kwanza nikupongeze kwa kazi unaoyoifanya, pia nikupe pole kwa uzito wa majukumu. katika yote uyafanyayo kitu kikubwa umekuwa uki hakikisha unabana matumizi na kusimamia mali za nchi kwa faida ya taifa, mimi binafsi ningependa kugusia hili la mali za nchi hususani zinazotumika kama vitendea kazi kwa maendeleo ya taifa. sote tunafahamu gharama kubwa inayotumika kuvipata, katika utendaji wako baadhi ya wanaopewa dhamana ya kusimamia katika idara fulani fulani, ili kuhakikisha kuwa wako salama wanatumia mtindo wa kuweka ndugu au jamaa katika idara aliyopo kwa sababu sasa hivi wanasema watu hawaaminiani. hili linasababisha hasara kubwa na isiyo fahamika. kwa sababu wanaowekwa wanakuwa hawana uzoefu. wazoefu wanapelekwa sehemu tofauti zisizokua za taaluma zao. au utakuta mtu ametenda kazi kwa weledi na kwa muda mrefu anaondolewa. hii ni kuwavunja moyo na kujenga chuki. wanaowekwa kindugu au kijamaa huaribu au kuboronga kwa sababu hawana uzoefu au heshima ya kazi kwa sababu tu: amewekwa na mkuu wa idara. hawa watu wa huku chini kwa kweli wanaliingizia taifa hasara kubwa sana. haijulikani ni kwa sababu linapotokea janga ripoti huandikwa ya uongo. mfano mdogo hapa tunapofanyia kazi kuna mkuu mmoja baada ya kuhamishiwa tu, alimleta dereva mwingine na kumtoa aliyemkuta, wakati aliyemtoa aliendesha gari hiyo kwa miaka tisa na miezi minne, na jamaa walikua wanamsifia sana kwa utunzaji wa gari. aliyepewa mgeni kakaa nayo wiki tatu, kaiangusha na haifai tena. na jamaa alikua jeuri sana kwa sababu tu ameletwa na mkuu. viongozi wa mkoa wapo na walimweleza amwachie driver gari, lakini hakuwasikia wakuu wake, nao pia wakafanya kosa kunyamaza, jamaa yupo na kapewa gari nyingine na aliyekua anaendesha hiyo ya pili kawekwa benchi. mfano mwingine jamaa kaletwa asimamie mradi kaleta na ndugu zake. baada ya muda watu wakapunguzwa lakini alihakikisha ndugu zake wamebaki. ndugu yake mmoja aliiba vitendea kazi. lakini sijui ripoti iliandikwaje, vilinunuliwa vingine na kazi inaendelea. na hiyo fedha iliyonunuliwa hivyo vifaa vingine ni ya serikali, kwa kweli huku ni majanga hizi gari zinazopiga chini kila siku sijui zinaandikiwa ripoti gani, au sababu ya ajali ni nini !! zipo gari kwenye miradi ambazo zinatunzwa sana, ukichunguza ni zile ambazo madreva ahabadilishwi anakua ni mmoja tu. na inarudishwa serikalini katika hali nzuri sana. vivyo hivyo mashine, n.k . hawa wakuu wanapohamishiwa sehemu ya kazi wawe na hekima. mtu anapokua ametunza kifaa chochote alichokabidhiwa athaminiwe na kinapoenda sehemu nyingine apelekwe huko huko aendelee kukitunza, kwa sababu hana haja ya interview, amesha pasi kwa 100%. tusioneane aibu wengine waumie: kazi nzema.