Sithubutu hata Kidogo ati Kujifnya Natoa Ushauri Kwa Mh. Magufuli, Nikijifanya Kuwa Ninaufahamu Kumpita, Kabisa sidhani hivyo. Ila kuna Jambo Moja Tu naona Mtazamo wake sio sahihi. Na Hilo Ndio Nataka Nimshauri autazame upya Mtazamo wake wa Kisiasa Na Akiridhika na Nisemalo Afanye U-turn
Nianze kwa Kusema Namuunga Mkono 1000% Kwa Kukataza Safari za Kipuuzi na Nampongeza sana.
Namuunga Mkono 1000% Kuhakikisha Kuwa Hospitali zetu hasa za rufaa angalau zikikosa dawa basi ziwe na Vitanda na Vipimo na Mazingira safi.
Namuunga Mkomo 1000% Kupambana na Mafisadi
Namuunga Mkono 1000% Kwa Kukusanya Kodi Bila Utani.
Kiujumla anajitahidi, Kuweka Mazingira Mazuri ya Kiuchumi na Huduma za Jamii.
Shida Iko wapi?
Magufuli Bado anaamini Kuwa Kukandamiza Demokrasia na Kuendeleza Hujuma za CCM chama chake, Ni Moja ya Jambo la Maana. Magufuli Bado anaruhusu Unyanyasaji wa Raia na Viongozi wao Kwa Kutumia Vyombo vya Dola kwa Vile tu wanatofautiana na Chama hake. Haiingii akilini Mh Magufuli Kushabikia na Kunyamazi upuuzia unaofanywa na chama chake kwa Chaguzi za Mameya, au Uchaguzi "Fursa wizi kwa CCM" Zanzibar. Baba Mwenye Heshima Mtoto wake akimpiga mtoto wa Jirani, anamlabua na sio kumpongeza. Mama Mwenye Hekima mtoto wake akikamata kuku wa jirani akimleta nyumbani, anatakiwa amuulize umempata wapi, sio aseme, "leta tumnyonyoe tumle" Na hata mtoto, Baba yako akimkata mtoto wa jirani mkono, sio Unasema, "akome alizidi" Kesho itakuwa Ni Mkono wako.
Mungu Nisaidie mbona haya Mambo Ni wazi Natoka jasho Kushawishi Nieleweke Mithili ya Mtu ninayetafuta faida yangu? Far be from it! its out of good faith.
Iwapo Ataamua Kufanya U turn Na Kukuza Demokrasia Nchini, Na Kujenga Mawasiliano na Uhusiano Mzuri na Vyama Vingine, Akapitisha kwa haraka Katiba Mpya isio na Doa, Akaruhusu Kuudwa Tume Mpya ya Uchaguzi, Akakataza Milele Polisi Kupiga Raia. Akasafisha Nchi Kwa haki na Akaongoza Nchi Bila Unafiki wala Uhuni wa Kisiasa.
Kitakachotokea Ni Nini?
Magufuli ataheshimika Dunia Nzima, Atapata Heshima itakayozidi Maelfu ya Viongozi Wakuu waliotawala Dunia, Kuanzia akina Faraoh Ramesses II ....Mpaka Obama, I dont have any doubt about this! Ukiunganisha na Uchapaji Kazi wake na Nia ya Kusaidia Wananchi Umaaru wake Utakuwa Kama wa Mandela, Nyerere, Gandhi Wote Ukiwafunganisha Pamoja. Hata Wapinzani watampenda na Msishangae Akapita Bila Kupigwa 2020. Na hata Inapobidi Kumchukulia hatua Mkorofi bila kujali ni chama gani Kila Mtanzania atakuwa Nyuma yake, kwanini Kwa sababu wanajua Ni mtenda haki kwa Vitendo! Pia Itakuwa Ni Utakaso Kwa CCM na Kwa Vyama Vingine, Nuru ya Haki yake Itamulika Maovu, Kwa Kuwa Atakuwa Ni Kioo cha Watanzania. Historia yake Itakumbukwa Kwa Miaka 1000 Plus! (Nasema Kwa Moyo bila Unafiki) Akikubali Ushauri wangu Miaka Michache tu Dunia Nzima Habari ya Mjini Itakuwa Ni John Pombe Magufuli!, Na hata Vitabu ya Kufundishia Siasa na Baadaye Historia Afrika Nzima, Vitamzungumzia Magufuli, Na Nichomekee tu, "wakati huo Usipojua Magufuli ni Nani Unastahili hata Ufukuzwe shule" Maana haitawezekana, Ni sawa na Uulizwe Umeshamsikia Mandela Useme hapana, "Wawapi wewe?"
Ila asipobadili Msimamo? Asipoacha Kushiriki au Kusimamia Hujuma na Unafiki, Atafanikiwa Kiasi, Na Pengine hata Kushinda tena 2020. Lakini hatajijengea heshima ya Kiwango anachostahili, Na Pia hata Mabadiliko atakayotolea Jasho Hayatadumu!
Yangu Ni Hayo!