Habari wana jamii wenzangu matumaini yangu ni kuwa sasa Tumejipumzisha na kusubiria weekend ianze lakini nina wakumbusha haya,
Je ungepata fursa ya kupewa microphone pale ikulu kuuliza swali kama wenzako walivyopata fursa hii ungemuuliza swali gani?
Kabla ya kuhainisha maswali ambayo ningemuuliza kwanza tuone makundi ambayo yanapata fursa ya kumhoji mheshimiwa Rais na wanaishia kujikanyaga tu wakati katamka anataka wa kumchalenge postively , saa nyingine wakishindwa kuuliza maswali muhimu kwa kuogopa nini sijui,
Kundi la kwanza ni BUNGE Waandishi wa habari nwametuaminisha kuwa baadhi ya wabune na bunge kwa ujumla linamuogopa mheshimiwa na pengine wanapopata fursa wanashindwa kuitumia kuuliza mambo ya msingi,
Kundi la Pili ni .MAWAZIRI mheshimiwa aliwahi kusema kuna mawaziri wanalalamika chini chini juu ya baadhi ya maamuzi yake, lakin hawajitokez kumshauri,
Sasa kundi la Tatu ni waandishi wa habari wamekuwa waoga mno ni aibu kwa wandishi wa habari. mekuwa kuwa mkisema juu ya Mawaziri kumuogopa Magufuli, sasa nao wameonekana kuwa miongoni mwa kundi linalomuogopa mheshimiwa Magufuli, unapataje fursa ya kukutana na Rais Magufuli akakuruhusu kumuuliza swali ukashindwa kuuliza yafuatayo?
NAANZA MASWALI YANGU OPENLY
1.Mheshimiwa Rais kuna tetesi kuwa ugumu wa uongozi wako unaletwa na mazingira mabovu uliyoachiwa na mheshimiwa KIKWETE na we umekuwa ukilalamika sana juu ya kwamba nchi imekuwa shamba la bibi, sasa mheshimiwa kutokana na kauli hizo je
a. unaweza kutuhakikishia vipi kuwa kuna kuhusika direct katika kutengeneza mazingira hayo magumu mpaka inakutesa wewe kuanza kusafisha upya?
b. katika juhudi zako za kusafisha nchi kuna sehem viongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya awamu iliyopita wanavyokukwamisha au kuna jinsi unavyopata kigugumizi juu ya ilo?
2. Swali langu la pili ni kuhusu IPTL, mheshimiwa rais unazungumziaje suala la IPTL mkataba wa kihuni ambao umetuingiza hasara kubwa sana watanzania ,au kuna mkono wa mkubwa yeyote ambaye anakwamisha suala ili?
3. Kuhusu Elimu , mheshimiwa rais hivi kuna hathari yeyote ukiamua wewe na wataalamu wa elimu kwa mamlaka uliyonayo kuviangalian upya baadhi ya vyuo na taasisi ziziso kidhi vigezo ili kutengeneza mazingira kwa watu walio serious katika masuala ya uwekezaji kwenye elimu wakafanya hivyo? na ambavyo havikidhi vigezo kufungiwa bila kuingiza siasa?
4. Kuna Uwezekano wa kurejea upya mikataba juu ya uuzwaji wa nyumba za serikali kwa awamu ya uongozi wa mheshimiwa mkapa? ili kama kuna watu walipata nyumba katika mazingira yasiyoeleweka either warejeshe au walipe, na pia shirika la nyumba likatoa maelezo juu ya kwanini mazingira kama hayo yalijitokeza?
5.Mheshimiwa Rais swali ili linahusu AJIRA KWA VIJANA NA UHAKIKI, lina vipengere 3
a.mheshimiwa umejihakikishia vipi kuwan uhakiki unaoendelea hautochelewa tena na kusababisha ajira kuendelea kusubiriwa?
b. Je hakuna njia yeyote ambayo inawezwa ikaundwa bodi ikibidi we uisimamie mwenyewe ianze mechanism ambayo itafanya uajiri bila kuleta Contradictions na kuvuruga zoezi la uhakiki uku zoezi la uhakiki likiendelea?
c. mheshimiwa kwanini zoezi la uhakiki lisiwe la miaka yote ili kuzuia kumaliza kuhakiki hapa wakingiza ujanja, ? yaan zoez la uhakiki liwe la miaka yote uku shughuli nyingine zikiendelea, maana haimaanishi kuwa uhakiki ukiisha ni kuwa pamesafishika hundred percent,
nimeishia hapo nakabidhi microphone
pia nina uhakika mheshimiwa atapitia uzi huu naomba muulize maswali mengine yasiyo ya uchochezi,
pia naomba JF MODERATORS MSIUNGANISHE UZI HUU MHESHIMIWA ATAUPITIA PLEASE,