Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Debe limepaa kigoma debe pamoja nakusaga 20000 jekwampango watani 1.5 tutanunua5000?
 
Wakati ameingia rasmi kazini baadhi walimshangilia na baadhi kuwa na wasiwasi. Alijitabanaisha angekuwa mkombozi wa vibarua katika ofisi yake. Alichagua kiranja mkuu ambaye hakujulikana sana na kuchagua wasaidizi wa kiranja mkuu ili iwe rahisi. Hapo ndipo wengi waliaanza kugawanyika kwani vibarua walihoji utendaji wa baadhi ya viranja kutokana na wao kuwa viranja katika uongozi uliopita. Vibarua wakajipa moyo huenda amekuja mkurugenzi mpya wataweza kubadilika. Kweli kwa muda wa miezi kadhaa ya mwanzo mkurugenzi pamoja na viranja walionyesha mbwembwe zao katika nyadhifa zao. Baada ya muda mkurugenzi akaamua kushuka chini tena kishirikiana na kiranja mkuu kuchagua viongozi wa vibarua katika maeneo yao wanakoishi. Hapo napo palionekana kama mkurugenzi anatoa fadhila kwa baadhi yao. Walalahoi wakaingiwa na hofu mioyoni mwao ila wakajipa moyo.

Sasa ofisi ikawa imekamilika sababu maeneo yote yanaviongozi pendwa wa mkurugenzi na wanamheshimu na kumnyenyekea.kazi zilianza kwa manjonjo kama wafanyavyo bondia wanapopima uzito ikiwa ni pamoja na kutoa kauli ambazo baadae hugeuka kuwa visingizio.

Kweli kuna ambao walionyesha ufanisi na ambao wao ilikuwa kuropoka na kuwanyanyasa vibarua kwa kauli zao mbaya na wengine kila leo wakiwa mbele ya vibarua kuwatisha na kujisifu. Mkurgenzi bila kukua kuwa uongozi siku zote ni ushirikiano wa ofisi yake pamoja na vibarua akaanza kutoa maneno ya kejeli kwa vibarua na kuwatisha aliowachagua bila kujua kuwakejeli vibarua ni kosa kubwa kwani wao kwa umoja wao ndiyo waliompandisha hapo.

Baada ya vibarua kuanza kuona mbele si pazuri wakaanza kunong'ona chini kwa chini na hapo baadhi ya wateuliwa na wao wakaanza kurudi nyuma ili wamwachie mkurugenzi nafasi yake. Leo hii mkurugenzi ndiye kila kitu bila kujijua ya kwamba safari wote watafika wamechoka yaani,mkurugenzi,kiranja mkuu,viranja wengine,viongozi wa vibarua pamoja na vibarua wenyewe. Pamoja na kufika huko kiranja atakuwa amechoka zaidi kutokana na yeye kujiona ndiyo kila kitu na hivyo kupelekea viongozi aliochagua badala ya kumsaidia wanakuwa mzigo tena.

Ila nabaki nikimshangaa sana huyu mkurugenzi sababu kabla ya kugombea ukurugenzi alitakiwa kuandaa aina na majina ya viranja pamoja na viongozi ambao wangesaidiana naye, ila cha ajabu leo ni mwezi mmoja na siku bado anachagua viranja na viongozi. Mda anaotakiwa kukaa ofisini ni miezi 5. Hivyo kumebaki miezi 3, sasa lini vibarua wataona mtunda ya huo uongozi mpya? Hii haitofautiani kuchukua mkopo wa biashara ili hali hujui unataka kufanya biashara gani.

Mkurugenzi bado unao mda kidogo usiogope kuanza upya.fanya uamuzi sahihi kwa maslahi ya vibarua na ukifata taratibu za ofisi,weka sifa,ujuaji,visasi pembeni. Shirikiana na viongozi wenzako vizuri. Ubabe,majivuno,dharau zitakukwamisha. Kila mmoja kati ya hao wanaokuzunguka hawajui kesho yao hivyo wanachokifanya ni kukuliwaza kwa maneno matamu ili waendelee kupata mishahara yao


Siyo kila mwenye upara ni anajua mambo yote.


Siyo kila mwenye mvi anakipawa cha kuongoza au ana hekima na busara.

Mkurugenzi anahimiza sana sala. Naomba apitie hapa ,Mithali28:2 : kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi, bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa, 5: watu wabaya hawaelewi na hukumu; bali wamtafutao Bwana huelewa na yote. 9: yeye aligeuzaye sikio lake asiiisikie sheria hata sala yake ni chukizo
Mkuu aliyepungiwa akili uonea watu wake. Mithali 28:16
 
Hamumsapoti lakini mnampromoti kuna siku mtaangaika kumsafisha kama mnavyoangaika kwa EL wekeni hakiba ya maneno
 
kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndo kufanya kosa so UKAWA tunamda mzuri wa maandalizi na na kurekebisha kasoro zote 2020 hatuhangaika kumuokoteza JPM
 
Pole sana siyo kila anayechangia huku mada ni mwanasiasa au ni kada. Hakuna sehemu jf wamesema wachangiaji wawe wanachama wa chama fulani . ila asante ukisikia yowe ujue ...........
Hamumsapoti lakini mnampromoti kuna siku mtaangaika kumsafisha kama mnavyoangaika kwa EL wekeni hakiba ya maneno
 
kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndo kufanya kosa so UKAWA tunamda mzuri wa maandalizi na na kurekebisha kasoro zote 2020 hatuhangaika kumuokoteza JPM
Tatizo siyo ukawa. Elimu kwa wananchi ndiyo inayotakiwa zaidi kwani kinachompa mtu uraisi siyo chama bali ni uelewa wa wananchi juu ya mahitaji yao wanayoyatarajia
 
Serikali ya Raisi Magufuli imekuwa ikifuatilia sana makosa madogo madogo ya wanasiasa na wananchi katika mambo yenye mtazamo wa kisiasa, wakitoa kisingizio kwamba lazima watu wejenge tabia ya kufuata sheria.

Mara nyingi najiuliza kama hii harassment ya polisi kwa wanasiasa na wananchi lengo lake kweli ni kuweka nidhamu ya kutii sheria za nchi au ni suala tu la manufaa binafsi kwa Raisi Magufuli (self-serving).

Basi ikiwa Rais Magufuli ana uchungu sana na watu kufuata sheria, tuna watu wako gerezani walipatikana na hatia za kukata viungo na hata kuua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) hasa watoto wasioweza hata kujilinda, walioua wanawake wazee kwa kisingizio cha uchawi, majambazi walioua raia wasio na hatia nk. Baadhi yao wamehukumiwa kifo, kunyongwa hadi kufa, na kinachosubiriwa ni sahihi ya raisi tu.

Basi kama Rais wetu ana uchungu na matukio ya kuvunja sheria kwa ujumla na sio tu katika ulingo wa siasa kwa manufaa yake binafsi, basi na aweke sahihi watu hawa wanyongwe. Kuweka sahihi ili watu hao wanyongwe ni wajibu wake wa kikatiba ambayo aliapa kuilinda na kuitekeleza.
 
Urais ni taasisi, inayoongozwa na rais. wananchi humchagua rais ili aongoze taifa.

Kwa msingi huo rais anatokana na ridhaa ya wananchi wa nchi husika. na ndo maboss wa rais.

Hivyo ukuu wake, unatokana na wananchi wenyewe kumpatia ridhaa hiyo. ila inaleta ukakasi pale boss wa rais ambaye ni mwananchi anapotakiwa asihoji lolote.

Yaani umwajiri mtu, unamlipa mshahara halafu ukaona hafanyi vyema kazi yake ukawa hauruhusiwi kumhoji chochote.

Je ni sahihi kwa wananchi kumhoji, kumkosoa, kumrekebisha hata kumkaripia rais waliyemchagua na wanamlipa mshahara?
 
Siyo sahihi kumkaripia Rais wa nchi ila ni sahihi kumkosoa, kumshauri, kumrekebisha na kumpinga kwa hoja zenye manufaa kwa taifa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…