Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
TL
Magu ni CCM?
CCM wanavua gamba?
Mamba je anatokwa na chozi?
Unafahamu Chozi la mamba ni nini?
Magu alishasema mtawala hapendi kutawaliwa, zaidi hawezi kutawaliwa na vyama vya "ovyo ovyo".
Kama unafikiri unamwonea iko siku atakuliza.
Nakuelewa, Lakini Naweka 0.5% kuwa anaweza Kuwa anavizingiti, Na kwa wakati mwingine anasema-sema tu kufurahisha Genge. Kama Msimamo wake ni Kama wa CCM, CCM hii ninayoijua leo Hataniliza Mimi, Atajuta mwenyewe Kwani atakuwa Ameihujumu Fursa a Dhahabu aliyoipata!
 
Mkuu umeongea point sana. Lakni watakuja majamaa na mapovu,kazi yao ni kulinda CCM halafu wakimaliza wanaenda kudai buku 7 yao.

Mimi naamini siasa safi lazim kiwa na majadiliano maana Magu yeye anajiona anafanya sawa lakini anaweza akawa raisi mmoja wa ajabu sana
Lakini aliyekuwa akiyafanya hayo yote anayoyaomba ndugu yako mlimwita dhaifu! Sasa kaja strong mnaanza kulia! Mlikuwa hamumtaki raisi anayechekacheka, sasa amekuja mwenye sura ya kazi mnataka awachekee!
Please, mod tunaomba wimbo wa " Jua na Mvua unapenda nini?" Nadhani anahusika sana hapa nchini kwa sasa! Nadhani kipo cha kujifunza ktk hizi Bongo flavours!
 
Unamshauri magufuli juu ya demokrasia na utawala bora wakati kwenye chama ukipendcho umejaza genge la wapiga dili na mafisadi,wameshatangaza kugombea urais 2020,kinyume na katiba yenu lakini umekaa kimya
Toa kwanza boriti kwenye jicho lako
 
Alishasema anahusika Znz na Yale ya muungano tuu, yasiyo ya muungano hayamhusu na hawezi tolea uhamuzi. Hawa jamaa miaka michache iliyopita walikuwa wanapiga kelele eabara kuwaamulia mambo yao sasa Leo kwa nn wanalia lia, mtu ambayo anahusika sana Ni JK maana yy ndiye m/kiti na ndiye aliyemweka Shein kuwa rais, JPM bado Hana ubavu huo bwana CCM watampigia Kura ya kutokuwa na imani naye
 
Kwanza napongeza juhudi zako za kupambana na ufisadi kukwepa kodi na nidhamu serikalini lakini kuna sehemu unakosea uncle ivi siku mabalozi wamekuja ikulu ulimuacha mahiga akakuwakilisha sio? Ulikuwa na kazi gani ambayo ulishindwa kuhudhuria? Anyway na siku wamekuja wasanii niliona upo wewe makamu wa Rais na waziri mkuu hivi kwa muono wako wasanii wetu ni muhimu kuliko mabalozi wetu? Embu wasomi nisaidieni hii kitu kidogo maana hawa wasanii tena wa bongo hawalipi kodi wao akili zao kama kina wema sepetu hata umeme wameunganisha kiwizi wizi hawalipi kodi kiufupi hawakusaiidii kuongoza nchi. Kuna baadhi ya mambo unayafanya ni dharau kubwa sana hasa ile ya mabalozi jaribu kubadilika. Mimi ni muumini wa dini ya mwenyezi Mungu nisieamini katika misaada lakini tulipo hapa tunahitaji hawa wakuba watupige tafu la sivyo tutalimia menoo
 
Kwanza napongeza juhudi zako za kupambana na ufisadi kukwepa kodi na nidhamu serikalini lakini kuna sehemu unakosea uncle ivi siku mabalozi wamekuja ikulu ulimuacha mahiga akakuwakilisha sio? Ulikuwa na kazi gani ambayo ulishindwa kuhudhuria? Anyway na siku wamekuja wasanii niliona upo wewe makamu wa Rais na waziri mkuu hivi kwa muono wako wasanii wetu ni muhimu kuliko mabalozi wetu? Embu wasomi nisaidieni hii kitu kidogo maana hawa wasanii tena wa bongo hawalipi kodi wao akili zao kama kina wema sepetu hata umeme wameunganisha kiwizi wizi hawalipi kodi kiufupi hawakusaiidii kuongoza nchi. Kuna baadhi ya mambo unayafanya ni dharau kubwa sana hasa ile ya mabalozi jaribu kubadilika. Mimi ni muumini wa dini ya mwenyezi Mungu nisieamini katika misaada lakini tulipo hapa tunahitaji hawa wakuba watupige tafu la sivyo tutalimia menoo

Mabalozi ndio wanalipa Kodi?
 
Ndugu watanzania

Kuna masuala ambayo rais Dr JPM kwa sasa anaendelea kuyafanya hatua nzuri na mwelekeo mzuri ktk kujenga tanzania yenye uchumi mzuri.

Kwa nchi yetu ilivyo kubwa ni mapema mno kuanza kumsifia rais kwa sababu nchi hii ina matatizo mengi mno ambayo yanahitaji sisi sote watanzania tubadilike kifikra na kitabia.

Moja nchi inatatizo la maji ambalo ni janga kwa nchi ambayo ina ziwa victoria na bahari.

Hili tatizo la maji limeenea karibia nchi nzima ingawa tunaishi lakini maeneo mengi maji ni sugu.

Dawa mahospitali yanapatikana kwa shida kitu ambacho tunahitaji kuwa na mipango ya muda mrefu.

Miundo mbinu mawilayani ni tatizo ambako wakulima wengi ndo walipo tunahitaji kuziboresha kila mwaka walau kwa kiwango cha kokoto.

Umeme kwenda vijini bado nalo ni tatizo kubwa kiasi ambacho tunahitaj kushirikiana na makampuni ya solar kulimaliza, rushwa ni sugu Tanzania kwa sababu ya sheria zetu rais anahitaji kubadilisha sheria zetu ili tudeal na rushwa kikamilifu mfano mtu akibainika ameiba afilisiwe mali zake na kufungwa hii itasaidia kutuweka salama lakini kwa sasa sheria zetu mtu amekwapua bil2 anafungwa miaka 3 tu na kutoka hii inachochea watu kupiga.

Katiba yetu ya nchi isimamie misingi ya uwajibikaji mpaka kwa rais ili rais yeyote atakayekuja katiba aiogope na kumfanya awe mwadilifu leo magufuli anaweza akafanikiwa kuijenga nchi akaja mwingine akaiharibu kwa hiyo kuna umhm rais dr. JPM aiangalie katiba yetu.

Foleni miji kama DSM, Arusha na Mza ni kitu ambacho Rais wetu akifanyie kazi kwa mawazo yangu ni kuhamisha ofc ktkt ya miji na kujenga hosp nje ya miji na ikiwezekana gari zitembea kwa zamu namba zenye A- B zitembee siku zinazogawika kwa mbili na namba C-D zitembee siku ya jumatatu j5 ijumaa na jumapili zitembee zote.

Wafanyakazi washushiwe kodi kwenye PAYE angalau asilimia 2 na kudhibiti mfumuko wa bei kwenye masoko ili maisha yawe nafuu kwa kila mtz.

Kuweka ubia kwenye ndege zetu tutakazonunua kama wakenya wanavyofanya badala ya kuendesha sisi inaonyesha tunafail kila tukiinvest uhitaji wa kuwa ubia mfano na KLM kwa asilimia ni msingi mzuri, hali kadhalika hata kwenye baadhi ya vitu ili kuondoa urasimu kwenye utoaji wa huduma.

Suala la kuficha pesa nje nalo ni tatizo kwa taifa letu...mfano huko visiwa vya jersey na hii report ya panama iliyotoka tunahitaj kuchunguza hili rais ni mfupa kwake, kudhibiti watu kuficha pesa nje kwa kuwa na mifuno dhabiti ya kipesa hasa bank kuu yetu ili iweze kusimamia kwa uweledi.

Mwisho watz tubadilike kazi tunachapa sana hilo liko wazi tatizo ni mioango yetu kukosa pesa na usimamizi ulio imara, tushirikiane kama watz vyama wafanye kazi kwenyebmajimbo waliyonayo kwa kushirikiana na raia hasa matatizo madogo madogo kama marehemu filikunjombe alivyokuwa anafanya. Rais akiweza kuyasimamia haya na tukaona matokeo yake ndo tuanze kusifia.

Kwa sasa tumuunge mkono kwa haya anayofanya na kumkosoa pale anapokosea pale anapojikwaa tumsaidie ili tanzania hii iwe kama rwanda iwe kama south africa iwe kama namibia iwe kama ghana n.k

Week njema.
 
Wasakatonge! Akikohoa makofi, akipiga chafya makofi, bendera fuata upepo.
 
Kila mtu akianza kuorodhesha mambo ambayo anataka Rais ayafanye ili ndio ampe sifa basi hata Magufuli akipewa miaka 30 ya kuongoza haitotosha. Mi nachojua watu wanachomsifu Magufuli kuona ameanza na mwanzo mzuri wenye kuonesha kuwa ni mtu ambaye ana nia ya kweli ya kuleta maendeleo.
 
Sawa tumekubali kumsifia kwa masharti kuwa akikosea tuwe huru kumkosoa pia
 
Wasakatonge! Akikohoa makofi, akipiga chafya makofi, bendera fuata upepo.
Mkuu yawezekana hayo uliyosema ni ukweli kabisa,lakini pia yawezekana wewe ukawa umeliona hilo jambo na ukalisema labda kwa kuwa wewe upo upande wa pili, ila hilo tatizo liko pande zote.
 
Nauliza tu hii mipango imekufia wapi?

Kamata kamata ya machangudoa

Ada elekezi

Safari za nje

Utumbuaji majipu

Ziara kushitukiza
 
Hapo kwenye ada elekezi ndio patamu, kila raia mpenda elimu alikuwa anasubiri kwa hamu kweli, sijui kigugumizi kwake kimetoka wapi?!
 
Kwenye ada elekezi, Mshauri Mwelekezi aliambiwa akarudie kazi maana haikuwa kamilifu kukidhi matakwa, bila shaka kulingana na hadidu rejea!
 
Si
Nauliza tu hii mipango imekufia wapi?

Kamata kamata ya machangudoa

Ada elekezi

Safari za nje

Utumbuaji majipu

Ziara kushitukiza
jakuelewa maana yote yanaendelea wewe uko wapi mwenzetu?
 
Kuna ule msemo wa Maulid wa Kitenge: "mbona kama unapepesa macho?"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom