Kukiwa na hatua za hapa na pale za kuchunguza na kubaini kwa jinsi gani serikali imekua ikipoteza mapato yake hasa kwa upande wa kodi ni vizuri vyombo hivi vikafanyia kazi mapendekezo ya wadau yanayolenga kuisaidia serikali.
Niliwahi kuandika kuwa ujanja uliofanyika kwa bandari kavu ambazo kimsingi zilikua na harufu ya utoroshaji makontena ilikuwa ni kuwahammisha wahusika wa bandari hizo,kwa mfano bandari ya PMM,ALIEKUWA inchaji wa TRA alitoka miezi michache BANDARI Kavu ya azam na kuhamishiwa BANDARI kavu ya PMM,Na sasa amehamishwa tena na kupelekwa bandari ya ETC CARGO iliyopo mbagala.Na wengine wengi.
Hatua ya pili ya upelelezi huu ambao ni kama serikali imewaacha wakuu wa Taasisi za umma ambazo ndizo zenye mamlaka ya kuruhusu mzigo huo uingie sokoni kwa watumiaji au hapana,mbali na madhaifu yao lakini mpaka leo unaona si Tbs,tfda wala mamlaka ya mionzi waliotoa tamko kuhusu upotevu wa kontena hizo na kulaani vikali uingizaji wa mizigo hiyo bila kujua ubora wake.
Hatua ya pili ya upelelezi ujikite sasa kwenye taasisi hizi wadau wa bandari ambao wao ndio waliopewa mamlaka na bunge kukagua na kuruhusu mizigo yote kwenda kwa watumiaji kulinda afya za walaji,upelelezi huo ujikite kwenye mizania kwamba je kila kontena iliyotoka ilipita kwenye taasisi za serikali? kama haikupita ilitokaje na nani atakae beba lawama za kuingiza mizigo isiyo salama kwa Watanzania hawa wanaotakiwa kulindwa na serikali yao.
- Kimsingi ili kontena itoke bandarini inahitaji vibali vifuatavyo kutoka serikalini ..
-
- RISITI ZA MALIPO YA TOZO ZOTE ZA BANDARI
- RISITI ZA MALIPO YA KODI
- VIBALI VYA TAASISI ZA SERIKALI( kama vile tbs,tfda,tume ya mionzi,bodi ya sukari),kama mzigo uloingia nchini utawahusu moja taasisi hapo juu ni lazima upate kibali kutoka kwao ndio afisa wa TRA aweze kuupa ruhusa mzigo huo kutoka bandarini.
Kimsingi baada ya tra kukata kodi lazima mzigo upate vibali vya taasisi hizo za serikali na ndipo uingie sokoni au uwafikie watumiaji,lakini kumekuwa na kuikwaji wa taratibu hizo.
Rai yangu kwa serikali ya JPM nikuwa mapato yanayopotea kwenye taasisi wadau wa bandarini ni mengi kwa ujumla wake,Serikali kuwakaba TrA na kuwasahau hawa wengine wakina Tfda na wenzake ni kutoa penyo wa kuendelea kupoteza mapato ya serikali na kwenda kwenye mifuko ya watu.