Kabla ya kilio cha kuadimika kwa madawa katika mahospitali yetu hakijaisha, sasa kimeibuka kilio kingine cha wanafunzi wengi wa vyuo vikuu kukosa mikopo na hivyo kuendelea kuongeza lawama kwa serikali.
Mh.Raisi,lawama hizi kwa mtazamo wangu si za lazima kabisa bali ni za kujitakia tu kwa nyinyi kushindwa kuwa na vipaumbele na zaidi watu kutaka kuishi maisha ya anasa kwa gharama ya serikali,serikali ambayo teyari ina mzigo mkubwa wa kuhudumia wananchi wake.
Mh.Raisi,mimi nina ushauri mmoja tu kwako juu ya namna bora na ya haraka ya kumaliza tatizo hili bila hata kuathiri bajeti ya serikali wala kuhamisha mafungu na mambo mengine ya aina hiyo.
Mh.Raisi,unachotakiwa ni kufanya maamuzi magumu ya kufuta sitting allowance za wabunge na kuondoa magari ya anasa maarufu kama mashangingi serikalini.
Unachotakiwa ni kupeleka muswaada /mapendekezo Bungeni katika Bunge lijalo la November au January mwakani ya kuwataka wabunge waachane na malipo haya ya sitting allowance ili fedha zitakazookolewa zikahudumie watoto wa masikini pamoja na kuboresha huduma za jamii.
Malipo haya jamani ni ya aibu kwa wanasiasa waliotuomba kura kwa lengo la kutetea masikini na wanyonge wa nchi hii.Hivi nyinyi watu hata nafsi zenu haziwasuti kuendelea kulipwa fedha hizi?Mbona mwalimu au Police traffick hana kitu kinachoitwa standing standing allowance?Nyie huu uhalali wa kujilipa fedha hizi mnaupata wapi?!
Mh.Raisi,nina hakika hakuna atakaepinga hadharani pendekezo hili kwani hata wao nafsi zao zinawasuta kupokea fedha hizi ila tu imekosekana nguvu ya kupendekeza jambo hili lifike mwisho.
Mh.Raisi,eneo lingine ni hili la matumizo ya magari ya anasa maarufu kama mashangingi kwa mawaziri na viongozi wengine waandamizi serikalini.
Magari haya mbali na kuwa yananunuliwa kwa gharama kubwa,lakini hata gharama ya kuyahudumia ni kubwa mno kuanzia mafuta,vipuri,service,n.k.
Hivi kuna ulazima gani wa waziri,naibu waziri,makatibu wakuu,wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya umma, wakuu wa mikoa,wilaya,vigogo wa polisi,magereza, na jeshi wote kutumia magari haya?
Hivi Land Cruiser Mkonge New Model haziwatoshi?Anasa za aina hii katika ya umasikini huu kwa faida ya nani?Nani atakaethubutu kupinga hili?Atakaekupinga kwanini usimfukuze?
Mh.Raisi,kaa na watendaji wako kisha mfanye tathimini juu ya kutekeleza uamuzi huu na zaidi muweke timeframe ya kutekeleza mpango huu.
Mh.Raisi,maamuzi ya aina hii ndio tunayoyata.Huu ndio udikteta tunaouhitaji na sio ule wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na mambo mengineyo yanayafanana na hayo.
Fedha zitakazopatikana zilelekeza kwenye huduma za jamii kama vile kununulia madawa na vifaa tiba,ujenzi wa madarasa,kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu,n.k.
Mh.Raisi,hebu jiulize bei ya shangingi moja ingesomesha watoto wangapi wa masikini vyuo vikuu?
Mh.Raisi,kama mliona kuhudumia nyumba za serikali ilikuwa ni gharama mpaka mkaamuza kuziuza, kinawashinda nini kwenye mashangingi haya?
Hivi katika mataifa tajiri na yaliyoendelea,viongozi waandamizi serikalini wanatumia magari haya haya ya gharama?
Naamini hata UkAWA waliposema elimu bure mpaka chuo kikuu,vichwani mwao walikuwa na policy za aina hii sera ambazo nyinyi zimewashinda kwa kukosa dhamira na uthubutu tu.