Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mtataka na nauli iwe ngapi mkuu, hebu jipangieni kwanza tuone, Shilingi Mia moja kwa trip ni nyingi sana itawaumiza?
 
Mmepataaa!!sema jingine[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kama nawaona wasukuma wenzangu mtakavokua mnashinda mnazunguka tu kwenye mwendo kasi, kama mlivokua mnashinda kwenye ngazi za rock city mall hadi mkapigwa marufuku!!!
 
Kwa staili hii ya kejeli Na matusi haifai.

Rais kama mwanadamu yeyote hakosi mapungufu basi tutumie busara Na hekima kubainisha basi kwa mwenye akili atatambua kuwa pale nilikosea.

Utaratibu Wa kumuombea uendelee ili atende haki, kwan akiachwa Na akatenda injustice usidhan hutaumia

Huu utaratibu unashika mizizi unakuta matusi Na kejeli ambazo hazihimiliki.

Hakuna kiongozi yeyote awezae kuchukua udhaifu katika kebehi,dharau Na matusi haya.

Let us change for the better no one is perfect except God.


Jf is only place we dare to talk openly but not place to insult others.
 
Huu uzwi ufutwe tuu maana sioni mantiki ya mtoa maada kuituhumu jamii forums bila hata kutoa mifano yenye uhalisia
 
! Mheshimiwa pole na kazi za kila siku.Nakuomba angalia swala La wazabuni kwenye taasisi za serikali hasa mashuleni kinachofanyika ni wizi uliobarikiwa kupitia GPSA .Yaani unaibiwa kuliko unavyofikiria.Mimi ni mwalimu huwa roho inaniuma sana jinsi tunavyonunua vitu kwa wazabuni kila kitu bei ni Mara mbili ya kila kitu sasa hapo ni hesabu gani tunafanya? Ushauri wangu;watu waliopewa kusimamia taasisi hizo wape idhini ya kufanya manunuzi kama ulivyo waamini ili atakayeshindwa upate nafasi ya kumshughulikia.Mheshimiwa Rais naomba Fanya hivyo hawawezi kuiba wamenyooka ili tuondokane na huu mchwa(wazabuni) wanaokula pesa za watanzania kwani hawana tofauti na acacia.Nakuomba tena shughulikia hili utaokoa pesa nyingi na kukaa kila Sikh wanasema wanaidai serikali "wizi mtupu" nikipata nafasi naweza kuongea nawe ana kwa ana nikakueleza madudu yanayofanyika.MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA
RAIS JOHN JOSEPH POMBE
MAGUFULI

kwanza kabisa kwa heshima na taadhima
mheshimiwa Rais nikuombe radhi kwa
uvumilivu ulionao dhidi ya watanzania wasio wakweli na wanaotuhumu kwa kila
jambo liwe baya au zuri unalolifanya..
Mheshimiwa Rais, wewe ni binadamu
kama tulivyo wengine na una
moyo..tunajua unaumia sana pale
unapofanya jambo zuri kwa manufaa ya walio wengi hasa watanzania masikini
ambao wengi wao ndio waliokupigia
kura...kwa hilo mheshimiwa tunakupa
pole nyingi.

Mheshimiwa Rais, watanzania
wanatakiwa watambue kuwa nawe una familia..hivyo wanapokupa stress,
inaathiri hata familia yako..tunakuomba
sana uwe mwenye kusubiri kwani
naamini ipo siku wale waliokuwa
wanabeza na kutoa maneno yao
yakukera hata kukufanya usiwe na raha wataumbuka..na kuaibika mbele ya
macho ya watanzania..kwasababu
tunaamini yote uyafanyayo mazuri ni kwa
nia iliyo safi kulikomboa Taifa letu
lililokuwa limebaki mifupa tu..wajanja
walitafuna nyama yote..

Mheshimiwa Rais,kwa muda wa miaka
michache tangu umekuwa mteule kupitia
mungu kwa kuchaguliwa kuwa
Rais..tumeshuhudia ukifanya mambo
mazito bila kuogopa mtu yeyote..awe
mtanzania au Taifa lingine..kwakweli umejitoa nafsi yako na moyo wako wote
muwatumikia watanzania..tumeona
ukipambana na maovu pale
bandarini, umepambana na
wanaotorosha madini kupitia
mchanga, umeondoa kero za rushwa na ufisadi ambazo zilikuwa zimekomaa
katika ofisi za umma, umepambana na
watumishi hewa..na kila lililowezekana
mbele yako umelifanya bila simile ili
kuleta ukombozi katika Taifa letu..

Mheshimiwa Rais, nakufananisha na viongozi wawili tu katika Tanzania
ambao waliwahi kujitoa kwaajili
yetu..Sitamsahau Edward Moringe
Sokoine, na Marehemu baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere..wewe ni wa tatu kati ya viongozi waliowahi kuleta chachu katika
Tanzania..Mungu akubariki sana.

Mheshimiwa Rais, bado una safari
ndefu..na kumbuka unahitaji viongozi
wenye mlengo wako ili ndoto zako
zifanikiwe..kwa hilo sina shaka nalo sana kwani umekuwa ukiwatumvua wale wasio
na mlengo wako..hiyo ni nzuri na ndiyo
inayokuongezea alama zaidi katika imani
zetu watanzania..tulishuhudia
umewatumbua hata marafiki zako wa
karibu walioonesha kuvurunda katika utawala wako..baba usiache hilo..ikitokea
we tumbua tu mpaka wale wenye nia safi
wataonekana..bora ubaki na watu
wachache lakini wenye mlengo wako..
Mheshimiwa Rais, umekuwa fair sana
kwa hata wapinzani..wale walioonekana ni dhahabu umekuwa ukiwachukua na
hawakuangushi..kumbe hata upinzani
kuna ambao wanakubali kuwa wewe ni
Rais wa wanyonge na hawakusita
kukuunga mkono na kukusaidia kazi..Si
haba.. wateue baba kama uwezo wanao na umewaamini wape nafasi..

Tanzania ni yetu sote na kila mmoja anahaki ya
kupewa nafasi alitumikie Taifa lake bila
kujali itikadi zao..

Mheshimiwa Rais wangu,kuna jambo
nataka nikwambie leo hii..kama mtanzania naomba niseme..mimi ni
mzalendo..naomba nikupongeze kwa
kuwajali wasomi..hili ni jambo kubwa
sana katika historia ya Tanzania..wasomi
walidharaulika sana, walifichwa
,walikebehiwa, walisengenywa, wa litukanwa, walifanyiwa kila lililobovu..ila
baba tangu umeingia madarakani..ume
thamini na kuwapa nafasi kubwa sana
katika Taifa hili..nchi yoyote
hukombolewa na watu walioelimika,wa
kizuiwa na kudharauliwa hakuna jema litakalofanyika..Maofisi mengi yalijaa
watu wasio na sifa.. ndio maana hata
utendaji kazi ulikuwa dhaifu,watu
walifanya kazi kwa mazoea na
kujuana..na point hii imenigusa na
kunifanya leo niandike barua hii kukupongeza kabla mwaka
haujaisha..umesafisha ofisi zote
watumishi fake..nimeipenda sana staili
yako hii ya kujali na kuwatambua
wasomi..umewapa fursa ya kuonesha
talents zao..

Mheshimiwa Rais wangu, nakuombea
maisha mrefu, mungu akulinde na akupe
afya bora wewe na mama yetu
Janeth..mwambie tunampenda sana,
aendelee kukunongoneza matatizo ya
walimu..tunae mama mwenye subira, mpole na mwenye unyenyekevu dhidi ya
watanzania..tunampenda sana Mama
Janeth..Mungu ampe afya tele aweze
kukuhudumia Rais wetu mpendwa.
Ameen..!!
 
Kimsingi sifa zote ninazo mpaka za kuwa Rais. Mtukufu hizo wizara tajwa zimepwaya kabisa ningefurahi ukanikonsida Mimi Fukara niliyetupwa jalalani huku mikoani Bw. Deogratius Nalimi Kisandu ili niweze kuitumikia Serikali yako. Niteue kwa miezi Sita tu halafu unitumbue na ufanye ulinganifu na mawaziri tangulizi. Nipe Wizara kamili bila Unaibu maana ukinipa unaibu Mawaziri wako watanitenga kama walivyopanga ukiniteua.

Najua fika Mh. Rais hunitaki kabisa na unanichukia sana maana wamekupandikiza chuki vizuri sana wapinzani wangu. Pia Rais Mimi sijawahi kukanyaga Ikulu kwa hiyo huyo uliyetambulishwa sio Mimi ni FEKI.

Mtukufu Rais huu sio utani hebu nitoe machakani, ikiwezekana niteue hata Makamu wa Pili wa Rais nikunyooshee Nchi.

Salimia pia familia yako, nimeamua kujipigia debe mwenyewe, Mimi ni ka mwalimu tu kakawaida Mkolani sekondari Mwanza ila hapa sasa nipo Kahama nyumbani na uguza afya yangu.

Ili usipotoshwe tunaweza kuchati Inbox nikakupa namba yangu.

Uwe na kazi njema Mh.Mtukufu Rais.

Ndimi,
Deogratius Nalimi Kisandu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…