Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
MUHESHMIWA DR JPM, MULIKA JESHINI HUKUUU.
TAFUTA MIFANO YA NCHI NYENGINE ZEMNYE MAJESHI MADOGO KWA UWINGI WA WATU LAKINI VIFAA VYA KUTOSHA NA VYA KISASA.
- WALIMU, MADAKTARI, WAUGUZI, MAFUNDI, MABAHARIA, NA FANI NYENGINE MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA.
JESHI NA WIZARA YA ULINZ ZIJITEGEMEE KIUCHUMI NA KUSAIDIA NCHI KATIKA SEKTA ZENYE UPUNGUFU KAMA VILE ELIMU, AFYA, MIUNDO MBINU NA HASAHASA KILIMO.
JESHI LIAJIRI WATAALAAM WA KILIMO NA LILIME KWELIKWELI KUONDOA TATIZO LA CHAKULA.
 
MUHESHMIWA DR JPM, MULIKA JESHINI HUKUUU.
TAFUTA MIFANO YA NCHI NYENGINE ZEMNYE MAJESHI MADOGO KWA UWINGI WA WATU LAKINI VIFAA VYA KUTOSHA NA VYA KISASA.
- WALIMU, MADAKTARI, WAUGUZI, MAFUNDI, MABAHARIA, NA FANI NYENGINE MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA.
JESHI NA WIZARA YA ULINZ ZIJITEGEMEE KIUCHUMI NA KUSAIDIA NCHI KATIKA SEKTA ZENYE UPUNGUFU KAMA VILE ELIMU, AFYA, MIUNDO MBINU NA HASAHASA KILIMO.
JESHI LIAJIRI WATAALAAM WA KILIMO NA LILIME KWELIKWELI KUONDOA TATIZO LA CHAKULA.
jeshi lipewe matrekta badala ya vifalu uwiiiiiii
 
Kwanza nikupongeze kwa jitihada zako za utumbuaji majipu ambapo baadhi ya watu wameendelea kuhoji na kuzikosoa. Binafsi nimefarijishwa na utumbuaji huo kwa kuwa kilio chetu hasa watoto wa wakulima kilikuwa hilo genge la mafisadi. Mh.Rais, nikuombe sana kwa utashi wako kabisa na kwa dhamiri yako uliyoionesha katika kututumikia maskini wa nchi hii na kuipiga pasi nchi yetu naomba nikushauri jambo moja. Nakuomban utengeneze taasisi imara, na hii itatokana na katiba thabiti maana tunaweza kufurahia utawala wako miaka mitano au kumi na baada ya hapo kikawa kipindi cha kilio karne nzima kwa njama za mafisadi. Ili kujenga taasisi imara nakuomba uishughulikie katiba mpya kwa kufanya mambo mawili penye uwezekano. Kwanza napendekeza uitishe bunge la katiba ambalo halitakuwa na wanasiasa ili kuifufua rasmu ya mzee Warioba ambayo inabeba maoni ya wananchi na wewe umedhihirisha kuwasikiliza wananchi na kuwatumikia kwa moyo wako wote. Pili, kama kuifufua rasmu ya mzee Warioba ina ugumu wa kisheria, naomba serikali yako ifanye marekebisho ya kisheria ili kuruhusu uwezekano huo. Kama bado kutaonekana kuleta utata, naomba serikali yako ianzishe mchakato wa kura ya maoni ili katiba inayopendekezwa ipitishwe na kisha uifanyie marekebisho makubwa ili kuingiza maoni halali ya watanzania yaliyohujumiwa. Kwa kuyafanyia kazi hayo utakuwa umewapatia watanzania zawadi ya karne na karne kwa kupata katiba bora na hivyo kuepuka mikono ya wanyonyaji. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki katiba ya wananchi, Mungu mbariki rais wetu Dr.Pombe Magufuli
 
Barua yako imenefikia kijana lakini matakwa yako ni magumu sana yako nje ya uwezo wangu.....
 
Amuagize waziri wake wa Fedha aweke kwenye Finance Bill 2016 mependekezo ya kuondoa misamaha mbalimbali ya kodi ikiwemo ile ya marais (wa JMT and SMZ) na pia posho za wabunge na wafanyakazi wa serikali ziwe zinatozwa kodi. Hiki ni chanzo kizuri tu cha mapato....pesa hizo zikasaidia kutoa elimu bure kwa watoto wetu.
 
muombe haya mukiwa kitandani anakupakua nadha atakusikilaza kwa umakini na ubunge wa vitanda maalum pia atakupatia
Mkuu unalijua vizuri somo la subnetting?
Wenzio wanyea debe kwa sasa
Stay tuned!
 
Hakuna kama Magufuli wapinzania hawana hoja wala pa kuhemea zaidi ya kukimbia mijadala bungeni.
 
ANGU aingie madarakani nasikia ameshatumbua majipu zaidi ya 160.

Majipu hayo ni wanasiasa na watendaji wakuu waliokuwa kwenye taasisi nyeti. Walitumbuliwa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kutimiza majukumu yao au kushiriki kwa namna moja kwenye vitendo ya ufisadi.

Wametumbuliwa hadi sasa inauma hadi watetezi wa haki za binadamu wanamkosoa Rais. Wanasema Rais anachofanya eti si haki, eti hafuati utawala wa sheria ambao unamtaka mtuhumiwa kupewa nafasi ya kujitetea. Wengine wanamshutumu Rais kwamba si haki kumfukuza mtu kwenye majukwaa ya kisiasa.

Lakini jambo jema, JPM hakusubiri naye amewajibu “wanasema tunawanyanyasa sijui haki za binadamu eti kwa sababu tunawatangaza hadharani kwa hiyo wao walikuwa na haki mno kuwaibia hadharani Watanzania, waliwaibia Watanzania hadharani lazima tuwatangaze hadharani, mateso waliyoyapata Watanzania mamilioni kwa sababu za kuibiwa na hawa wachache lazima na wao waanze kupata hayo mateso.

“Kwa hiyo unaweza kuona hawa wanaowatetea nao ni majipu nao tutaanza kuwafuatilia, lakini kwa bahati nzuri aliyewateua ni mimi na niliwataja hadharani kwa hiyo kwa nini wafurahi siku ya kuteuliwa na wasitajwe hadharani siku ya kutumbuliwa,” amesema.

Katika hili, mimi sioni tatizo maana utawala wa sheria tumekuwa nao tangu tupate Uhuru mbona haukulisaidia Taifa hili kupiga hatua. Mbona mfumo huo wa utawala ndio uliofanya Tanzania kuwa shamba la bibi watu wakawa wanaiba watakavyo. Wengine wakatamba kwamba ni nyoka wa makengeza, pale wanapoona kuna rupia inanukia lazima watie mguu.

Tena wanaosema vile ni wale walioshiriki hata kutunga sheria zetu na wanajua udhaifu wa sheria hiyo uko wapi. Tukashuhudia watu wakapiga fedha nyingi tu kupitia akaunti za EPA, wale wote walioshtakiwa sijawahi sikia kama kuna mtu mmoja kafungwa, zaidi ya kufungwa wale watani wangu wa Kigoma tu na yawezekana walifikia huko kwa kuwa hawakujua kutumia pesa hizo walizokwapua, kama alivyosema wakili mmoja wa taasisi yetu ya kusaka mafisadi.

Lakini wengine wote sijawahi kusikia kama wamefungwa, halafu leo hii tunalilia utawala wa sheria kwa faida gani nchi imepata kupitia utawala huo wa sheria? Nasema JPM ni heri uitwe dikteta kwa faida ya Watanzania, sioni faida ya utawala wa sheria! Kuna ufisadi mkubwa tu umefanyika kwenye Escrow, Richmond lakini mbona hakuna mtu ambaye amefungwa jela licha ya kuwa kulikuwa na utawala wa sheria?

Mbona wahusika wote tunawaona mitaani wakiendelea kutamba na hayo mapesa waliyokwapua? Kwa kweli kwa Tanzania kulilia utawala wa sheria ni kutaka turudi nyuma wajameni. Mnataka turudi kwenye zama za watu wachache waendelee kufaidi nchi hii, wakati mamilioni tukizidi kuogelea kwenye dimbwi la umasikini.

Angalia wale tunaolilia utawala wa sheria, wafanyakazi hewa tumeimba miaka mingapi, lakini bado watu waliendelea kuneemeka na fedha hizo na huku wakijenga majumba mazuri na kutembelea magari ya kifahari wengine tunabaki kuwakodolea mimacho tu.

JPM kwa maneno yake anasema ’mpaka leo wafanyakazi hewa tuliowatoa kwenye register wamezidi 7,700 na bado uchambuzi unaendelea, sasa mnaweza mkaona kama kuna wafanyakazi hewa wa namna hiyo ndani ya serikali, hayo mabilioni ya fedha yangeweza kwenda kwenye huduma mbalimbali.”

Lakini kuna watu ndani ya Serikali ambao wanashughulika na watumishi, walikuwa wanapokea mishahara miwili na zaidi na hata kutumia wafanyakazi hewa kukopa. Tunashangaa huko mitaani mfanyakazi wa Serikali inakuwaje anakuwa na fedha lukuki kiasi hicho? Kumbe wenzetu walikuwa na njia ovu za kupata fedha hizo.

Hao ni mafisadi na kwa bahati mbaya ndio waligeuka kuwa wafadhili wakubwa kwenye tafrija zetu za harusi, Huko makanisani tuliwaona miungu watu, maana walitoa michango ya ujenzi wa makanisa kutoka kwenye walizoiba na sisi tukawapigia makofi na kuwaona watu wenye upendo.

Halafu mnasema eti turudi kwenye utawala wa sheria, una faida gani kwetu? Nakuomba Rais wangu JPM ongeongoza kama wanavyofanya kule China. Leo hii China ina maendeleo kwa sababu hailei mafisadi. Tena wao wanaenda mbali zaidi ukikutwa na hatia ya ufisadi lazima ufe na mali zako zitaifishwe. Natamani sheria kama hiyo sasa itungwe Tanzania.

JPM ifanyie kazi hii ili uweke mfumo ambao hautegemei mtu, hata siku ukiacha madaraka utakuwa umeacha mifumo mizuri ya kushughulika na wezi wa mali za umma. Tanzania haihitaji tena utawala wa sheria, kuruhusu hilo ni kuruhusu kuendelea kuibiwa.
 
Usitamani kila kitu, China haina uongozi mzuri wa kuigwa. Kama kuna vitu vizuri vya kuchukua basi tamani hivyo.
 
Hivi akili inakutuma kwamba maendeleo yanaletwa na mtu mmoja? Dira ya nchi yako unaijua kweli hata kwa miaka miwili ijayo mpaka sasa ama miaka 50 ijayo?
 
Naunga mkono hoja,asiige ujamaa ila baadhi ya Sera za China.Akiziintroduce Bongo nani ataiba na kazi zitafanyika.
Ndiyo tunahitaji bunge live lakini uchumi ndiyo hoja ya msingi.Watanzania wanalia na umasikini ishu live weng hata hawajishughulishi nayo.
 
Ukila sana vichwa kuku akilinazo hufanana na za kuku
 
Usitamani kila kitu, China haina uongozi mzuri wa kuigwa. Kama kuna vitu vizuri vya kuchukua basi tamani hivyo.

Ipi ya kuigwa sasa shamba la bibi? Mimi ni miongoni ya ninaotaka kuanzishwa sheria ya kifo na kufirisiwa ukutwapo na hatia ya ufisadi. Si lazima tuchukuwe yote ya China lakini tulipofika angalau hili moja ni sawia. Wangapi wamekufa kwa kukosa dawa kisa mafisadi wamezimeza na bado tunacheka nao! Mimi binafsi ilifika mahali mtu mwenye kitambi nikamchukia kwa imani kuwa lazima awe fisadi.
 
Rekebisha hapo..." atuongeze " nina imani umemaanisha atuongoze
 
Utawala wa sheria ni lazima uwepo. " Rule of Law ".

Hakuna anayetakiwa kuwa juu ya sheria za nchi.
 
BARUA YA WAZI KWA RAIS WA JMT, DOKTA; JOHN POMBE MAGUFULI
Tupe akina “DAU” Wengi

Mheshimiwa Rais, kwanza nakuamkia shikamoo na hongera sana kwa kuliongoza na kulisimamia ipasavyo taifa letu hili pendwa la Tanzania, sisi wananchi wako wa huku Liwale hasa kata hii ya Mpiga miti tunafarijika sana na mwenendo mzuri wa serikali hii ya awamu ya tano unayoisimamia.

Mheshimiwa Rais, kwa kuwa upo serikalini muda mrefu utakuwa unafahamu vema kuhusu tukio la mwaka jana hapa wilayani kwetu LIWALE, la vurugu kuhusu STAKABADHI GHALANI, kwa kweli huu mfumo ni JIPU na linahitaji kutumbuliwa iwapo kweli unahitaji kuiendeleza nchi hii ambapo sisi wakulima ndio wengi kuliko sekta ingine hapa Tanzania. Sitaki kwenda ndani zaidi kuhusu jipu hili kwani nahofia unaweza ukalitumbua kwa haraka kisha jipu hili likaota tena.

Mheshimiwa Rais; Sisi wakulima ndio watu ambao ni masikini wa kutupwa, japo kuwa ndio sekta yenye wataalamu wengi kuliko sekta yeyote, lipo tatizo ambalo wengi wa viongozi wetu hawalioni, na ndio maana badala ya kutuletea mbegu bora wanatuletea mbolea, balada ya masoko yatakayo nufaisha mkulima mmoja mmoja wanatuletea Stakabadhi ghalani, Tatizo hilo ni kwamba hatuna Viongozi bora, Viongozi wenye kuthubuti, wenye kujituma na wenye mapenzi thabiti ya kuendeleza taifa letu pendwa, viongozi kama Dokta Ramadhani Dau.

Mheshimiwa Rais; Wiki ya jana ulifungua Daraja la kigamoni nimefarijika sana japo nimelioma kwenye video na picha tu, Daraja ambalo ulitueleza kuwa wazo lilianza toka enzi ya mkoloni lakini wazo lilishindikana, ikafika mahali ukapongeza na kusifia jitihada za shirika la NSSF, Bodi yake na hasa ukampongeza Dokta Dau,kwa juhudi zake za kiuongozi katika kufanikisha kwa ujenzi wa daraja hilo.

Mheshimiwa Rais; Daraja limewashinda watu wengi, lakini kuja kwa aliyekuwa mkurugenzi wa NSSF kwako, Daraja liliwezekana, wewe mwenyewe kwa kushirikiana na Dokta Dau, mmejaribu, mkajenga na mmeweza, kwa nini usitutafutie viongozi kama Dau katika sekta yetu hii ya Kilimo? Akina Dau hao walete mapinduzi ya pili ya kijani, watuunganishe na Masoko, Akina Dau watakao simamia vema rasilimali za Taifa hili.

Mheshimiwa Rais; ntakwambia tatizo kubwa linaloikumba nchi yetu, ni kutokuwa na aina ya viongozi kama yako, viongozi kama Dokta Ramadhani Dau, viongozi wenye uwezo wa kusimamia majambo na yakatekelezeka, ni viongozi wawili tu ambao mnastahili pongezi kubwa, wa kwanza ni wewe mwenyewe ulisimamia barabara na zikajengwa na wa pili ni Dau kasimamia Daraja lililomshinda mkoloni na likajengwa, tena kwa pesa zetu za ndani, Hakika watu kama Dau wanastahili kupongezwa, na tunahitaji akina Dau katika sekta ya Kilimo.

Mheshimiwa Rais; Tunakuomba tuletee Dau huku kwenye Korosho, tuletee Dau kwenye Katani, Tuletee viongozi kama Dau kwenye Ufuta na Pamba, tuletee Dau alete mapinduzi ya Kilimo Tanzania.

Mwisho nasema hayo ni mawazo yangu tu yananisumbua kwa muda mrefu sana nimeona kwa kuwa wewe umekuja kwa kauli mbiu ya hapa kazi tu pengine unaweza ukafanyia kazi kwa kutuletea viongozi kama Dau tukasonga mbele.

Nakuombea kwa Mungu akupe hekima na busara katika kutekeleza majukumu Mazito ya kuingoza Tanzania.

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Hassan Mchunga
S.L.P 40
Mpiga Miti
Liwale-Lindi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom