Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Well said mkuu, tatizo huyu bwana kakua akichunga ng'ombe kwa hiyo ana knowledge ya kutawala na si kuongoza thus why walisema anafaa zaidi kuwa mnyapara
 
Utu mnaoutaka mliutumia vibaya dhidi ya JK ...
JK aliwapa utu mkamuita dhaifu na mkamtukana sana ....TUSIWE WANAFIKI ...
Nani aliyenyimwa uhuru wa kukosoa?
Nani aliyenyimwa kupata taarifa?
 
Utu mnaoutaka mliutumia vibaya dhidi ya JK ...
JK aliwapa utu mkamuita dhaifu na mkamtukana sana ....TUSIWE WANAFIKI ...
Nani aliyenyimwa uhuru wa kukosoa?
Nani aliyenyimwa kupata taarifa?
Nani mwenye mamlaka ya kuamua how mtu mwingine atumie Uhuru wake? Unajua why tulipigania uhuru?
 
kuna awamu nne za wahitimu walimu shule za misingi, na kila mwaka wanaongezekaa mkuluu futa basi haya mafunzoo watoto wa masikini wanauza mashamba wanaenda kusoma , wakirud ajira hakuna na mali za nyumban zimeishia chuoni!!, kwa hili unafanyaakosa saana ,
 
Salaam Ndugu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Nikiri kwamba miye Frey ni mwanachama wa kawaida wa chama cha Mapinduzi nisiyekuwa na madaraka yoyote ndani ya chama na Dola.
Ujumbe wangu kwako Ndugu Mwenyekiti.
Ninaomba uwahimize waheshimiwa mawaziri na viongozi wengine wa dola kutoa majibu na ufafanunuzi kwenye Social Media ya upotoshaji ya kazi mbalimbali za serikali na wizara zao unaofanywa na wanaharakati na watumiajji wa mitandao Kama walivyo Fanya bungeni wiki hii.
Ndugu Mwenyekiti upotoshaji mkubwa unaofanywa kwenye mitandao ya kijamii inahusu sana sana utendaji ndani ya dola lakini cha kushangaza hao mawaziri na viongozi wengine wa serikali wako mitandaoni tena wakipost mambo yao ya kikazi na binafsi lakini inapokuja suala la kujibu hoja ya watumiajji mitandao wako kimya kana kwamba haiwahusu.
Nitumie fursa hii pia kuwaomba viongozi wangu wa Chama kuanzia Secretariat na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kushauriana na Mwenyekiti na Mh Rais kuona huu umuhimu.
Asilimia kubwa ya vijana wako kwenye Social Media na ndiyo wahathirika wakubwa wa uwongo mitandaoni.
Asante Mh Rais kwa kupokea maoni yangu.
Mungu akubariki sana kwa kazi njema unaifanyia Watanzania.
 
Mkuu, kwanza naunga mkono hoja!, ila ninaswali dogo kwako, kwa vile umetolea mfano wa kilichofanywa na Bunge wiki hii, naomba utusaidie akina sisi ambao hatukufanikiwa kuona kilichofanywa, ni hoja zipi Bunge limezijibu?.

Hili la serikali usikae kimya ijibu hoja naungana na wewe na mimi nimekuwa nikilipigia kelele sana, ila tofauti na wewe, unataka serikali ijibu hoja za kwenye mitandao ya kijamii!, kwa uwezo gani?, hata serikali ya Marekani ambayo ni super power ina kila aina ya uwezo, haiwezi kujibu hoja za kwenye social forums!.

Mimi hoja yangu ni serikali ijibu hoja za kwenye media na mifano ni hii
Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, Nchi Yako Inatukanwa!, Rais Wako Anatukanwa!, Tumenyamaza!. Huu Ni Uzalendo Gani?!.

Jarida la Economist Lilianza Zamani na Nilieleza Humu.
‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
nilisema baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni. Tulikaa kimya bila yoyote kukanusha popote!.

Kuhusu Udikiteta Tanzania, SABC Wakafuatia
Mimi kama mwandishi, kazi yangu ni kusema na kuandika tuu. Baada ya Taarifa hiyo ya SABC nilisema kitu humu Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta!
Nikasisitiza Uzalendo wa kweli ni kutokubali na kutonyamaza kimya wakati rais wako anaposemwa vibaya kwa hoja za uongo na media za nchi nyingine, bali ni kwa viongozi wetu kujitokeza kwenye media zetu kuukanusha huo uongo kuhusu udikiteta kwa kuusema ukweli na ikibidi serikali yetu sio tuu ikanushe bali pia ihitaji kuombwa radhi na ikibidi hata tudai fidia!. Hata Kikwete aliposingiziwa kuhongwa suti na Marekani, nilitoa hoja hii Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!, na Ikulu yetu iliingilia kati.

Jee Rais Magufuli ni Malaika Mtakatifu, Yuko Perfect. Hakosei?
Pamoja na matatizo yake yote na mapungufu ya kibinadamu ya rais wetu Magufuli, kwa sababu na yeye ni binadamu tuu kama sisi na sio malaika, hivyo anaweza kabisa kukosea. Pale rais wetu anapokosea na kusemwa vibaya na kwa ukweli kuhusu makosa yake, itabidi tukubali tuu, akubali kukosolewa na sisi tuwe wavumilivu, tuwe wadogo tuu. lakini Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi yetu, kamwe tusikubali rais wetu kudhalilishwa kwa kusemwa vibaya, kwa kusingiziwa vitu vya uongo na media za nje bila ya media za ndani na viongozi wetu, kukanusha na kumtetea, au kuunyamazia udhalilishaji kama huu ni sawa na kushangilia rais wetu kudhalilishwa. kitendo cha kuuacha uongo kama huu kuendelea, ndiko kunakopelekea uongo huu sasa kuanza kugeuka kama ukweli, na mwisho wa siku utageuka ukweli kabisa, na kitakacho fuata ni vilio na kusaga meno, and that time ikifika, hata sina uhakika kama tutakuwepo to tell the story, tutakuwa ni tayari...siku nyingi!.

Jarida la Africa Confidential Likaita Serikali yetu "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Jarida la Africa Confidential toleo la 58, story number 20 lililochapishwa Oktoba 6, 2017,
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!
Haya sio maneno mazuri kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ushindi halali katika sanduku la kura, kupitia uchaguzi ulioendeshwa na 'Tume huru ya Uchaguzi', hivyo uchaguzi ulikuwa ni 'huru na wa haki' hivyo matokeo ni 'halali' na nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata misingi ya katiba, na kuheshimu utawala wa sheria.

Kwa Nini Serikali Inakemea Uongo wa Media za Ndani na Kufungia lakini Media za Nje iko Bubu?.
Ikulu yetu, Waziri Mwakyembe na Idara yetu ya Habari, tusikalie kuyafungia tuu magazeti ya ndani kwa kutoa habari za uongo, au nyingine ni za kweli msiopendezwa nazo, huku tukikaa kimya wakati habari za uongo kuhusu nchi yetu zikienezwa na media za nje!, zinazowafikia mamilioni?. Habari yoyote ambayo sii ya kweli, kuihusu Tanzania na rais wetu, ikitolewa media yoyote, tusikae kimya, ikanushwe!, vinginevyo itaonekana ni kweli!. Ile filamu ya mapanki iliyochezwa kituo cha TV cha Aljeeza, JK alikuja juu tukapinga. Wachina waliposingiziwa kubeba pembe za ndovu, tulialika waandishi wao na kukanusha!. Hili la udikiteta, kwa nini hatukanushi au ndio ukweli wenyewe?.

Jarida la Economist Laishukia Tena Tanzania!, Laitukana Nchi Yetu, Lamtukana Rais Wetu.
Ni muda sasa jarida la The Economist limekuwa likiisema vibaya nchi yetu, na kumsema vibaya rais wetu, ikiwemo kumuita majina ya ajabu ajabu, mimi nikiwa ni mwandishi wa habari, kanuni kuu nambari moja kwa mwandishi wa habari, ni kusema ukweli daima, hivyo sina tatizo kabisa na chochote kitakachoandikwa kwenye gazeti au media yoyote, kuihusu nchi yetu Tanzania, au rais wetu Magufuli, kama kitu hicho ni cha kweli, lakini natatizwa sana na uongo wowote unaoandikwa kwenye magazeti na majarida ya kimataifa, likiwemo jarida hili la The Economist, kwa lengo la kuhadaa ulimwengu kwa kutoa story na propaganda za uongo kuhusu Tanzania na rais wetu, na kuzieneza kimataifa zisambae dunia mzima, wanaoujua ukweli kuhusu haya yanayosemwa ni sisi Watanzania, nchi yetu inatungiwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anatungiwa na kusingiziwa uongo, tumenyamaza!, rais wetu anapachikwa majina ya ajabu ajabu, dikiteta, dinasauria wa Dodoma, na sasa ameitwa rogue, tumenyamaza!, rais anadhalilishwa na kutukanwa huku sisi tumenyamaza!, huu ni uzalendo gani?!.

Kuna wanaoamini kila kinachosemwa na media za nje kuhusu Tanzania ni kweli, na kila kinachosemwa kumhusu rais Magufuli ni kweli, huo ni mtazamo wao kutegemea na uwezo wa uoni wa jicho lao, linaona vipi, kuna kitu mmoja anaweza kukiona ni sawa, na mwingine akakiona sii sawa, mimi kwa upande wangu, naona hii sii sawa kwa nchi yetu kusemwa vibaya na rais wetu kuzushiwa uongo na kusingiziwa uongo.

Kwa vile uongo huu unasambazwa kimataifa na huku sisi Watanzania wenyewe tumenyamaza bila kuukanusha, matokeo yake sio tuu, jamii ya kimataifa, utauamini uongo huo, bali hivyo ndivyo itakavyo tuelewa na hivyo ndivyo itakavyo muelewa rais wetu, bali uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, uongo huo hugeuka kuwa ukweli!. Hii tabia ya kusikia uongo na kuunyamazia, kunaweza kabisa kupelekea haya ya uongo yanayosemwa sasa, kuja kuwa ya ni ya ukweli na yatakuja kutokea Tanzania kwa siku za usoni!, ni mpaka pale yatakapokuja kutokea, ndipo watu watalia na kusaga meno!, tena wakati huo ukifiki, it might be too little too late.

The Economist walianzia hapa ‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"
Tukanyamaza, sasa wameibuka tena na uongo mwingine
Tanzania's rogue president - Democracy under assault - The Economist

Katika report hiyo, wamemtukana rais wetu kuwa Rogue President. Kwa vile mimi sijui Kiingereza, ilinibidi nikatafute kwanza kamusi kuangalia neno rogue maana yake ni nini, mtu anaeitwa rogue ni mtu wa namna gani, na taifa likiitwa rogue state ni taifa la namna gani, naomba kwa heshima ya rais wetu, nisitoe tafsiri ya neno hilo, ila kwa kifupi ni kuwa, rais wetu ametukanwa!.

Kwenye report yao, japo kuna mambo machache ya kweli kuhusu Tanzania, lakini pia wamechomekea mambo mengine mengi ya uongo kumhusu rais wetu na hoja za udikiteta ambazo inabidi zikanushwe.

Hii ni Makala toka jarida la The Economist, linamsakama sana Rais Magufuli, katika Makala hii, linahamasisha rais Magufuli adhibitiwe kwa kuwekewa vikwazo vikali kabisa kiuchumi.
How to save Tanzania
hawa watu wanamuita rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kuwa ni an authoritarian and erratic president who is transforming a stable, if flawed, democracy into a brutal dictatorship.

Ni haki kweli kumuita rais wetu, an authoritarian na erratic president na kumtuhumu kuwa ana transforming a stable, democracy into a brutal dictatorship?. Kuna ukweli wowote hapa?. Hawa watu hivi ndivyo walivyoiambia dunia kuhusu Tanzania, kweli hivi ni vitu vya kunyamazia?.

Wakati haya yakisemwa, wiki hii hii, ndio hii wiki, waziri wetu wa habari, na naibu wake wako busy kumshupalia Diamond, mwanamuzi kijana mdogo anayejituma, hadi kufikia kiwango cha naibu waziri kufanya mahojiona ya kujidhalilisha, na Diamond akajibu mapigo kwa kumdhalilisha zaidi!.

Waziri Prof. Mwakiembe, Naibu, na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Dr. Abasi, fanyeni press conference mjibu hoja serious kama hizi zinazohusisha reputation ya taifa letu kimataifa na sio kujikita kwenye trivia issues za sanaa, mambo ya sanaa, waachieni Basata, nyinyi mjikite kwenye serious policy issues, inchi yetu inadhalilishwa kwa hoja za uongo kuhusu udikiteta, nyinyi mnadiscuss nyimbo za Bongo Flava, sijui wamevaaje etc, this is nonsense!.


P
 
Watapingaje ikiwa kuna ukweli hoja hujubiwa kwa hoja ndio maana wanaogopa hamna aliyetayari kupoteza tonge lake.
 
Serikali ya Tanzania inaweza kuongeza kipato kutoka kwenye mitandao ya kijamii ikiwa tu itaanzisha utaratibu wa kuwakata kodi watumiaji wote wa mitandao hiyo kila siku. Inaaminika hapa Tanzania kuna watumiaji wa mitandao ya kijamii milioni 14 kwa siku(14,000,000), hizi takwimu sio, rasmi lakini ikiwa zitafanyika takwimu rasmi idadi hii inaweza kuwa kubwa zaidi.

Ikiwa Serikali yako itaamua kuanza kukata kodi ya sh. 200 tu kwa kila mtumiaji wa mitandao ya kijamii kwa siku, TRA itakusanya sh. 84,000,000,000 (Bilioni 84) kwa mwezi, na kwa mwaka itakuwa sh. 1008,000,000,000 (Trilioni 1 na bilioni 1). Hii ni pesa mingi sana ambayo kama ikikusanywa itaweza kuisaidia Serikali katika kupata pesa za kujenga nyumba za waalimu nchi nzima. Kwa mahesabu haya ya haraka haraka, utaona kuwa hii mitandao ya kijamii ni "migodi" iliyolala.

Mfano ikiwa kila nyumba moja itajengwa kwa sh. 50,000,000 (Milioni 50) basi kwa mwaka zitajengwa nyumba 20,160 nchi nzima na baada ya miaka 5 zitakuwa zimejengwa nyumba 100,800 na hapa tutakuwa tumeondoa tatizo la nyumba sio tu kwa waalimu, bali pia kwa askari polisi, askari magareza, madaktari na wanajeshi wetu. Tena tenda hii ya ujenzi wa nyumba hizi wapewe wanajeshi kama walivyopewa ile tenda ya kujenga ukuta wa Mererani. Na uzuri ni kwamba watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaongezeka kila mwaka na hawapungui.

Mheshimiwa Rais Magufuli, nakuomba ulichukue hili wazo na ulifanyie kazi haraka iwezekanavyo kwani huku kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Youtube, Instagram, JamiiForum, snapchat, n.k watumiaji wake, wengi wao wanapesa za kuchezea tu na hazina kazi maalumu. Kuna watu wanashinda kwenye mitandao ya kijamii siku nzima wakipost "ujinga" tu na kutukana wenzao, hivyo itakuwa bora sana kama wakianza kulipia "kodi" maalumu ya kutumia mtandao hiyo kwa siku. Sidhani kama Sh. 200 itakuwa nyingi sana kwa mtu kushindwa kulipia. Mimi binafsi nipo tayari kulipia hiyo Sh. 200 kwa siku.

Mheshimiwa Rais, nchi hii itajengwa na Watanzania wenyewe na hii ni mbinu mojawapo ya Watanzania kuchangia katika ujenzi wa nchi yao. Mitandao ya kijamii siyo chakula wala siyo maji, hivyo atakayeshindwa kulipa hiyo kodi hawezi kufa wala kudhurika kwa namna yoyote ile.

By Son of Gamba.
 
Museven anakata shilingi ngapi kwake?
 
Nasikia kuna wanaume wakiishiwa kabisa mipango; wanakuwa tayari kuwakodisha wake zao!!

Hakuna kitu kibaya kama akili ya mwanaume kugota na kuishiwa ujanja wa kiume!!

Ndo hapo, wakikutana wenyewe kwa wenyewe, wanaweza kushauriana kufanya hata yale yaliyo haramu kuu kufanywa hata na dada zao!!

Mungu, zinusuru bongo zetu!
 
Siyo kila huduma unatoza makodi, utawafanya wananchi warudi kuishi enzi za stone age

Badala uje na vyanzo vingine vya mapato wewe unawaza kutoza kodi hata huduma za msingi za raia.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…