Ndugu watanzania
Kuna masuala ambayo rais Dr JPM kwa sasa anaendelea kuyafanya hatua nzuri na mwelekeo mzuri ktk kujenga tanzania yenye uchumi mzuri.
Kwa nchi yetu ilivyo kubwa ni mapema mno kuanza kumsifia rais kwa sababu nchi hii ina matatizo mengi mno ambayo yanahitaji sisi sote watanzania tubadilike kifikra na kitabia.
Moja nchi inatatizo la maji ambalo ni janga kwa nchi ambayo ina ziwa victoria na bahari.
Hili tatizo la maji limeenea karibia nchi nzima ingawa tunaishi lakini maeneo mengi maji ni sugu.
Dawa mahospitali yanapatikana kwa shida kitu ambacho tunahitaji kuwa na mipango ya muda mrefu.
Miundo mbinu mawilayani ni tatizo ambako wakulima wengi ndo walipo tunahitaji kuziboresha kila mwaka walau kwa kiwango cha kokoto.
Umeme kwenda vijini bado nalo ni tatizo kubwa kiasi ambacho tunahitaj kushirikiana na makampuni ya solar kulimaliza, rushwa ni sugu Tanzania kwa sababu ya sheria zetu rais anahitaji kubadilisha sheria zetu ili tudeal na rushwa kikamilifu mfano mtu akibainika ameiba afilisiwe mali zake na kufungwa hii itasaidia kutuweka salama lakini kwa sasa sheria zetu mtu amekwapua bil2 anafungwa miaka 3 tu na kutoka hii inachochea watu kupiga.
Katiba yetu ya nchi isimamie misingi ya uwajibikaji mpaka kwa rais ili rais yeyote atakayekuja katiba aiogope na kumfanya awe mwadilifu leo magufuli anaweza akafanikiwa kuijenga nchi akaja mwingine akaiharibu kwa hiyo kuna umhm rais dr. JPM aiangalie katiba yetu.
Foleni miji kama DSM, Arusha na Mza ni kitu ambacho Rais wetu akifanyie kazi kwa mawazo yangu ni kuhamisha ofc ktkt ya miji na kujenga hosp nje ya miji na ikiwezekana gari zitembea kwa zamu namba zenye A- B zitembee siku zinazogawika kwa mbili na namba C-D zitembee siku ya jumatatu j5 ijumaa na jumapili zitembee zote.
Wafanyakazi washushiwe kodi kwenye PAYE angalau asilimia 2 na kudhibiti mfumuko wa bei kwenye masoko ili maisha yawe nafuu kwa kila mtz.
Kuweka ubia kwenye ndege zetu tutakazonunua kama wakenya wanavyofanya badala ya kuendesha sisi inaonyesha tunafail kila tukiinvest uhitaji wa kuwa ubia mfano na KLM kwa asilimia ni msingi mzuri, hali kadhalika hata kwenye baadhi ya vitu ili kuondoa urasimu kwenye utoaji wa huduma.
Suala la kuficha pesa nje nalo ni tatizo kwa taifa letu...mfano huko visiwa vya jersey na hii report ya panama iliyotoka tunahitaj kuchunguza hili rais ni mfupa kwake, kudhibiti watu kuficha pesa nje kwa kuwa na mifuno dhabiti ya kipesa hasa bank kuu yetu ili iweze kusimamia kwa uweledi.
Mwisho watz tubadilike kazi tunachapa sana hilo liko wazi tatizo ni mioango yetu kukosa pesa na usimamizi ulio imara, tushirikiane kama watz vyama wafanye kazi kwenyebmajimbo waliyonayo kwa kushirikiana na raia hasa matatizo madogo madogo kama marehemu filikunjombe alivyokuwa anafanya. Rais akiweza kuyasimamia haya na tukaona matokeo yake ndo tuanze kusifia.
Kwa sasa tumuunge mkono kwa haya anayofanya na kumkosoa pale anapokosea pale anapojikwaa tumsaidie ili tanzania hii iwe kama rwanda iwe kama south africa iwe kama namibia iwe kama ghana n.k
Week njema.