Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
msababishaji mkubwa wa mishahara hewa ni wakurugenzi, maafisa utumishi na watumishi wa hazina wasio waaminifu. mathalani watumishi wengi walioacha kazi, kufariki na kustaafu bado salary slip zinatoka hazina. maghufuli katika hili asicheke na mtu. mkurugenzi yeyote atakayelipa mfanyakazi hewa kwa maana amekufa,kaacha kazi ama kastaafu afilisiwe mara moja...
 
Kwenye vyeti fake...nusu ya serikali itatoka kazini! Vyombo vya ulinzi ndio usiseme! Labda aanze kuanzia sasa.....sio waliopo kazini!
 
Kwenye kichwa cha uzi huu, marehemu waliokufa ndio watu gani au kitu gani?
 
Sithubutu hata Kidogo ati Kujifnya Natoa Ushauri Kwa Mh. Magufuli, Nikijifanya Kuwa Ninaufahamu Kumpita, Kabisa sidhani hivyo. Ila kuna Jambo Moja Tu naona Mtazamo wake sio sahihi. Na Hilo Ndio Nataka Nimshauri autazame upya Mtazamo wake wa Kisiasa Na Akiridhika na Nisemalo Afanye U-turn

Nianze kwa Kusema Namuunga Mkono 1000% Kwa Kukataza Safari za Kipuuzi na Nampongeza sana.
Namuunga Mkono 1000% Kuhakikisha Kuwa Hospitali zetu hasa za rufaa angalau zikikosa dawa basi ziwe na Vitanda na Vipimo na Mazingira safi.
Namuunga Mkomo 1000% Kupambana na Mafisadi
Namuunga Mkono 1000% Kwa Kukusanya Kodi Bila Utani.
Kiujumla anajitahidi, Kuweka Mazingira Mazuri ya Kiuchumi na Huduma za Jamii.

Shida Iko wapi?

Magufuli Bado anaamini Kuwa Kukandamiza Demokrasia na Kuendeleza Hujuma za CCM chama chake, Ni Moja ya Jambo la Maana. Magufuli Bado anaruhusu Unyanyasaji wa Raia na Viongozi wao Kwa Kutumia Vyombo vya Dola kwa Vile tu wanatofautiana na Chama hake. Haiingii akilini Mh Magufuli Kushabikia na Kunyamazi upuuzia unaofanywa na chama chake kwa Chaguzi za Mameya, au Uchaguzi "Fursa wizi kwa CCM" Zanzibar. Baba Mwenye Heshima Mtoto wake akimpiga mtoto wa Jirani, anamlabua na sio kumpongeza. Mama Mwenye Hekima mtoto wake akikamata kuku wa jirani akimleta nyumbani, anatakiwa amuulize umempata wapi, sio aseme, "leta tumnyonyoe tumle" Na hata mtoto, Baba yako akimkata mtoto wa jirani mkono, sio Unasema, "akome alizidi" Kesho itakuwa Ni Mkono wako.

Mungu Nisaidie mbona haya Mambo Ni wazi Natoka jasho Kushawishi Nieleweke Mithili ya Mtu ninayetafuta faida yangu? Far be from it! its out of good faith.

Iwapo Ataamua Kufanya U turn Na Kukuza Demokrasia Nchini, Na Kujenga Mawasiliano na Uhusiano Mzuri na Vyama Vingine, Akapitisha kwa haraka Katiba Mpya isio na Doa, Akaruhusu Kuudwa Tume Mpya ya Uchaguzi, Akakataza Milele Polisi Kupiga Raia. Akasafisha Nchi Kwa haki na Akaongoza Nchi Bila Unafiki wala Uhuni wa Kisiasa.

Kitakachotokea Ni Nini?

Magufuli ataheshimika Dunia Nzima, Atapata Heshima itakayozidi Maelfu ya Viongozi Wakuu waliotawala Dunia, Kuanzia akina Faraoh Ramesses II ....Mpaka Obama, I dont have any doubt about this! Ukiunganisha na Uchapaji Kazi wake na Nia ya Kusaidia Wananchi Umaaru wake Utakuwa Kama wa Mandela, Nyerere, Gandhi Wote Ukiwafunganisha Pamoja. Hata Wapinzani watampenda na Msishangae Akapita Bila Kupigwa 2020. Na hata Inapobidi Kumchukulia hatua Mkorofi bila kujali ni chama gani Kila Mtanzania atakuwa Nyuma yake, kwanini Kwa sababu wanajua Ni mtenda haki kwa Vitendo! Pia Itakuwa Ni Utakaso Kwa CCM na Kwa Vyama Vingine, Nuru ya Haki yake Itamulika Maovu, Kwa Kuwa Atakuwa Ni Kioo cha Watanzania. Historia yake Itakumbukwa Kwa Miaka 1000 Plus! (Nasema Kwa Moyo bila Unafiki) Akikubali Ushauri wangu Miaka Michache tu Dunia Nzima Habari ya Mjini Itakuwa Ni John Pombe Magufuli!, Na hata Vitabu ya Kufundishia Siasa na Baadaye Historia Afrika Nzima, Vitamzungumzia Magufuli, Na Nichomekee tu, "wakati huo Usipojua Magufuli ni Nani Unastahili hata Ufukuzwe shule" Maana haitawezekana, Ni sawa na Uulizwe Umeshamsikia Mandela Useme hapana, "Wawapi wewe?"

Ila asipobadili Msimamo? Asipoacha Kushiriki au Kusimamia Hujuma na Unafiki, Atafanikiwa Kiasi, Na Pengine hata Kushinda tena 2020. Lakini hatajijengea heshima ya Kiwango anachostahili, Na Pia hata Mabadiliko atakayotolea Jasho Hayatadumu!

Yangu Ni Hayo!
 
Mkuu umeongea point sana. Lakni watakuja majamaa na mapovu,kazi yao ni kulinda CCM halafu wakimaliza wanaenda kudai buku 7 yao.

Mimi naamini siasa safi lazim kiwa na majadiliano maana Magu yeye anajiona anafanya sawa lakini anaweza akawa raisi mmoja wa ajabu sana
 
Wewe kwa imani na akili yako hasa unafikiri yeye hayajui hayo? Kama unafikiri kama hayajui hayo basi unahitaji psychological evaluation, honestly! Hukufanya vibaya kutimiza wajibu wako though!
 
Wewe kwa imani na akili yako hasa unafikiri yeye hayajui hayo? Kama unafikiri kama hayajui hayo basi unahitaji psychological evaluation, honestly! Hukufanya vibaya kutimiza wajibu wako though!

Misimamo Inampofusha Mtu, Haina maana Kila Lililo wazi Kwako Liko wazi kwa Mwingine, Kuna Msemo usemao, "I showed you the stars and the moon but all you could see was the tip of my finger" The Question is not whether you had eyes, but whether you wanted to see! Hata Mimi Nimekuwa Nikiwaza Kama wewe, Hivi kweli inawezekanaje asione hili, Halafu Nafasi aliyoipata Ndio Nafasi ya Pekee? Lakini Pia Nikajiuliza Inakuwaje Mtu aihujumu Fursa yake ya Dhahabu yeye Mwenyewe. Nikaamua Tu wacha Nisiassume, Nishauri tu akiniona Juha Basi.
 
Lazima wenyewe watakuwa wanakucheka wenyewe huku wakisema,"there is more to it than meet the eyes, son!"
 
Makufuli hana ujasiri huo unaomfikiria wewe,sisi kina gogo la shamba tulishasema ujasiri wa mtu unaonekana pale anapotetea haki bila kujali kama atapoteza maslahi aliyokuwa nayo. sasa ukimuangalia Makufuli wakati wote akiwa waziri alikuwa anamsifia sana Kikwete kuliko waziri mwingine yoyote katika utawala wa Kikwete hivyo alikuwa anaogopa kupoteza maslahi yake,sasa anayoyafanya kwa sasa ni yale tu, yasiyoweza kumpotezea maslahi ndio maana hawezi kuwashughulikia watu kwenye upande wa ccm maana huku anaweza kupoteza maslahi. mfano mzuri ni uchaguzi wa meya dar wewe umesikia yule aliyepeleka hati feki ya Mahakama amechukuliwa hatua gani? upende usipende tunayokuambieni sisi kina gogo la shamba tuna huwakika nayo, nawaomba wana JF zigatieni sana tunayoyasema
 
Anafahamu ila anaogopa, usicheze na ccm wanaweza kumtoa kwenye urais akawa raia wa kawaida, ulizia habari za IDD amin Dada walimtoa kwenye urais akawa raia na akaikimbia nchi yake
 

Hii ndo shida ya watz wengi, ili ushauri wako uwe na bases ya future ni lazima ujue the past and the present, huwezi kumshauri mjinga kabla hujamuelimisha, bado hajui na haelewi maana na umuhimu wa hayo unayomshauri, so toa elimu kwanza
 
Wewe kwa imani na akili yako hasa unafikiri yeye hayajui hayo? Kama unafikiri kama hayajui hayo basi unahitaji psychological evaluation, honestly! Hukufanya vibaya kutimiza wajibu wako though!

Misimamo Inampofusha Mtu, Haina maana Kila Lililo wazi Kwako Liko wazi kwa Mwingine, Kuna Msemo usemao, "I showed you the stars and the moon but all you could see was the tip of my finger" The Question is not whether you had eyes, but whether you wanted to see!
Ushaur hauna miguu wala kichwa
Nisamehe lakini Nahisi Ni wewe unaweza kuwa huna kichwa, Ila miguu I hope Unayo.
 
Wabongo mnaupenda sana uhuru lakini kinyume chake uhuru huohuo unawafanya kuwa watumwa.

Msipo jitambua mtaendelea kuteseka sana badilikeni sasa.
 
Mtoa mada nalo jambo lkn cccm itAweza kumove on
Uncle magu tumuombe ajarib kuya gusa ayo km kwel amna remote ya msoga
 
Mh. Magufuli amezungumzia Kuwa anakerwa anapoona Kuwa CCM, hawakubali Kushindwa, Hii Kwangu Ni hatua Nzuri ya Yeye Kuona, Tatizo Kubwa la Nchi yetu (Uhuni wa Kisiasa) Lakini Pia Inawezekana Kwa sababu huyu Jamaa ana akili mno, ameamua, Kupuliza (kupooza wasio CCM) Baada ya Kuona CCM ilivyoamua Kutoa gloves na Kung'ata Masikio Zanzibar ni too much, hivyo akaona Apulize Kupooza. Lakini Nisimwonee Inawezekana Ni mambo yanayomuudhi sana ila Kuna yanayomkwamisha! Au inawezekana Ni uma puliza Kama ya Nyerere kumuibia Salmin Urais Zanzibar 1995 kutoka kwa Seif Sheriff Hamad, Kisha Akagoma kumwibia Mrema ubunge Temeke.
 
TL
Magu ni CCM?
CCM wanavua gamba?
Mamba je anatokwa na chozi?
Unafahamu Chozi la mamba ni nini?
Magu alishasema mtawala hapendi kutawaliwa, zaidi hawezi kutawaliwa na vyama vya "ovyo ovyo".
Kama unafikiri unamwonea iko siku atakuliza.
 


Soma hapa.
Link DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMTUMIA SALAAM ZA PONGEZI DK. SHEIN KWA USHINDI ZANZIBAR
 
Hivi siku hizi posho ni 7000? Nilifikiri bado 5000. Gharam za maisha zimepanda.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…