Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Sisi wakazi wa jiji tungeomba ufanye ziara uone hali ya jiji ili ujue kwa nini CCM ilishindwa vibaya.ni kutokana na wananchi kuona kama wametelekezwa, miundo mbinu mibovu isiyofanyiwa ukarabati, uchafu nk.barabara zina mahandaki eg vingunguti ambayo inatakiwa kupunguza msongamano wa junction ya tazara lakini imetelekezwa,huko kitunda,kivule etc barabara ni mahandaki.to mention a fiew na kwakuw Tamisemi ipo ofisi yako tunaomba mwongozo.
 
Hizi ziara zimekuwa kama vituko sijui ndo wanatafta kick kwenye magazeti na luninga au ndo kuna mchezo unachezwa wa ubabaishaji ili waonekane viongozi bora kumbe bora viongozi,Tumekuwa watawaliwa wa CCM kwa miaka 54 leo hii ndo waonekane bora vipi hiyo miaka
ya nyuma walikuwa wapi kuyafanya maisha bora kwa kila mtanzania,leo hii kila kiongozi anataka kuonekana mchapakazi kama siyo cinema ni nn hebu shtuka MTANZANIA
NB;NITAUAMINI UONGOZI WA MAGHUFULI ENDAPO UTAPITISHA
RASIMU YA KATIBA YA WARIOBA KUWA KATIBA YA TANZANIA
 
Hii sinema inamaanisha ili Tanzania iendelee kwa kasi iliyonayo,inahitaji katiba mpya yenye nguvu dhidi ya watawala maana si rahisi kumpata magufuli mwingine wakati wote.
 
Naona jamaa fulani wameanza kujitangaza kuna.mdahalo kujadili hhotuba ya raisi..hizo pesa kwanini msiamue.mpelekewn dk mseme zikanunue.arv za wagonjwa...nani anaitaji midahalo wakati tunatafuta pesa za kusomesha watoto bure

mh raisi usikubali watu kutumia jinalako kwa.manufaa yao wanahela zinawasha wakuletee ikulu ututangazie tunazifanyia ninii..
 
Mie namushauri Raisi amuteu either professor Lipumba and huyu professor Ngowi wa Mzumbe kuwa waziri wa fedha. Hwa watu wanaexposure wanauwezo wa kuchambua. Sasa tuwape hiyo kazi ili tuone matokeo. Rais aache kunga'ngania wasomi wanasiasa wanaoendekeza statusquo
 
Kwa akili ya kawaida ni ngumu kwa mtu anayekosoa uteuzi wa baraza lako la mawaziri kumteua kuwa waziri kwenye serikali yako!
 
Kwenye hotuba yako ya uzinduzi wa bunge la 11 ulisema hupendi michakato. Na unataka matatizo ya wananchi yashughulikiwe haraka...HapaKaziTu.
Lkn yawezekana JPM hujui neno mchakato limebeba vitu gani ndani yake. Kwa taarifa yako tu mhe.JPM , hili neno limebeba "urasimu wa kiserikali" (governmental bureaucracy). Yaani jambo linafuata taratibu za kiserikali katk kushughulikiwa kwake ndiyo maana linachelewa. Urasimu (bureaucracy) siyo mbaya, Bali unajenga ufanisi na uhakika wa maamuzi ya serikali. Kibaya ni urasimu usiokuwa wa lazima (red-tape).
Ninaamini ulikusudia kupiga marufuku "redtape" lkn siyo urasimu. Maana hata wewe unaupenda sana urasimu. Tena urasimu unanao upenda wewe unaelekea kwenye red tape.
Umeekaa mwezi mzima ndipo umekuja na baraza la mawaziri nusu. Huu ni urasimu usiyo kuwa wa lazima. Ni bora ungetuambia tu kwamba wizara zilizobakia zitakuwa chini yako. Huo unao ufanya ndiyo mchakato wenyewe. Hutaki kukurupuka. Na wenzako watafanya michakato kwasabb hawataki kukurupuka. Magufuli michakato haikwepeki.
 
Lipumba ni mpinzani
 
Lipumba huyo msaliti wa mabadilik hafai hata kidogo,,labda awe mwenyekiti wa ccm taifa kwenye uwaziri hatumtaki
 
Kukiwa na hatua za hapa na pale za kuchunguza na kubaini kwa jinsi gani serikali imekua ikipoteza mapato yake hasa kwa upande wa kodi ni vizuri vyombo hivi vikafanyia kazi mapendekezo ya wadau yanayolenga kuisaidia serikali.

Niliwahi kuandika kuwa ujanja uliofanyika kwa bandari kavu ambazo kimsingi zilikua na harufu ya utoroshaji makontena ilikuwa ni kuwahammisha wahusika wa bandari hizo,kwa mfano bandari ya PMM,ALIEKUWA inchaji wa TRA alitoka miezi michache BANDARI Kavu ya azam na kuhamishiwa BANDARI kavu ya PMM,Na sasa amehamishwa tena na kupelekwa bandari ya ETC CARGO iliyopo mbagala.Na wengine wengi.


Hatua ya pili ya upelelezi huu ambao ni kama serikali imewaacha wakuu wa Taasisi za umma ambazo ndizo zenye mamlaka ya kuruhusu mzigo huo uingie sokoni kwa watumiaji au hapana,mbali na madhaifu yao lakini mpaka leo unaona si Tbs,tfda wala mamlaka ya mionzi waliotoa tamko kuhusu upotevu wa kontena hizo na kulaani vikali uingizaji wa mizigo hiyo bila kujua ubora wake.

Hatua ya pili ya upelelezi ujikite sasa kwenye taasisi hizi wadau wa bandari ambao wao ndio waliopewa mamlaka na bunge kukagua na kuruhusu mizigo yote kwenda kwa watumiaji kulinda afya za walaji,upelelezi huo ujikite kwenye mizania kwamba je kila kontena iliyotoka ilipita kwenye taasisi za serikali? kama haikupita ilitokaje na nani atakae beba lawama za kuingiza mizigo isiyo salama kwa Watanzania hawa wanaotakiwa kulindwa na serikali yao.

  1. Kimsingi ili kontena itoke bandarini inahitaji vibali vifuatavyo kutoka serikalini ..
  2. RISITI ZA MALIPO YA TOZO ZOTE ZA BANDARI
  3. RISITI ZA MALIPO YA KODI
  4. VIBALI VYA TAASISI ZA SERIKALI( kama vile tbs,tfda,tume ya mionzi,bodi ya sukari),kama mzigo uloingia nchini utawahusu moja taasisi hapo juu ni lazima upate kibali kutoka kwao ndio afisa wa TRA aweze kuupa ruhusa mzigo huo kutoka bandarini.

Kimsingi baada ya tra kukata kodi lazima mzigo upate vibali vya taasisi hizo za serikali na ndipo uingie sokoni au uwafikie watumiaji,lakini kumekuwa na kuikwaji wa taratibu hizo.

Rai yangu kwa serikali ya JPM nikuwa mapato yanayopotea kwenye taasisi wadau wa bandarini ni mengi kwa ujumla wake,Serikali kuwakaba TrA na kuwasahau hawa wengine wakina Tfda na wenzake ni kutoa penyo wa kuendelea kupoteza mapato ya serikali na kwenda kwenye mifuko ya watu.
 
Mbona hizi kampuni zote majina ni ya mama mdogo?
Kunani nyuma ya pazia?

 
Wakuu Mh Rais alishangaa mchanga wa madini kupelekwa nje na pia madini yetu kutorosha. Hebu soma haya majukumu ya TMAA (Tanzania minerals Audit Agencies) alafu unambie hawa jamaa kama si jipu namba mbili baada ya TPA/TRA


  1. To monitor and audit quality and quantity of minerals produced and exported by large, medium and small scale miners; to determine revenue generated to facilitate collection of payable royalty;
  2. To audit capital investment and operating expenditure of the large and medium scale mines for the purpose of gathering taxable information and providing the same to the Tanzania Revenue Authority (TRA) and other relevant authorities;
  3. To monitor and audit environmental management, environmental budget and expenditure for progressive rehabilitation and mine closure;
  4. To collect, analyze, interpret and disseminate minerals production and exports data for projecting Government revenue, planning purposes and decision making in the administration of the mining industry;
  5. To counteract minerals smuggling and minerals royalty evasion in collaboration with relevant Government authorities;
  6. To assess values of minerals produced by large, medium and small scale miners to facilitate collection of payable royalty;
  7. To advise the Government on all matters relating to the administration of the mineral sector with main focus on monitoring and auditing of mining operations to maximize Government revenue;
  8. To promote and conduct research and development in the mineral sector that will lead to increased Government revenue; and
  9. To examine and monitor implementation of feasibility reports; mining programs and plans; annual mining performance reports; and environmental management plans and reports of mining companies.

MH. RAIS TUTUMBULIE HILI JIPU
 
TMAA + STAMICO hayo yote ni majipu makubwa katika kudhibiti madini yetu.
 
Majipu mengine hayajaiva jamani,na hayatakaa yaive ndani ya utawala wa CCM.......mnampa Rais ubaya tu wamiliki wa Chama.
 
Majipu mengine hayajaiva jamani,na hayatakaa yaive ndani ya utawala wa CCM.......mnampa Rais ubaya tu wamiliki wa Chama.

Hili ta TMAA mpaka linatoa usaha lenyewe, kwakweli litumbuliwe tu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…