunduliwa hivi karibuni.

Pia tunataka mwongozo wako juu ya utaratibu wa kugawana hii keki yetu tamu tuliyopewa na Mungu. Tunajua kuna jambo kubwa lililojificha juu ya hii keki, haswa pale mtawala aliyekutangulia akishirikiana na wale watu wanaokulaga Siku zote bila kushiba, walipoibua hoja Kule bungeni kwa hati ya dharura.

Sisi wananchi wako tunaokupenda na kukuamini, tunataka utufafanulie, ule udharura ulikuwa ni wa nini. Na je? Ni lini haswa sisi wananchi wenye nchi yetu tutanza kuonja hii Keki?.
 
ukiona mtu anazungumzia keki ya nchi ujue ni chadema wanawaza uchumi wa nchi wagawane wao.
na walikataa kuupisha muswada wa sheria ya gass na mafuta wakitegemea wangechukua nchi ili wagawane vitalu bila nyumbu kujua madhara yake
 
ukiona mtu anazungumzia keki ya nchi ujue ni chadema wanawaza uchumi wa nchi wagawane wao.
na walikataa kuupisha muswada wa sheria ya gass na mafuta wakitegemea wangechukua nchi ili wagawane vitalu bila nyumbu kujua madhara yake
inawezekana ww ni mmoja wa wale wanufaikaji wa hati ya dharura. Lakini jua hii nchi ni yetu wote. Kuuliza juu ya mali zetu siyo dhambi!
 
Nani kakwambia kwamba gesi ni yetu?Je Dhahabu ilikuwa yetu?Almasi ya Mwadui ni yetu?
Unajua kuwa tumewapa wageni mali zetu kwa bei ya chee?Juzi kuna Kampuni inaitwa Swala Energy inatafiti mafuta na imepata gesi inakataa kulipa kodi eti sababu itatumia pesa nyingi,je walilazimishwa?Tuache rasilimali zetu zikae kwani haziozi kuliko kutupa kwa bei ya chee,tuangalie mataifa yaliyofanikiwa kama Algeria na wengine katika miradi hiyo.
 
Ingawa watanzania wengi wamefurahia ujio wa Magufuli kama Rais wa Jamhuri yetu tukufu, bado kuna wengi wanaona kama swala la utawala bora na sheria siyo kipaumbele kwa Rais John Pombe. Naomba nitofautiane kidogo.

1 Kwa nchi yetu ilipofika,bila juhudi za makusudi kutafuta na kuimarisha vyanzo vya mapato hatuwezi kutoboa kama taifa. Kama alivyosema Rais Magufuli, Mafisadi wana nguvu sana nchi hii. Inahitaji ujasiri wa kipekee kupambana nao. Kama mnakumbuka Pinda aliwahi kusema kwamba kuna watu ukiwagusa nchi itayumba!Just imagine....the Prime Minister saying that.

2. Wengine wanadiriki kusema kwamba TZ siyo TRA na Bandari tu. Aangalie na kwingine. Sahihi kabisa. Lakini hivi niulize.....hizo program zote alizoahidi atazitekeleza vipi bila kuwa na pesa? Naamini kabisa akisimamia bandari na TRA......tutapata hela ya kupambana na changamoto za taifa letu. Kiukweli Magufuli ameonyesha kwa vitendo kwamba inawezekana. Ofcourse tuna vyanzo vingi vya mapato. Lakini tujue kabisa huu ni mwanzo.

3. Approach ya Magufuli kufukuza hawa watendaji corrupt na wazembe ni swala la kuungwa mkono. Hivi kuna utawala wa sheria unaoruhusu watu kuiba na kuwa wazembe maofisini? Sasa kati ya hao watendaji wabovu na Magufuli nani hafuati utawala wa sheria? Kiuhalisia wengi wanaolilia the so called utawala wa sheria wanafanya hivo kinafiki. Wanajua kabisa kwamba the so called utawala wa sheria wa kuzungusha kesi mahakamani miaka kumi na zaidi ndo umetufikisha hapa. Na wanajua kabisa bila Ujasiri wa Magufuli mafisadi papa watapeta daima.

4. Magufuli has a vision. Tumpe nafasi. Tumuunge mkono.

Masanja
 
Mkuu uko sawa kabisa. Ila kwa awamu hii ya huyu mtumbua majipu Imani yetu inaanza kurudi, Nina Imani Mali za wananchi zitarudi mikononi mwetu.
 
Ushauri wangu wa sasa kwa Mh. Rais ni kutokuchagua idadi kuubwa ya mawaziri,achague tu mawaziri wachache ila wachapakazi watakaoendana na kasi yake na kumsapoti.
 
Huu uzi ni maalum kwa ajili ya kutazama baadhi ya watanzania ambao sio wabunge ama hawapo kwenye mifumo rasmi ya kisiasa! Lakini sehemu walipo wanatenda kwa uweledi mkubwa sana kujenga taifa lao.

Please kama unamfahamu muandike hapa na sifa zake. Kwa kuanzia tu kuna yule mwanasheria wa NEMC. Sasa, endeleeni. Huu uzi una maana kubwa sana!

Karibuni!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…