Julius Malema Jr
JF-Expert Member
- Feb 1, 2015
- 653
- 155
Huo wimbo wa UKABILA na UDINI kaimbe na familia yako. Kama hukidhi vigezo usitake ubebwe kwa ajili ya dini ama kabila lako.
Ni kweli kabisa...ila asiishie kwenye makampuni tu...ende hadi kwenye vyama vya kiasa...tunashuhudia baadhi ya vyama ili kupata cheo cha uongozi ni lazima uwe umetokea ukanda flani au umeoa koo flani..
Ukikanyaga mwiba lazima utoe kelele hata kama upo ngangariHuo wimbo wa UKABILA na UDINI kaimbe na familia yako. Kama hukidhi vigezo usitake ubebwe kwa ajili ya dini ama kabila lako.
Huo wimbo wa UKABILA na UDINI kaimbe na familia yako. Kama hukidhi vigezo usitake ubebwe kwa ajili ya dini ama kabila lako.
Wana JF,
Habaru zenu
Nianze kwa kumpongeza Rais Magufuli kwa uzalendo alionao!
Tumo katika zama za kutumbua majipu. Tumemulika sana upande Wa uchumi au mapato ya serikali. Utumbuaji Wa majipu TRA, TPA, PCCB nk.... ni jambo linalotupa faraja.
Japo tumeangalia uchumi, lakini kuna jipu LA AJIRA KATIKA OFISI ZA UMMA. Naamini ni kubwa kuliko yote.
Watanzania tuna haki ya kupata ajira serikalini kwa misingi ya uadilifu. Zisiangaliwe dini, kabila, koo, eneo tunakotoka na jinsia. Cha kuangaliwa uwe uwezo Wa MTU kufanya kazi husika.
Kwa masikitiko makubwa, ajira serikalini zinazingatia dini, kabila na kanda katika wizara na mashirika mengi. Ukuu wa idara unazingatia dini, kabila na kanda. Huu mdudu umeanza kututafuna na utatupeleka pabaya sana.
Tutajikuta tuna dini fulani au kabila fulani ndiyo limeendelea kiuchumi sana kuliko dini au makabila mengine.
Kuna baadhi ya mashirika kama TRA, TPA, NSSF, baadhi ya mabenki nk...., yamelalamikiwa kuwa na ukabila na udini.
Tumefika mahali tumeanza kusema, kwa mfano, kupata kazi maliasili lazima uwe kabila fulani. Kupata kazi Tra lazima uwe kabila fulani, kupata kazi nssf lazima uwe dini fulani.....
Hii nchi ni yetu sote. Tuna haki ya kupata ajira kwa usawa bila upendeleo.
Namuomba Muh. Rais aunde tume ya kuchunguza jambo hili. Kwa mfano, Je TRA kuna zaidi ya nusu ya wafanyakazi kabila moja au dini moja! Kama ni hivyo kwa nini? Tuendelee na uchunguzi katika mashirika na wizara zote. Penye mapungufu ajira ziitishwe upya na uwiano uzingatiwe.
Bila kufanya hivi, watu wataendelea kuvutana na baadhi ya kabila, dini na kanda zitaendelea kuwa za wasindikizaji. Watoto wao hata wakisoma haitokua rahisi kupenya katika ajira serikalini. Barua za kazi lazima zitaendelea kuwekwa kapuni.
TANBIHI
Tuache mtindo Wa kukwepa kuzungumzia udini na ukabila. Tunazidi kulifanya jipu hili liwe kubwa zaidi na sugu. Kadri linavyozidi ukubwa watu wanazidi kuumia. Rais Magufuli tafadhali Pasua jipu hili.
Jipu la kuajiri kwa kigezo cha dini na kabila Lipo sana kwenye baadhi ya taasisi za serikali,ukienda TRA 80% ni kutoka kule na ukienda NSSF 90% ni dini Ile.
Well said mkuu...huu wmbo akaimbe mwenyewe apa anazunguka sana mbuyu ila analenga makabila ya kaskazin I. E wachaga...wameru na wapare...jamaa asilolijua ni kua kwenye taasisi nyingi za elimu wamejaa wanafunzi wa kanda ya kaskazin cz watu wa kaskazin wamewekeza kwenye elimu na ukiangalia ata performance wanaongoza sasa unaanzaje kuwanyima kazi??kna Kimei...Nassari...Msuya etc
Nimeona ulivyo mbaguzi,mdini na mkabila.
Kama huna hulka hiyo, umejuaje wingi wa kabila flan,dini au ukanda fulani.
Na je, kama wana qualification katika nafasi zao wanazuiliwa kuajiliwa kisa mf, wahehe kuajiliwa kanda ya ziwa ama wahaya kanda ya kati?
Mnachuma LAANA zenu wenyewe kwa tabia za kichochezi. Nyumbu mkubwa
OK. Mleta Uzi weka vielelezo
Tatizo dini ile kukunbatia ajira ktk sekta za umma na kudharau wengine wanapojiajiri
Nimeona ulivyo mbaguzi,mdini na mkabila.
Kama huna hulka hiyo, umejuaje wingi wa kabila flan,dini au ukanda fulani.
Na je, kama wana qualification katika nafasi zao wanazuiliwa kuajiliwa kisa mf, wahehe kuajiliwa kanda ya ziwa ama wahaya kanda ya kati?
Mnachuma LAANA zenu wenyewe kwa tabia za kichochezi. Nyumbu mkubwa
Umeongea ukweli mtupu.
Nini kifanyike?