1. VIATU NA MIKANDA YA NGOZI TOKA NJE YA TZ
2. TOOTHSTICKS TOKA NJE YA TZ
3. JUICE AINA YOTE TOKA NJE
4. BIDHAA ZOTE AINA YA PLASTIC IKIWEMO NA MIFAGIO AINA YOTE PIA PIPE AINA ZOTE ZA BOMBA
5. BIDHAA AINA ZOTE ZA MBAO TOKA NJE YA TZ
6. KOKI AINA ZOTE ZA MABOMBA
7. BIDHAA AINA ZOTE ZA CHOKAA IKIWEMO NA RANGI
8. AINA ZOTE ZA BIDHAA MASHULENI
9. VYOMBO VYOTE VYA MAJUMBANI
Ukishafanya hivyo yaani Tanzania ya Magufuli ya viwanda itawezekana kabla hata haijafika 2017. Kupiga marufuku bidhaa hizo hapo juu toka nje ya TZ kutachochea ujenzi mkubwa sana wa viwanda vya kutengeneza hizo bidhaa mhimu kwa matumizi ya binadam. wawekezaji wataitumia hiyo fursa kukuza wigo wa biadhara zao na kuongeza ajira kwa Watz.
Jambo la mhimu kwako ni kuhakikisha umeme haukatiki kwakuwa tayari gass asilia ipo. Pia uongee na makampuni yanayo jishulisha na utengenezaji wa bidhaa za kielectronic mfano: computer, simu za mkononi, cd, flash, aina yote ya vyombo vya muziki, memory cards e.t.c kuja kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hizo. Mungu akikupa neema zungumza pia na yale makampuni yanoyotengeneza vipuri vya magari ikiwezekana waje kujenga viwanda vya hiyo shuguli.
Mungu akikuwezesha kuyafanya haya ifikapo 2024 tutaibadilisha katiba yetu ili uendelee kutuongoza kwakuwa utakuwa umeyafanya yale amabayo si marais waliokutangulia tu bali marais wote wa Africa hawajayafanya kuwa wanapoingia madarakani kazi yao hugeuka kujilimbiza mali nying mno ambazo kiukweli hawataweza hata kuzimaliza kwa matumizi yoyote binafis. Kadhia hii imeleta kilio kikubwa mno katika bara zima la Africa, na hii ndiyo imesababisha nchi zote za Afriva kuwa tegemezi kwa weupe huku tukiwazidi kwa utajiri wa vitu vya asili. Ni aibu kubwa imetupata waafrica hata mbele zake YEYE aliyetuumba tumeleta fadhaa kumbwa ya kwamva tumeonekana watu wasiojipenda na wasio na akili hata ya kujua kuwa ni matajiri kuwazidi watu weupe.
Uwepo wa viwanda ktk taifa ni injini ya maendeleo; chonde chonde baba yangu Magufuli wingu la tamaa ya kujilimbikiza mitrilion huk wengi wakifa maskini lisikufunike kabisa bali wewe Rais Magufuli uwe hodari ukafanye yaliyo mema mbele zake aliyekuumba na mbele za watu wako watanzania
Basi, Neema na Amani itokayo kwa Mungu wetu, yaani BABA yetu wa Mbinguni iwe juu yako katika utumishi huu uliokupa Yeye aliyejuu kupita vyote; uwe hodari, ufanye kiume jitie nguvu na wala usiwaonee haya wote wapendao dhuruma na kuhujumu nchi yetu; watu kama ni wabaya si kwa watanzania tu bali hata mbinguni walishakataliwa;
Wewe uwe na moyo wa kuijenga Nchi yetu kwa moyo wa upendo kwa Tanzania na kwa Mungu: Sasa na atukuzwe MUNGU muumba mbingu na nchi yeye aliyetupa kukaa kwenye kiti cha enzi cha Tanzania ili ufanye yaliyo ya akili. Amina na Amina.