Wewe
VUTA-NKUVUTE tatizo lako ni nini? Unaogopa nini Magu akikabidhiwa chama? Ni vyema kuendeleza BAVICHA kuliko kurukia mambo ya CCM ambayo CDM wameyashindwa. Ngoja tuweke kwa ufupi hapa uozo wa katiba ya chama kinachojinadi cha demokrasia.
Mosi, ukomo wa madaraka, nafasi ya uenyekiti CDM ni nafasi ya kifalme, unaruhusiwa kuishika hadi uchoke mwenyewe, ingekuwa hii kitu ipo kwenye katiba ya CCM au ya Tz kuna nyumbu wangejidai wanaipenda sana demokrasia ila kwa kuwa ipo CDM, nyumbu wote wapo kimya.
Pili, sheria kandamizi dhidi ya uhuru wa mwanachama wa CDM kwenda mahakamani, katiba ya CDM inawakandamizi wanachama wake, ukienda mahakamani kuishtaki CDM, na ukashindwa kesi ni umejifukuzisha uanachama, hii ni sheria kandamizi tena kwa chama kinachojinasibu katika demokrasia ya kweli, ndio kitanzi hichi hichi walikitumia kumuondoa ndugu
Zitto, he CDM ni chama cha demokrasia?
Tatu, tumeshuhudia CDM wakitumia muda mwingi wakituhumu watu kutofuata sheria au katiba, je CDM wanafuata na kuheshimu katiba yao? Kutokuwepo kwa watu wanaowazonga zonga CDM haimaniishi ni wasafi, ila bado hawajapata umuhimu wa kukosolewa katika mizania sawa na CCM, mfano mdogo tu ni katiba ya CDM inasema wazi Nafasi ya katibu mkuu lazima ijazwe ndani ya miezi mitatu baada ya kuachwa wazi, je kwa nini hii sheria haikufuatwa au kina Lisu wanajua kunyoosha kidole kimoja kwa CCM tu?