Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
ushauri kwa baba janeti kwa dakika zilizobaki kuelekea 2020.
1. aachane na swagga zingine na kujikita katika usambazaji wa umeme vijiji vyote.
2. alipe kipaumbele swala la katiba ya walioba.
3. aangazie swala la uhuru wa habari na kujieleza.
akiweza haya mkeka wake hauchaniki 2020.
 
ahahahahaha anashika kwa mkono anatupia golini 🙂
Refa anaweka mkpira kwenye penalty box, mpira unabebwa... Refa hapulizi kipenga, jamaa anatembea nao mpaka golini.... Halafu utasikia na raa wanashangili
 
Refa anaweka mkpira kwenye penalty box, mpira unabebwa... Refa hapulizi kipenga, jamaa anatembea nao mpaka golini.... Halafu utasikia na raa wanashangili
ni Tz tu utakuta aina hii ya democrasi yani ni kama tom na jerry
 
Hata asipofanya kitu kushinda kupo pale pale siamini kama kunauchaguzi huru africa mashariki wao wajanja wakuongeza sifuri wakipata 100 +0= 1000
 
Awaongezee posho wakina lizabon,jingalao, jeshi la polis,tume ya uchaguz na mahakama huo ndo msingi wake uliobaki.
 
Wakuu.
Rais anaweza kua na nia njema na wakulima mkoa wa kigoma kama alivyotangaza kwenye vyombo vya habari alipohutubia hadhara katika uwanja wa umoja kasulu.
Aliwaeleza wakulima walime pale kagera nkanda cha ajabu vyombo vya dola vinawanyanyasa na kuwatesa wakulima wale bila aibu,
 
Tukiacha unafiki na tukasema ukweli kama mh Raisi anavyosisitiza, kweli ameanzisha Mambo mengi yenye kuwasha masikio na kusisimua miili yetu lakini karibia yote yanafeli kutokana na ukurupukaji na kutokua na mipaka na miongozo inayompa mwelekeo.

Tujikumbushe haya aliyoanzisha na kufeli:

SAMAKI WA KAGUFULI,

NYUMBA 70, MASAMAKI NA WENZAKE,

MANJI NA MAJEZI YA JESHI,

ACACIA NA MAKINIKIA,

TANZANIA KUA DONA COUNTRY,

MILLION 50 KILA KIJIJI,

Haya Ni baadhi tu ya yale aliyoanzisha na kushindwa Kwa Muda mfupi sana alioingia MAHALA patakatifu.

Namuomba Mh Raisi, wimbo wa msemakweli Ni mpenzi wa Mungu sasa auimbe kwa vitendo kama anavyojua IMANI bila MATENDO imekufa, Ni wakati sasa wakujitengenezea heshima ya kweli. Mtauliza afanyaje sasa atengeneze hiyo heshima? Jibu;

ARUDISHE MCHAKATO WA KATIBA MPYA.

Katiba yenye kipengere kinachosema;

HATA KAMA NI RAISI HURUHUSIWI KUAMUA KWA UTASHI WAKO JAMBO LOLOTE, LENYE MASILAHI KWA TAIFA BILA KULISHIRIKISHA BUNGE, WATAALAMU WENYE UELEWA WA JAMBO HILO PAMOJA NA WANASHERIA.

karibu msaidie raisi kujitengenezea heshima.

moods wenye mitazamo ya kina Jerry Muro hawachelewi kufuta uzi kama juu.
 
Hakuna Nchi Dunia hii iliyowahi kuandika Katiba mpya bila ya tukio kubwa kutokea, hivyo Tanzania hatuna haja ya kuandika Katiba mpya, bali tunaweza kuboresha iliyopo kama kuna haja ya kufanya hivyo!
 
Nikupongeze mh rais katika uteuzi ulioufanya leo hii,hapa kidogo katika uteuzi wako wa ma rc ungefanya mabadiliko huyo mnyate ungemleta dar na rc makonda angekwenda arusha huyu makonda anafaa zaidi arusha baada ya kufanya kazi kubwa ya kuliletea maendeleo na ulinzi na amani jiji la dar es salaam sasa ingekua ni zamu ya arusha na mnyate angeingia dar es salaam nafikiri angepata uzoefu zaidi

Natumaini ushauri wangu utaufanyia kazi muda si mrefu!
 
Miaka miwili sasa Tangu Raisi achaguliwe.
Kuna nambo mengi yamepita kwenye kipindi hiki ambayo yamegawanya maoni ya wengi.

Kuna ambao wanaona ni Chanya na wengine kuona kama ni muendelezo ule ule wa chama tawala waliofanya kwa zaidi ya miaka 50.

Watanzania wengi wana imani ya kukombolewa kiuchumi na Raisi huyu Na yeye amejigamba kwamba atawavusha watu kwenda kwenye nchi ya asali na Maziwa.

Maoni nitayaelekeza kwenye mfumo wa kodi.

Uingereza:

Nilichojifunza kwa hawa wakoloni wetu ni kwamba kampuni kubwa huwa zinalipa corporation tax kidogo. Mfano Uber, Macdonalds, Google etc. Hawa Mabwana wakubwa wanalipa tax kidogo sana, ila wanaajiri watu wengi sana.

Mfano: Uber ana madereva 40,000 jijini London. Kwa Wastani Dereva wa Uber
Watumia lita kati ya 80 hadi 100 za mafuta, iwapo serikali inachukua senti 40 Pound kwa kila Sasa ukichukua 40,000*80*0.40*52 = £66,560,000 wastani kwa mwaka, hii ni kwenye ushuru wa mafuta ya petroli tu. Hapo bado kuna Tyre, vipuri, oil n.k

Madereva wanalipa wastani kati ya £100 na £200 income tax kwa wiki. 40,000*100*52 = £208,000,000.

Hapo unaona Uber inaweza kuwa inalipa very low Corportion tax ila indirect wanaiingizia serikali ya Uingereza zaidi ya Milioni 270 za Pound kwa mwaka.

Hapa kwetu:

Msimu uliopita kulikuwa na kampuni zilizokuwa zinasafirisha mizigo kwa ndege UK to TZ. TRA walikuwa wanalipisha mizigo kwa kilo. Mimi nilikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni.

Kwa mawazo ya haraka hataka unaweza kusema tulikuwa tunalipa kodi kidogo, lakini tulikuwa tunaingiza zaidi ya kilo 1000 kila wiki hapa nchini, mizigo yetu mara nyingi ilikuwa bi Perfum, Make UP, Vipuri vya magari n.k

Wastani wa kodi ilikuwa ni kwenye 2m to 3m a week. Kwa sababu tulikuwa tunalipa kodi kidogo na sisi tukawa tunawacharge wateja zetu shipping kidogo na wao wanawacharge wateja zao kidogo.

Sasa awamu ya 5 ilivyoanza TRA wakabadili mfumo, badala ya kilipa kwa kilo wakawa wanatulipisha kwa Thamani ya mzigo. Hii ikafanya bishara iwe ngumu ngumu kwa sababu kodi ikatoka kwenye 2/3 mil na kuwa 7/8. Wateja zetu ilabidi wapandishe bei ya bidhaa zao mara 3 ili kukava cost zetu.

Mwisho wa siku sisi sote tumefunga Biashara. Tulikuwa na wateja 10 ambao walikuwa na Wastani wa wafanyakazi wa 3. Sisi tulikuwa na vijana kama 10 walikuwa wanatusaidia kusabaza mizigo.

Hapo unaona Swissport na TRA wanepoteza 3/4 mil a week na vijana kama 40 wamepoteza Ajira. Wenye nyumba 10 wanakosa kodi, halmashauri zinakosa kodi, Tanesco inakosa pesa. Kuna gari tulikuwa tumeikodi kusambazia mizigo mwajari wake anakosa pesa, mafuta, vipuri n.k

Tunakuomba mhe Raisi usaidie kuangalia suala hili la Kodi, Mtu unaweza kuwa unalipa initial kodi ndogo lakini biashara unayoifanya inaweza kuwa na inaingiza pesa nyingi Serikalini na pia ina mchango mkubwa kwenye jamii.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom