Wakati ameingia rasmi kazini baadhi walimshangilia na baadhi kuwa na wasiwasi. Alijitabanaisha angekuwa mkombozi wa vibarua katika ofisi yake. Alichagua kiranja mkuu ambaye hakujulikana sana na kuchagua wasaidizi wa kiranja mkuu ili iwe rahisi. Hapo ndipo wengi waliaanza kugawanyika kwani vibarua walihoji utendaji wa baadhi ya viranja kutokana na wao kuwa viranja katika uongozi uliopita. Vibarua wakajipa moyo huenda amekuja mkurugenzi mpya wataweza kubadilika. Kweli kwa muda wa miezi kadhaa ya mwanzo mkurugenzi pamoja na viranja walionyesha mbwembwe zao katika nyadhifa zao. Baada ya muda mkurugenzi akaamua kushuka chini tena kishirikiana na kiranja mkuu kuchagua viongozi wa vibarua katika maeneo yao wanakoishi. Hapo napo palionekana kama mkurugenzi anatoa fadhila kwa baadhi yao. Walalahoi wakaingiwa na hofu mioyoni mwao ila wakajipa moyo.
Sasa ofisi ikawa imekamilika sababu maeneo yote yanaviongozi pendwa wa mkurugenzi na wanamheshimu na kumnyenyekea.kazi zilianza kwa manjonjo kama wafanyavyo bondia wanapopima uzito ikiwa ni pamoja na kutoa kauli ambazo baadae hugeuka kuwa visingizio.
Kweli kuna ambao walionyesha ufanisi na ambao wao ilikuwa kuropoka na kuwanyanyasa vibarua kwa kauli zao mbaya na wengine kila leo wakiwa mbele ya vibarua kuwatisha na kujisifu. Mkurgenzi bila kukua kuwa uongozi siku zote ni ushirikiano wa ofisi yake pamoja na vibarua akaanza kutoa maneno ya kejeli kwa vibarua na kuwatisha aliowachagua bila kujua kuwakejeli vibarua ni kosa kubwa kwani wao kwa umoja wao ndiyo waliompandisha hapo.
Baada ya vibarua kuanza kuona mbele si pazuri wakaanza kunong'ona chini kwa chini na hapo baadhi ya wateuliwa na wao wakaanza kurudi nyuma ili wamwachie mkurugenzi nafasi yake. Leo hii mkurugenzi ndiye kila kitu bila kujijua ya kwamba safari wote watafika wamechoka yaani,mkurugenzi,kiranja mkuu,viranja wengine,viongozi wa vibarua pamoja na vibarua wenyewe. Pamoja na kufika huko kiranja atakuwa amechoka zaidi kutokana na yeye kujiona ndiyo kila kitu na hivyo kupelekea viongozi aliochagua badala ya kumsaidia wanakuwa mzigo tena.
Ila nabaki nikimshangaa sana huyu mkurugenzi sababu kabla ya kugombea ukurugenzi alitakiwa kuandaa aina na majina ya viranja pamoja na viongozi ambao wangesaidiana naye, ila cha ajabu leo ni mwezi mmoja na siku bado anachagua viranja na viongozi. Mda anaotakiwa kukaa ofisini ni miezi 5. Hivyo kumebaki miezi 3, sasa lini vibarua wataona mtunda ya huo uongozi mpya? Hii haitofautiani kuchukua mkopo wa biashara ili hali hujui unataka kufanya biashara gani.
Mkurugenzi bado unao mda kidogo usiogope kuanza upya.fanya uamuzi sahihi kwa maslahi ya vibarua na ukifata taratibu za ofisi,weka sifa,ujuaji,visasi pembeni. Shirikiana na viongozi wenzako vizuri. Ubabe,majivuno,dharau zitakukwamisha. Kila mmoja kati ya hao wanaokuzunguka hawajui kesho yao hivyo wanachokifanya ni kukuliwaza kwa maneno matamu ili waendelee kupata mishahara yao
Siyo kila mwenye upara ni anajua mambo yote.
Siyo kila mwenye mvi anakipawa cha kuongoza au ana hekima na busara.
Mkurugenzi anahimiza sana sala. Naomba apitie hapa ,Mithali28:2 : kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi, bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa, 5: watu wabaya hawaelewi na hukumu; bali wamtafutao Bwana huelewa na yote. 9: yeye aligeuzaye sikio lake asiiisikie sheria hata sala yake ni chukizo
Mkuu aliyepungiwa akili uonea watu wake. Mithali 28:16