Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hivi unajua muda unaotumia shangingi from dar to dom au maeneo mengine??? Kinachomatter ni comfort na muda wa kufika kwenye ziara zao... hivi umtoe wazir dodoma to mtwara kwenye mkonga??? Hahaha sasa atakuwa ana tofauti gani na mkuu wa kitengo??? Acha wale maisha ili na wewe ufight uje uyakute hayo mambo... imagine ungekuwa wewe waziri je ungeshauri hivyo?? Suala la sitting allowance kikwazo ni wabunge wa ccm kwani wao kwa wingi wao ndio wenye nguvu ya kujenga hoja ya kuindoa hiyo kitu. But kumbuka ndio mshahara wao na perdiem hiyo...
 
Mbunge anapokea 12 milioni kwa mwezi. ..hivi iyo pesa wanaweza kukopeshwa wanafunzi zaidi ya watatu kwa mwaka
 
Ndio maana huwa sitoi michango ya madawati ma vitu vingine vya aina hiyo.
 
Sasa kama pesa hakuna wauze shangingi wamuuzie nani sasa kama baba analalamika njaa watoto jee ...
 
Kwaio unataka magufuli ageuke bunge maana hio sheria si itabidi iridhiww na hao wabunge? ambao wataikataa, mkulu atageuka legislature n executive....
 
dah.. mkuu ungepata kachanc ka sekta ya kumshauri na kumshawishi ili akubali nazan tungekua mbali kidogo... ila tuishi kwa matumaini kwamba ujumbe utafika
 
Mh Rais nimejiuliza maswali mengi magumu juu ya hatma ya Tanzania chini ya utawala wako. Ni ukweli usiopingika kuwa Wasukuma wana uzoefu mkubwa wa utawala kutokana na mfumo tulilipitia wa Kitemi.

Kwa upande wangu toka moyoni mwangu kwa mfumo unaotumia kiutawala una matokeo hasi zaidi kuliko chanya. Kwanza mipango ulinayo ni mizuri kwa taifa hili lakini Urais una ukomo, ungekuwa ni utawala wa kifalme matunda yako tungeyafurahia.

Pili impact ya maendeleo kwa wananchi wa kawaida ni ndogo sana. Kulalia huko ni sawa na Herode alichofanya kwa kumwadhibu Yesu ili awafurahishe Wayahudi.

Tatu kutrain wasomi sana katika siasa ni kazi.Uhalisia unaonyesha wengi wao si wa kweli.

Nne walio upande wako ni wachache.Namanisha wapo hapo kwa ajili ya mishahara.

Tano washauri wako wameufanya uongozi wako kuwa mgumu. Hapa pana changamoto kubwa.

Sita nakushauri huu ni wakati wako wa kutekeleza kauli mbiu yako ya Hapa Kazi tu kwa vitendo.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Sisi wanaume wa kiafrika kuwa na wanawake watatu, wanne au watano ni jambo la kawaida Sana....
 
Nature ya mtu ni vigumu kuibadilisha kwa muda mfupi but as time goes watu watajifunza kitu na Ku shape their mind baada ya kuona output waliyoitarajia ni tofauti na kama jinsi walivyofikiri hivyo kuwa na subira muda ni mwalimu mzuri
 
Leo tarehe 19 Oktoba 2016; hapa jamii forum pekee zaidi ya post 5 plus hii yangu nimeziona zikiongelea chuki ya wananchi dhidi ya utawala serikali.

Potelea mbali waweza kusema ni propaganda za wapinzani na mafisadi kama ilivyoada kutoa majibu mepesi kwa maswali na mambo mhimu yanayohitaji uangalizi mkubwa, ila kuna jambo mh. Rais kama uko makini bila shaka ulitakiwa kuwa umeligundua, fuatilia matukio ya na mlio wa ngoma (maoni ya wananchi utaelewa).

Zilianza tetesi za mizigo bandarini likapita.

Ikaja mtikisiko wa uchumi BOT wakakanusha.

likaja issue ya deni la taifa BOT watakakanusha,

likaja issue ya maisha magumu na kupotea kwa pesa ukasema mafisadi wameficha pesa,

likaja ukosefu wa dawa mkasema hakuna tatizo,

likaja tatizo la mikopo ya wanafunzi bado galina majibu ya kutosha,

Walimu wametoa siku 15 unaona km mzaha tu, kuna issues ya watu kushushwa madaraja kiukweli linamkera kila mtumishi.

Chukizo la kila kijana ni AJIRA KUSITISHWA LINAMPA KICHEFUCHEFU na HASIRA kila kijana maana ni muda ambao vijana wengi hawajui mstakabali wa maisha yao.

Serikali tutasema mengi na kujitahidi kujivua majukumu mengi ila twende turudi bado serikali inalo jukumu la kupanga msitakabali wa wananchi (vijana) wake. Huwezi kusema tukalime pasipo kujua tukalime wapi? Tulime nini? na kulime kupeleka wapi? Juzi kati mwezi wa 8 na 9 tumeshuhudia nyanya zikioza, hapa naongea ila walima tikitiki wanajua machungu waliyonayo moyoni.

Mh. Rais ebu sumbua kichwa kubuni mikakati ya ajira URAIS si rahisi kuna kichwa majibu rahisi hayawezi kutufanya tukuone kama baba. Kutana na vijana na watu wakushauri binafsi siamini kama wewe pekee unaakili ya kutatua matatizo yote ya nchi hii.

Narudia kutana na vijana tukupe mawazo yetu ujue wapi tumekwama na wapi usaidie tusonge mbele.
 
Nimekuelewa sana mkuu
 
Rais pitia hapa uone vijana wako tulivyo makini nawe!

umetuliza vijana kwa mengi ,ajira na,mikopo kwa wanavyuo ,
 
Kuna vijana wapo wamemzunguka Kama vile makonda, hapi na gumbo wanatosha
 
Hakika umenena mkuu, JPM ausome huu uzi na kuufanyia kazi, asiwaletee watu maisha ya kikoloni hii nchi ni ya watanzania wote, wote tuna hati miliki halali.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…