Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
swali
1:alipokuwa kenya alisema tz tuna mpango wa kukuza uchumi ktoka 7.9% had kufikia 7.2% na kusisiza,je hizo takwimu alikaririshwa au ilikuwa ni akili yake?..
 
*SERIKALI IPIGE MARUFUKU MATAMASHA YA FIESTA NA MATAMASHA MENGINE YOTE YANAYOZIDI KUMOMONYOA MAADILI YA VIJANA WA KITANZANIA KWA KUENEZA, KUHALARISHA NA KURASIMISHA UHUNI NCHINI*

Na Emphraim Makamba

SABABU kuu ya mimi kuandika waraka huu ni hofu kubwa inayo niandama baada ya kuona matamasha haya yameachiwa kuendelea kutamalaki nchi nzima kwa kuvuka mipaka ya majiji na sasa kuanza kuzitafuna mpaka halmashauri za miji midogo midogo ya Tanzania. Kwa hakika majiji kama Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, mambo ya kihuni na ya hovyo hovyo imekuwa sasa ni kama moja ya mambo muhimu katika maisha ya watu wahuni ila sasa ninapoona uhuni huu unapelekwa mpaka vijijini siwezi kuendelea kuwa mnafki na kunyamaza kimya. Ninaomba mnisaidie kupaza sauti yangu iwafikie wale wenye mamlaka waliopo kule juu.

Fiesta ni tamasha kubwa la KIHUNI nchini. Mahali popote ambapo tamasha hili linapokuwa likifanyika ni wazi kabisa mambo mbali mbali ya kihuni huwa yanakuwa yakifanyika sambamba na tamasha hilo kabla, wakati na baada ya tamasha.

NUSU UCHI ndio namna ya kuvaa mavazi kwa dada zetu na binti zetu wakati tamasha hili linapofanyika. UKAHABA na UFUSKA ndio mahala pake na hufanyika wazi wazi katika viwanja hivyo na biashara ya ukahaba na madawa ya kulevya hufanyika kupendezesha matamasha haya. Wasanii wanaoimba MATUSI MATUSI katika nyimbo zao ndio hupata nafasi kubwa ya kusherehesha matamasha haya na husafirishwa kwenda kusambaza UCHAFU huo mpaka mikoa ambayo haina hatia na uchafu wa mijini. Fiesta Rukwa, Tabora, Singida, Lindi, Manyara na mikoa midogo midogo mingi mpaka kufikia hali ya kusikitisha sana. Wasanii kama Snura wa chura, ManFongo wa hainaga ushemeji, Shilore na Kanga moko na wasanii wengine wengi wanaosifika kwa mashairi ya kihuni kihuni na kutumbwiza kwa kucheza nusu uchi ndio hupata nafasi kubwa sana ya kusafiri kwenda kusambaza huu UPUUZI katika mikoa yote midogo midogo nchini.

Mwaka 2005 baada ya Rais wa awamu ya nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuingia madarakani kwa mara ya kwanza kama mkuu wa nchi, nilipata nafasi ya kukutana na Chief of Staff kwa chakula cha mchana na alitaka kujua nini maoni yangu kuhusu swala la vijana hasa hasa nyanja za utamaduni na maadili. Tuliongea mengi ila nilimwambia kitu kimoja ambacho nilimuomba akichukue kama dira. Nilimwambia kwamba:

*Erick Shigongo* na *Joseph Kusaga* ni vijana wawili nchini wanaotakiwa kudhibitiwa haraka sana kupitia vyombo vyao vya habari vya Global Publishers Limited na Clouds Media Group kabla ya janga kuu la mmomonyoko wa maadili utakaoikumba taifa hili na isipatikane tiba ya haraka kwa muda mrefu. Wote tumeshuhudia namna magazeti ya udaku ya Global publishers yanavyoharibu kwa kasi jamii yetu. Wote tumeshuhudia na tunaendelea kuwa mashahidi wa namna jinsi CLOUDS MEDIA GROUP kupitia vyombo vyake vya habari vya Clouds Fm na Clouds TV vinavyojitahidi kila siku kubomoa kizazi hiki cha vijana wetu wa kitanzania kwa namna mbali mbali mpaka kufikia kuanza kuhamasisha USHOGA kwa kufanya mahojiano na shoga kupitia televisheni hiyo ambayo vijana wengi wanaiangalia na kuipenda. Juhudi na ushauri wangu uligonga mwamba baada ya kuona mkuu ndio kwanza anashikamana na hawa ambao kwangu mimi ninawaita Prime Suspects wa chanzo kikubwa cha kasi ya mmomonyoko wa maadili ya vijana wetu hapa nchini.

Wito wangu kwa serikali ni kwamba, *IT IS NOW OR NEVER* Kama tunataka kuokoa taifa hili la vijana wetu basi tuchukue hatua sasa lasivyo ifafikia mahali tutashindwa kuzuia upuuzi huu kama vile ilivyo kwa mataifa mengi ambayo ni wahanga wa upuuzi huu. Wazazi tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kuwatunza na kuwalea vijana wetu katika maadili safi na bora ya kumcha mwenyezi Mungu lakini pia serikali nayo itusaidie kwa maswala ya kiujumla. Tusikubali UHUNI kuwa sehemu ya utamaduni wetu.

_Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki vijana wetu wote nchini._
 
Uo naona ni wivu tu unakusumbua ......

Wenzio wanafanya ubunifu wa Ajira na kipato we ubabaki kulia lia
 
Rais yupi atapiga marufuku? Au unasemea FIESTA ipi?

Mkulu jana alisema anatamani awepo na yeye sema majukumu tu,hivyo ataangalia live kupitia Tv.

Ukute hata leo akawepo kwa kujiachua zake bila walinzi. Hahahahah!
 
Rais nae alisema anataka kuhudhuria hilo tamasha...,..

hapo ndio utakapouona ugumu wa kampeni yako.
 
Wanasemaga haina ushemeji atiii😎😎😎 Aibu kwa Taifa lol😵
 
Waungwana kwema!

Kutokana na hali ya nchi ilivyo na maisha ya watanzania yalivyo je wewe unadhani kipi kiwe kipaumbele cha taifa. Je kwa muono wako unafikiri kipaumbele hicho kitaweza kuwaletea wananchi maendeleo? Je, wewe ukikabidhiwa utawala utaweza kusimamia kwa asilimia ngapi kipaumbele hicho. Na je njia gani utakazozitumia kufikia malengo husika.
 
1479059532028.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom