Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.

Gazeti hilo halikuzuiwa na serikali lilizuiwa na sheria ya magazeti.Uvunjaji wa sheria wao ndio uliosababisha wao kufungiwa.Kazi ya Magufuli ni kusimamia sheria ikiwemo hiyo waliyovunja Gazeti la The East African sio kuvunja sheria.
 
Tuti Tuti & SONGOKA inaonesha ninyi ni Wazalendo wa kweli ila mnapungukiwa taarifa sahihi ya mnachokisema, niwashauri mtafute taarifa za utendaji wa TMAA kabla hamjajidhalilisha kwa kuchangia vitu msivyojua, taarifa hizi mnaweza kuzipata kwenye hansard za Bunge au hata tovuti ya TMAA mkaangalia annual report zao wameandika nini. Kwa kuwapa kidogo TMAA ni mojawapo ya Wakala bora kwa utendaji hapo TZ na Africa. Organization nyingi za Kimataifa zimeweza kujiridhisha na hatimaye kui-support TMAA katika utendaji wake. Kwa Africa TZ ni ya kwanza kuwa na Wakala wa aina hii. Nchi za Ghana, Malawi, Congo wamekuwa wakija TZ kujifunza jinsi TMAA inavyofanya kazi zake kwa ubora ili nao wakaanzishe (halafu ninyi mnasema uvunjwe!). Moja ya vitu ambavyo JK anajivunia kuanzisha ni TMAA hivyo ni bora mtafute taarifa ya nini hasa wanafanya kuliko kushauri vitu ambavyo tayari vinafanyika. Sijui kama mnafahamu kuwa kuna migodi sasa inalipa Corporate tax (30%) hii ni moja ya kazi nzuri za TMAA. ELIMU NI MWANGA NA NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK
 
Wengine wakati muafaka kwa baadhi ya viongozi kujulishwa mipaka yao

kinachoendelea kwa madc wengine mtaita vituko ukweli src.n kuchelewa uteuzi wa madc kwa mh raisi

kama cham tuwajuze mipaka yao na wapi wanaitaji ushirikiano na wapi wanaitaji kujua mamlaka ya mb..

Tusaidie kutangaza awa watu mapema nahisi tutaona mengi ya musa kabla ya uteuzi ...
 
Ni kweli makonda. Makonda hana staha na hajui mipaka. Na amewadhalilisha polisi maana wamekuwa kama mbwa tu.
 
Hili liko ndani ya uwezo wako na ninakuomba usimwachie Waziri peke yake kwani hataweza kwa kuwa ili kutatua hili tatizo la muda mrefu kunahitaji kushirikisha sekta nyingi ambazo Waziri wa Ufugaji kama yeye hawezi kutatua kwa sababu hana overlapping powers!

Kwangu mimi ni aibu sana karne ya 21 bado Wakulima na wafugaji wanapigana kwa kutumia silaha za jadi kugombania malisho, haya mambo yalipaswa yatokee mwaka 1890' na siyo 2015!

Ninachoshauri kifanyike kwa haraka kabisa, kwanza uzururaji upigwe marufuku, yaani WatanZania wote ni lazima wawe na makazi ya kudumu mambo ya hunters and gatherers yaishe kabisa nchini mwetu!

Watu wastarabishwe na hili linaweza kufanyika kwa kufanya hivi, kwanza watoto wote waliofikisha Umri wa kwenda shule lazima waende shuleni, Serikali ijenge shule za Bweni maalumu kwa hawa watoto wa hawa wafugaji wanaozurura TanZania nzima na kwamba Serikali itumie nguvu ukibidi kuwachukuwa ktk kwa wazazi wao na kuwapeleka shuleni za Bweni ambako huko watachanganyika na watoto wengine ktk sehemu nyingine za nchi kwa kufanya hivi tutakuwa tumeondoa kizazi cha kuwinda na kuzurura nchi nzima kutafuta malisho!

Yaani kusiwe na kijana wa Kimasai au sijui Kihandzabe au Kisandawe mwenye umri wa kwenda shule ambaye atakuwa anachunga ng'ombe, hii ndiyo nia pekee ya kuondoa hili tatizo, vyombo vya dola vitumike kutekeleza hili, mambo ya laiboni sijui jando na takataka gani yapigwe marufuku na kujenga TanZania moja yenye WatanZania waliolingana, hii ni karne ya 21 na haya mambo hayana nafasi tena ni lazima tufanye sasa wakati Katiba yetu bado inaturuhusu tukichelewa na kuleta katiba za Kizungu hili halitawezekana tena kwani kutakuwa na watu kuandamana na kupinga kila jambo!
 
TATIZO NI KUTAFUTA U-DC, au U-RC,
mpaka wanajisahau mipaka yao!!

MTU ANAFUTA LIKIZO YA MFANYAKAZI WAKATI NI HAKI YA MFANYAKAZI!!
 
Ningemshauri Raisi Magufuli badala ya kutaka kutekeleza ahadi nyingi kwa mara moja angewekeza nguvu zote kwenye ahadi kubwa moja au mbili kwa kipindi chote cha miaka 5 kwa mfano anaweza akasema kwamba mpaka mwaka 2020 ni lazima tuwe na Umeme wa uhakika na hapa naongelea labda kuanzi Mw 10 000 na kuendelea na pili kuboresha mfumo wa kodi haya mambo mawili tu Kodi na umeme mpaka 2020 sasa hii maana yake ni kwamba ahadi nyingine zote sijui meli kwenye maziwa yetu au Reli mpaka Burundi na Rwanda au kufufua sijui Air Tanzania zinasimama na nguvu zote kuelekezwa hapa kwenye Umeme na uboreshwaji wa Kodi tu, kila linalowezekana lifanyike ili kutekeleza hili!

Kwa kufanya hivi utakuwa umefanikiwa sana kuondoa tatizo moja au mawili makubwa badala ya kutaka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja kwangu mimi ukifanya hivi mwisho wa siku itafika 2020 kutakuwa hakuna ulichofanya, lkn kama ukichagua moja tu au mawili watu wataona na sasa kama ukiweza kutatua Umeme mengine yote yatafwatia bila ya shida!

Hiyo ni mifano tu lkn unaweza kuchagua kuanza na lingine kama Elimu tu, au kilimo tu au Reli tu lkn siyo mambo mengi kwa wakati mmoja!
 
Mh raisi toka nijaze mafuta n vituo vya total mliman city na bp external.vyenye kuwa.connected.na mashine za tra..

Vituo hivi bunda za karatasi zikiisha mafuta ayatoki. Ukikaa nkajiiliza hawa.wananini wawe connected.na.wengine watoe za.mkononi...nimeona.nikushairi baada ya kuamua kutoa bure efd..hawa wanaotoa mafuta zile pipes zao ziwe.connwcted kama total mliman city...na ikiisha karatas mafuta yanakata..

Kwahizi za mkononi anatoa.anavyojisikia tena wengine sikumoja nilicheka nkanunua na recept za laki kwa sh 5000..nilitakiwa sehemu..wakaanza zitoa fasta..nkajiiliza zinasaidia nn kama naweka mafuta ya alf kumi na tano nkapewa tra rcp za laki kwa shuguli zangu..

Tusikubali watoe mkononi system ya total mliman cty itumike kwa wote..
 
Wakuu habari

Ni mwezi sasa tunashuhudia ziara nyingi na matamshi makali kwa watumishi na taasisi za umma.

Viongozi mbalimbali akiwemo Rais, waziri mkuu na mawaziri wake na wakuu wa mikoa na wilaya sasa, imekuwa kawaida kuchukua vyombo vya habari na kwenda kwenye taasisi za umma kuangalia mapungufu yao.

Viongozi hawa wamekuwa msitari wa mbele kukaripia watumishi wa umma utadhani wao ni malaika.
Na mbaya zaidi wanafanya mbele ya vyombo vya habari kiasi kwamba wananchi wanakuwa wanawadharau watumishi hawa.

Kuna haja gani ya kuchukua vyombo vya habari kuongozana nao na kusema ni ya kushtukiza??

Je huku ni kujitafutia umaarufu wa utendaji?

Mimi ninavyojua, kama kweli kulikuwa na haja ya kuonesha upo serius na kazi na sio maigozo, ni vema ungekwenda bila vyombo vya habari unashitukiza alafu, waandishi wanakuja afu wanakuta ushaondokaa.

Hatutaki maigizo sisi, kama mnaona kunasehemu watendaji hawaendi vizuri mnawaondoa na sio lazima mpaka mtangaze kwenye live media.

Mbaya zaidi unamkuta waziri naye kifua mbele anamkosoa mtumishi wa umma, wakati yeye miaka yote hajawahi kwenda kuwasalimia au kujua nini kinaendelea jimboni kwake, au uozo huo upo jimboni kwake.

Plz Rais magufuli, ni muda wa kazi sasa, maigizo mwachiee JB.
 
Wakuu,

Hivi hii ya kuwakamata Wakwepa Ushuru, na wahujumu uchumi, na Nyama ya wizi, na ngozi na kila kitu halafu wanaambiwa wakalipe maana yake nini? Na tuliisikia wapi vile?

Bakhressa amelipa 2 Billion, kati ya waliolipa. Kwa hiyo kama asingekamatwa asingelipa. Na Raisi anachukua hatua gani, kuwafunga. Manake faini peke yake haitoshi hili ni jitu limekuwa linatuibia halafu maviongozi yetu yanaliomba omba. Na je wale wagonjwa wanaolala chini kwenye mahospitali nchi nzima, wakati yeye anaenda kutibiwa nje?
 

Attachments

  • Bakhressa_Mhujumu_uchumi.png
    52.4 KB · Views: 152
Du mtoa uzi,kwa hali ya kazi ilivyo sasa kuita maigizo,nakuomba usije sema hadharani,watanzania watakupeleka milembe
 
Du mtoa uzi,kwa hali ya kazi ilivyo sasa kuita maigizo,nakuomba usije sema hadharani,watanzania watakupeleka milembe

Mimi namuunga mkono mtoa mada.

Ukitaka kujua ni maigizo angalia shtukiza ya Mh. Raisi na ya hao wengine. Yani raisi akishtukiza media inamkuta huko tayari...tena kama ile ya wizara ya fedha ndo kabisaa tuliishia kupewa picha zilizopigwa kwa simu.

Sasa tofautisha na shtukiza za kina Kigwangalla na Makonda na wengineo....usanii mtupu...all for publicity!!!
 


Jikumbushe kwa kurudia kujisoma sasa, baada ya baraza la Mawaziri wa Magufuli kutangazwa.
 
Mimi ni mtanzania, mwenye mapenzi sana na nchi yangu kama walivyo baadhi ya watanzania wengine! nimeandika post hii kwa uchungu mkubwa sana sababu ni miongon mwa watanzania wachache tusiokupigia kura, na haina maana kwamba sijakupigia kura kwa kuwa si mtendaji" la hasha , bali sijakupigia kura sababu ya kuwepo ndan ya mfumo unaowakandamiza wa tanzania ambao wengi wetu hatukujua hatma ya maisha yetu ya mbelen! kas uliyoanza nayo, kwa hakika ilinifanya nijutie maamuz yangu ya kwa nn sijakupigia kura, sio mm tu hata watanzania wengi bilashaka walijuta juu ya hayo maamuz!

umetujenga sana ki hari, kiiman kias kwamba watanzania tumeanza kuwa na iman na ww! mh rais, pamoja na kusema ayo yote point ya msingi ninayotaka kuiongelea apa ni kwamba ww sio chama, taasis wala shirika, umewekwa apo na wananchi , na upu apo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na wala si taasisi au chama fln, unatakiwa ufanye maamuzi kama maguful wala si kama chama fln cha siasa, wapo viongoz wenzio wanaochukizwa na kas ya uongozi wako hivyo watataka wazorotesha utendaji wako uli uwe na wakati mgum 2020, hivyo unatakiwa kuwaepuka sana viongozi wa namna iyo, sio wao tu bali hata mawazo yao pia.

Taifa limefikishwa kwenye hali mbaya sana kwa sababu za interest za watu fln, ikumbukwe hii nchi ni yetu sote na wala sio ya fln, na hz raslimar ni za kwetu sote wala sio za fln, ninyi tumewapa dhamana ya kuzisimamia kwa maslah yetu sote sababu wote hatuwez kuwa viongozi wa hii nchi.

Hivyo mh rais weka pamba masikion ili usisikie la mtu yeyote wewe ni kuchapa kazi tu, maana wengi wa watanzania wamekuwa wakishtushwa na habar za vikao vyenye lengo la kukupunguza kas, sasa hao hawakupunguz bali wanakuharibia! mungu akutangulie kwenye iyo safar yako ambayo watanzania tumekuwa na iman nayo, na sisi tuko bega kwa bega na ww na tunaku ahid hatutakuangusha
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…